Kwanini wanaume wengi hufeli swali hili wakitongoza?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,722
109,263
Wanaume wamekuwa wakijifanya ni mabingwa kama siyo majabali wa kutongoza lakini mara baada tu ya ujio wa simu za mkononi hakika zimekuwa ni kama ni mateso makubwa kwao.

Nalisema hili kutokana na kwamba unaweza kumkuta mwanaume anapambana au anahangaika kuipata namba ya mwanamke fulani ambaye hajuani nae au labda namba yake kaipata tu kwa mtu ili aanze kumtongoza kwa simu ama kwa kumpigia au kumtumia meseji lakini imekuja kujulikana kuwa hakuna mtihani mgumu au swali gumu ambalo wanaume wengi hukumbana nalo na ambalo wengi wao hushindwa kulijibu na hatimaye kujikuta wanajichanganya na wanamkosa huyo mwanamke.

Utakuta mwanaume anaanza kujitutumua kwa kuwasiliana na huyo mwanamke lakini akiulizwa tu swali hili " je namba yangu umeitoa wapi au kakupa nani? " wengi wao hukata tamaa kabisa na hata kuishiwa tena nguvu za kuendelea kuwasiliana na yule binti au mwanamke kwani hakuna swali ambalo wanaume wengi hawalipendi na hawaliwezi kulijibu kama hilo.

Labda leo tupate uzoefu kutoka kwa wanaume ambao naamini humu mpo wengi ni kwanini wengi wenu pamoja na jeuri zenu zote mkiulizwa tu hilo swali tajwa hapo juu huwa mnajiumauma na hatimaye kusepa na kuishia kulalamika tu?

Na je unadhani majibu sahihi ya kumjibu mwanamke ambaye hujuani nae halafu umepata tu namba yake kwa mtu na unataka kumtongoza endapo atakuuliza hilo swali kuwa " namba yangu umeitoa wapi au namba yangu kakupa nani? " ni yapi au ni lipi?
 
Alituma applications fulani chuoni then nikaona picha nikampenda.

Basi siku moha nikapiga nikamwambia nimekosea namba. Siku nyingine tena hivyohivyo. Basi ikawa mwanzo wa mawasiliano na mahusiano.

Swali likaja siku moja akakomaa, namba ulipata wapi? Hahah anakulaga kiswahili mpaka kesho na sina mpango wa kumwambia.
 
Ah mimi ndio maana huwa napenda kuwaibukia na kuwaomba wenyewe. Na bahati nzuri sujawahi kunyinwa namba na siku nikinyimwa nitaacha kabisa kuomba namba

Mwenzetu unaonekana huwa unaoga maji ya baharini kila siku kwani kwa upande wangu kwa wastani tu kwa mwezi nikimsimamisha Mwanamke au Demu kama 37 ambao huwa nabahatisha tena nayo ni kwa taabu sana kupata namba zao kutoka kwao wenyewe ni wawili tu. Nipe siri kuu ya mafanikio yako mkuu.
 
Back
Top Bottom