Kwanini watu hufeli mahusiano kila wanapoanza upya?

Zemanda

JF-Expert Member
Jan 10, 2021
5,707
11,956
Mahusiano ya kimapenzi ni sehemu nyeti sana ya maisha ya mwanadamu na ndipo sehemu kubwa ya Maisha hufanyika au ni muda mwingi huwa tunatumia katika kufanya maisha yetu.

Kuna watu wanaopata nafasi ya kupata mahusiano ya kudumu muda mrefu ambayo huwapa nafasi ya kuambatana na mtu m'moja katika maisha ya ujana hadi uzeeni.

Ila hili swala halipo kwa kila mtu. Kwa wengine mahusiano ya kudumu ni ndoto ya kusadikika na hakuna matarajio ya kuyapata kwa sababu mbali mbali.

Leo nitaweka sababu kwann kuna watu hawana bahati au fursa ya kufurahia mahusiano ya muda mrefu na kudumu na wenza kwa uaminifu na kuwa na amani ya mahusiano hadi uzee.

Zifuatazo ni sababu kwann kuna watu hawafanikiwi kimahusiano:

1. Malezi ya mzazi m'moja: hapa niwe specific, malezi ya kulelewa na mama tu, hufanya kijana au binti kuona mapenzi ni pahala pa kupita tu ila maisha ni mtu kuwa mwenyewe. Kama ni mtoto wa kiume then kumuona mama bila baba ina mnyima nafasi ya kuelewa namna ya kumtreat mwanamke na hivyo kufeli kujua namna ya kuishi na mwanamke na kujua wajibu wa mume kwa mke.

Kama ni mtoto wa kike kuona Mama akipambana mwenyewe inampa sababu kuwa hakuna haja ya kuwa na mwanaume sababu mama hajawahi kuwa na mwanaume mimi nitaishije na mwanaume nataka kuwa kama mama.

2. Kutojifunza kutokana na makosa: kuna mtu makosa anayofanya kwa tabia zake kwa mwenza wake anahama nazo na kwenda nazo kwa mtu mpya. Kiburi hiki cha kuhisi yeye yupo sahihi huwa kinakuwa sugu na kumnyima nafasi ya kujifunza ili kujirekebisha. Matokeo yake kiburi kinakomaa na kuona mwenza anayekutana nae ndie mwenye shida kumbe yeye ndie tatizo.

3. Tamaa: kuna kuhitaji kitu na kutamani kitu. Mahitaji na tamaa ni vitu viwili tofauti. Mahitaji ni vitu ambavyo hatuwezi kuishi bila kuwa navyo ila tamaa ni vitu tunaweza ishi hata tusipopata. Kwa sasa watu wengi wamewekeza fikra kwenye tamaa na kutaka wenza wao wawapatie kile wanatamani hata kama kipo nje ya uwezo na hii huharibu maelewano. Kuendekeza tamaa si jambo zuri.

4. Poor Communication skills: kuna watu wamezaliwa na makuzi kama ya wanyama na hata pengine wasiwafikie wanyama katika kuwasiliana. Mtu anahitaji kitu badala ya kushawishi apatiwe anaweka vitisho, jeuri, mikwara, dharau, au mitego kuforce upande wa pili umpatie kitu ambao pengine hata hauna wazo kuwa kinahitajika. Ni ngumu sana kuishi na mtu asiyejua namna ya kuwasiliana na mwenzake.

5. Kuishi kwa mapokeo: hapa ni kuishi kwa kukopi mfumo wa maisha ya kizazi chako ulipotoka badala ya kutazama ni mazingira gani yapo sasa. Mfano, mtu anaclamisha kuwa wanaume ni providers kwa 100% na akikosa sio mwanaume halisi bila kutazama nyakati za sasa na miaka hiyo ni tofauti mambo mengi yamebadilika. Au mwanaume kudhani mwanamke anatakiwa kuwa mwoga kwa mume wake na kuishi kama paka na panya ndani bila kuwa best friends.

6. Kuishi double life: kuna watu wanaishi ila hawapo pale wanapoonekana kuwapo. Mfano mwanamke anakaa na kijana mwenye maisha ya kipato cha chini na huku anadate na mtu mwingine ambaye anamhitaji kwa sababu zingine, wizi wa mapenzi. Ni ngumu sana kuweza kusustain Maisha ya uhalisia kwa tabia hizi.

7. Matumizi mabaya ya muda: unatumiaje muda wako na mwenzi wako ina amua mnakuwa imara kwa kiwango gani. Kama unampenda utatengeza culture yenu itakayo wawezesha kufanya Maisha yenu kuwa simple kuishi pamoja na sio kuwa na mfumo wa Maisha ambao kuishi pamoja inakuwa ni vita au mzigo.

8. Kutofanya Psychological evaluation: ni vema kila baada ya muda kujitathimini kisaikolojia kama unakua au umeganda. Unakutana na mdada au mkaka wa miaka 25 au 26,27,28 au 30 ila mwenendo wake kitabia kwa wakati huo na alipokuwa miaka 22 ni sawa sawa. Hii inamaanisha huyu mtu hajifuatilii wala kujiboresha kiakili hivyo hakui. Mtu asiyekua kiakili ni ngumu kufanikiwa kimahusiano. Tabia zina athiri sana maamuzi ya mtu na mahusiano yake na wengine.

9. Uvivu: ni aspect inayoanzia kwenye fikra. Uvivu maana yake kwa kifupi ni kukosa msukumo wa kuwajibika kulingana na nafasi yako. Mtu mvivu huwa anaamini ana haki ya kufanyiwa yale anayoshindwa jifanyia hata kama ni wajibu wake. Mfano, wadada wengi leo wanalaumu wanaume kutowapa pesa za matumizi yao binafsi na kuamini sio watu sahihi ila ukweli ni kuwa wao wamerithi akili za umasikini tokea makwao na ndio maana wamezaliwa na sumu ya uvivu na kupenda kupewa vitu ambavyo sio stahiki yao. Ni ngumu kudumu na mtu kama wewe ni mvivu.

10. Kushindwa kuelewa purpose ya uwepo wako hapa duniani kwa kurejea maagizo ya MUNGU. Wengi mahusiano wanachukulia kama starehe kwa asilimia zote na kusahau majukumu na wajibu wa kuwapo katika mahusiano kwa misingi ya upendo, kujali, kujitoa, kupanga pamoja, kujenga pamoja, kutunzana, kuleta watoto, kuwalea kwa maadili, uaminifu, kuongoza na kutii. Nje ya hapa hakuna kudumu ni kupoteza muda.

Haya ni machache ila yapo mengi sana yanayochangia mahusiano ya sasa kuwa sehemu temporary ya kuishi huku mtu akingoja kwenda sehemu nyingine.
 
Tumejifunza kitu Asante kwa madini
 
Back
Top Bottom