Kwanini walibadilisha rangi za ndege za ATC?

1094193.jpg


Kwenye ndege hii hii nimependa design na rangi zilizopo, labda tu kama wakiirudisha wajaribu kubadili rangi ya kijani hapo juu imekaa kama ile kijani ya bendera ya Afrika kusini.

wewe ni kaburu nini... huoni bendera ya SA
 
Inatupa faraja na matumaini tunapoona ndege inayopeperusha bendera ya nchi mungu ibariki kampuni hii ikue iwe na uwezo wa kufanya hata safari za nje ya Tanzania kwani nionavyo ni namna nzuri zaidi ya kujitangaza kimataifa zaidi kuwa na nndege zenye kubeba nembo ya taifa zikifanya safari katika mataifa tofauti duniani mungu ibariki Air Tanzania ibariki Tanzania na utalii ndani yake..
 
Rangi hizo mchanganyiko wa za bendera ni mfumo wa rangi wa South African Airways (branding), ambazo ndege za ATCL zilipakwa wakati tukiwa ubia na shirika la ndege la Afrika Kusini (SAA). Angalia kwamba umbo lake linashabihiana na lile la SAA, na hata font na style ya maandishi ya Air Tanzania ni sawa na ya South African Airways, kwa kuwa hii ilkuwa ni branding ya SAA kwa ATCL. SAA walifanya hivyo ili kuihusianisha brand ya ATCL na ile ya SAA. Twiga na rangi ya bluu ni branding ya ATCL original, ya watanzania wenyewe, ambayo ilibadilika baada ya kutoka branding ya Air Tanzania Corporation (ATC), ambayo ilikuwa na twiga na mistari ya rangi ya bendera ya Tanzania katikati. Hii branding ya ATC iliachwa ili kukupa wazo kwamba shirika lilikuwa limebadilika.

Kinachoniudhi ni kwamba branding ya sasa ya ATCL imeiga kwa kiasi kikubwa ile ya Kenya Airways (KQ). Yaani hatuwezi kuja na kitu chetu original?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom