Kwanini Vifaa vya Ujenzi vitoke South Africa?

vassil

Senior Member
Apr 13, 2008
122
15
Baada ya kukaa ughaibuni kwa muda mrefu nikawaza kujenga kibanda changu huko mbweni hivyo nikaomba ushauri kutoka kwa ndugu na jamaa.Vitu vingi nikiuliza naambiwa ni vya kutoka South Africa,mabati vigae, bei ya cement ni kubwa saana nikaambiwa ni kwa sababu Cement inapelekwa S.Africa na Congo.Kampuni zetu kama Mbezi tiles nasikia zimekufa.Naombeni mawazo yenu watu wenye uzoefu wa mambo ya ujenzi ndani ya Dar-es-salaam
 
Mawazo gani mkuu? make hujawa specific kama unataka mawazo kuhusu gharama, au aina ya vifaa vya kutumia? Vigae sio vyote vinatoka S.A, nenda Nabaki Afrika utakuta vigae vya aina nyingine, kuna viwanda vingine hapa nchini vimeshaanza kutengeneza vigae(vile vya bati) ofcoz ubora wake sina uhakika nao, bt all in all too much is going on about building materials so inabidi uwe macho usijepigwa changa la macho!
 
Baada ya kukaa ughaibuni kwa muda mrefu nikawaza kujenga kibanda changu huko mbweni hivyo nikaomba ushauri kutoka kwa ndugu na jamaa.Vitu vingi nikiuliza naambiwa ni vya kutoka South Africa,mabati vigae, bei ya cement ni kubwa saana nikaambiwa ni kwa sababu Cement inapelekwa S.Africa na Congo.Kampuni zetu kama Mbezi tiles nasikia zimekufa.Naombeni mawazo yenu watu wenye uzoefu wa mambo ya ujenzi ndani ya Dar-es-salaam

...habari ndio hiyo ndugu yangu, mabati na 'vigae' vya south afrika (actually ni mabati mfano wa kigae) ndio vimeshika hatamu ya urembo kwa sasa, na bei yake mnnhh... mwaka 2006 kipande kilikuwa shs 9,000 mpaka umalize nyumba ya kawaida i.e vyumba vitatu, makadirio kwa wakati huo ilikuwa 9m/= 'vigae' tu.

...mbezi tiles bado zipo, ila ujue usipompata fundi mzuri, utabomoa nyumba! mfuko wa cement kwa D'salaam sasa nadhani waweza pata kwa shs 14,500/=. Kuna member mwenzetu hapa fair player waweza muuliza hayo mambo kwa kirefu, jaribu kumtumia private mail.
 
Back
Top Bottom