Kwanini upinzani wetu umeshindwa kututetea badala yake wanatetea wakwepa kodi na mafisadi ya ACACIA?

Beira Boy

JF-Expert Member
Aug 7, 2016
17,895
25,945
Aman iwe nanyi wapendwa katika bwana

Husika na kichwa cha habari hapo juu

Lengo la upinzan ni kutetea maslahi ya wananchi wanyonge na kuisimamia selikali, cha kusikitisha upinzani wetu wao wanajali matumbo yao tu wakifukuzwa bungeni huungana kwa pamoja kumushitaki speaker kwa maslahi yao

Kwa sasa wananchi wako kwenye matatizo makubwa ya hapa na pale wao wapo kimya nyumba na makazi ya watu yanabomolewa wao wamekaa tu, uhuru wa kujieleza haupo tena wao wamekaa kazi yao ni kutetea mafisadi

Acacia waliposhikiliwa makinikia yao hawa wapinzani wetu walikuja juu sana hadi nikasema yes huu ndo upinzani sasa lakin kwa sasa nyumba zinabomolewa na hakuna fidia wamekaa kimiya hakuna hata mmoja anayepasa sauti yake

Kwahiyo nyie wapinzani kazi yenu ni kutetea mafisadi, wauza ngada na wakwepa kodi? Mbona huku kitaa hatuwaelewi

Nguvu yenu kama upinzani iko wapi kwanini haionekani?

Kwanini msisimame upande wetu wanyonge badala ya kusimama upande wa mafisadi na wakwepa kodi?

Hao wakwepa kodi wanawalipa kiasi gani ili nas tujichange tuwe tunawalipa kiasi hicho muweze kusimama upande wetu wanyonge?

Wengine mtajadili mwandiko wangu mara hapa hujaweka koma, mara umeandika utumbo gan huu badala ya kujadili hoja

Balikiwen katika bwana

Cc mbitiyaza

LONDON BABY
 
Bahati mbaya umekosa uelewa na huna moyo wa kujifunza.

Mkwepa kodi hufilisiwa, hufungiwa biashara au kupelekwa mahakamani. Humwombi aje kwenye meza ya mazungumzo.

Wapinzani walipaza sauti zao kuhusiana na madini siyo kuwatetea wevi wa dhahabu bali kwanza kuiambia serikali isitumie ujinga wa wananchi kama wewe kujinufaisha kisiasa kwa mambo ambayo ni ya uwongo. Na pili kuliokoa Taifa dhidi ya upotevu wa pesa unaotokana na maamuzi ya hovyo ambayo mwisho wa siku tunaishia kupoteza hata kidogo tulichokuwa nacho.

Tumekwishajifunza maamuzi ya hovyo yalivyoligharimu Taifa, rejea samaki, mikataba ya bararabara, umeme wa IPTL, n.k. Tutaendelea kuwa wapumba.vu mpaka lini? Kila siku tunalipishwa kwa makosa hayo hayo na ambayo tungeweza kuyazuia, hatujifunzi tu?

Lazima watokee watu wenye akili ambao wanaweza kutamka kuwa upumbav.u kama huo, sisi kama Taifa hatuutaki. Sifa hazitafutwi kwa kuliletea Taifa hasara. Wenye akili hawakusikilizwa. Wajinga wakaunga mkono maamuzi ya kijinga. Sasa tunaambiwa kuwa tulipe fidia. Hayo ndiyo mliyokuwa mnayataka?
 
kweli huu ndio unafiki! wapi bunge live!? wapi kudadavua magazeti? wapi mikutano ya kisiasa, accacia wako huru, kama wameonewa ni haki yao kutafuta mawakili ili kwenda kutaka haki mahakamani! rais kasema pale lumumba haoni wa kumteua, wote mabashite!

ova!
 
USIWE HIVYO, UPINZANI HAUKUTETEA ACACIA ILA ILITOA USHAURI WA NAMNA YA KUSHUGHULIKIA JAMBO HILO ILI KUEPUSHA HASARA KWA TAIFA ITAKAYOTOKANA NA UKIUKWAJI WA MASHARTI YA MIKATABA YA MADINI MLIYOINGIA KWA UTASHI WENU.

HV NI KWELI HAMUELEWI AU NDIYO NJAA?

Jpm alijibu haogopi kushtakiwa baada ya Lissu kumshauri na kutoa tahadhari.
 
Kwanini usijiulize kwanza kwanini serikali yako imeshindwa kukutetea badala ya kulaumu upinzani kushindwa kukutetea? Acha unafiki bora uwe mchawi tujue moja!
 
Wala usitegemee kupata jibu hapa. Swali lako ni rahisi sana:

UPINZANI JAMANI, MBONA MMETUSAHAU TUNAOBOMOLEWA NYUMBA ZETU?

Watu wanakimbilia kusemea makinikia, mikataba mibovu, ufisadi wa CCM, n.k.
 
Sasa naona yale maneno yameanza kutimia:
images

Wapinzani wamepiga kelele kuhusu hili na lile na kila wakati wanakuwa wahanga wa serikali kwa vipigo, kesi, kupatilizwa visas, na kufungwa. Wakati wote huo tumekuwa nyuma ye serikali yetu pendwa ya hapa kazi tu na tumedai kuwa wanaolalamika ni wapiga dili kama rais wetu anavyodai. wamepinga na kupiga kelele, wameshutumiwa kama unavyowashutumu sasa na huenda wameishiwa ari na nguvu ya kutusemea maana hatuthamini kujitolea kwao.

Sasa yanaanza kuja mapigo yasiyoangaia vyama vya siasa maana sina hakika kama pembezoni mwa barabara na reli wamejipanga chadema..nina hakika wapo watu wa vyama vyote. Wapinzani wapo kimya sasa mnaanza kulalamika. Tunaipenda kazi ya serikali yetu ya kutuletea maendeleo. Msimcheleweshe Rais wetu. Hapa kazi tu. Wanaolalamika kubomolewa nyumba kupisha miradi ya maendeleo ni wapiga dili.

Yameanza kutimia, na huu ni mwanzo tu. Baada ya hapo, tutakuwa na akili iliyotulia kuweza kutafakari.
 
Aman iwe nanyi wapendwa katika bwana

Wengine mtajadili mwandiko wangu mara hapa hujaweka koma, mara umeandika utumbo gan huu badala ya kujadili hoja

Balikiwen katika bwana

Cc mbitiyaza

LONDON BABY
Hoja yenyewe iko wapi basi tuijadili? Wasalimie Kigoma
 
Wala usitegemee kupata jibu hapa. Swali lako ni rahisi sana:

UPINZANI JAMANI, MBONA MMETUSAHAU TUNAOBOMOLEWA NYUMBA ZETU?

Watu wanakimbilia kusemea makinikia, mikataba mibovu, ufisadi wa CCM, n.k.

Wewe badala ya kumlaumu anayebomoa, unamlaumu ambaye unadhani kazi yake ni kukutetea!!
 
Kwanini usijiulize kwanza kwanini serikali yako imeshindwa kukutetea badala ya kulaumu upinzani kushindwa kukutetea? Acha unafiki bora uwe mchawi tujue moja!
Kwanza kwa nini asiishangae kauli yake?
Iweje wapinzani watutetee dhidi ya serikali yetu?
Ina maana serikali yetu ni kandamizi?
Kama ni serikali pendwa chini ya Rais wetu mpendwa, kwa nini wananchi tuhitaji utetezi?
 
Sasa naona yale maneno yameanza kutimia:
images

Wapinzani wamepiga kelele kuhusu hili na lile na kila wakati wanakuwa wahanga wa serikali kwa vipigo, kesi, kupatilizwa visas, na kufungwa. Wakati wote huo tumekuwa nyuma ye serikali yetu pendwa ya hapa kazi tu na tumedai kuwa wanaolalamika ni wapiga dili kama rais wetu anavyodai. wamepinga na kupiga kelele, wameshutumiwa kama unavyowashutumu sasa na huenda wameishiwa ari na nguvu ya kutusemea maana hatuthamini kujitolea kwao.

Sasa yanaanza kuja mapigo yasiyoangaia vyama vya siasa maana sina hakika kama pembezoni mwa barabara na reli wamejipanga chadema..nina hakika wapo watu wa vyama vyote. Wapinzani wapo kimya sasa mnaanza kulalamika. Tunaipenda kazi ya serikali yetu ya kutuletea maendeleo. Msimcheleweshe Rais wetu. Hapa kazi tu. Wanaolalamika kubomolewa nyumba kupisha miradi ya maendeleo ni wapiga dili.

Yameanza kutimia, na huu ni mwanzo tu. Baada ya hapo, tutakuwa na akili iliyotulia kuweza kutafakari.
Mahaba kwako jemedari...!

Sumu ya panya inaua hadi mbwa, boma halikaliki sasa.
 
Back
Top Bottom