Kwanini unataka mtoto/ watoto?

Sio kweli ndoa umeielewa vibaya, dhumuni sio kupata watoto, watoto ni baraka kutoka kwa Mungu. Dhumuni la ndoa ni kujipatia msaidizi na kuwepo watoto au wasiwepo ni sawa tu. Adam aliumbiwa msaidizi ila Mungu aliwaagiza wazae waongezeke wakaijaze nchi. Kuzaa ni sehemu ya uumbaji ya Mungu mwenyewe kupitia mwanadamu.
Hii imetulia sana!
 
Binafsi naona watoto wana umuhimu sana kwangu,
Na namwomba mungu siku moja anipatie japo wawili,
Maisha yangu naamini hayatakamilika bila kuwa na watoto km wazazi wangu walivyonileta duniani,
Haka km itashindikana kuwa na wangu wa damu yangu basi nitaadapti na kutimiza lengo langu la kuwa na mtoto.
Jamani fanya japo hata sita si umesikia tunahitaji rasirimali watu?
wanaotuhimiza tupungue wenyewe wako wengi.
 
kwa mujibu wa maandiko matakatifu tunaambiwa tuzaliane kwa uzazi wa mpango na kuijaza nchi, hivyo ni haki yangu ya msingi kua na watoto ama mtoto
 
Wapo ambao kwao mtoto ni bahati mbaya ndio maana wanajitenga nao na unakuta mama anamchukia kabisa mwanae wa kumzaa na anamropokea au anasema kwa watu
"niliogopa kutoa mimba watu walinitisha" (ni mamangumdogo anamsema mwanae aliempata akiwa mwanafunzi.
 
Mimi napenda kuwa na watoto hata wanne(hongera waliojaaliwa kupata hata mmoja)
kwangu mtoto ni furaha,
mtoto ni faraja
mtoto ni ujasiri (maana kuna watu wengine wanaogopa)
mtoto ni alama
mtoto ni hamasa(watu wanajituma zaidi hasa wanapokua na watoto)
mtoto ni rafiki
kikubwa kuomba sana Mungu mtoto akue ktk njia impasayo asiyaache mafundisho yangu.
Napenda mtoto,
mtoto wangu ambae nitamtazama nishangae na kumsifu Mungu kua ametoka katika mwili wangu.

Tumezaliwa saba,japo kuna kutofautiana ila naamini wazazi wetu wanafurahi kwa ajili yetu.
 
Ni kweli wapo ambao wamepata watoto kwa bahati mbaya, wengine walijaribu
hata kutoa mimba ikashindikana. Ninaowakusudia hapa ni wale ambao wamedhamiria
kupata hao watoto. Tena wengine wamethubutu hata kwenda kwa waganga.
Wako ambao wanasema wanataka watoto ili wawasaidie hapo baadae.

Nataka kujua kutoka kwenu kwanini unahitaji mtoto/watoto mpaka kufikia kukosa
furaha ndani ya mahusiano na mwenza wako?
Unataka akusaidie?
Ni pambo la nyumba?
Kwanini mtoto?
Natafuta watoto si kwa sababu wanisaidie, wala si wawe mapambo ya nyumba. Natafuta watoto kwa sababu watoto niliowazaa mwenyewe ni extension ya nafsi yangu. Watoto wangu ni 'sehemu' ya mimi inayoishi ndani mwao. Hili linaniletea faraja kubwa sana na furaha isiyo na kifani; kwani ninapowaona wakitembea, wakicheka na kufurahi najiona mwenyewe. Ni kama nimezaliwa upya. Ni mimi huyu, ndani mwao, japo wao ni nafsi tofauti na mimi, ni watu huru na kamili. Lakini wapo kwa sababu mimi (nikishirikiana na Mungu) na mama yao ndiyo sababu ya uwepo wao. Ni furaha iliyoje? Nani atajinyima furaha hiyo ya kuwa na watoto? Ndiyo maana wakikosekana katika ndoa basi wanandoa tunakuwa kama tumekufa vile japo bado tunaishi.
 
Wapo ambao kwao mtoto ni bahati mbaya ndio maana wanajitenga nao na unakuta mama anamchukia kabisa mwanae wa kumzaa na anamropokea au anasema kwa watu
"niliogopa kutoa mimba watu walinitisha" (ni mamangumdogo anamsema mwanae aliempata akiwa mwanafunzi.
 
Kwa ninavyojua Dhumuni kubwa la ndoa ni watoto. Lakini ikitokea bahati mbaya wasipopatikana isiwe sababu ya kuvunjika kwa ndoa.

MBIO! Hapa tutapishana idea kama si mitazamo! Mtazamo wangu ambao nauamini ni kua kupata watoto sio dhumuni kuu la Ndoa.
Dhumuni kuu la Ndoa ni kupata UTULIVU (Full- Stop). Watoto ni Result ya UTULIVU.
 
Back
Top Bottom