Song of Solomon
JF-Expert Member
- Aug 5, 2021
- 2,733
- 5,490
Huyu apewe maua yake , ya lazima kuisoma natafsiri kwa kifupi tu.
Mkutano wa Familia
Mama yetu alifanya kitu cha kustaajibisha na kusichotegemewa. Alitutumia ujumbe wa mkutano wa dharura wa familia nyumbani. Sote wanne tulifika, lakini mama hakutupokea kwa furaha tuliozoweya. Kulikuwa na ubaridi fulani katika sauti yake.
Hata baba alishangaa kutuona wote watoto wake wa kiume pamoja na akamuuliza Mama kulikoni, akajibiwa subiri utajua sababu.
Mama akatushukuru kwa kuacha shughuli zetu na kufika lakini tumemuudhi. Na yeyote anayemuudhi yeye anakuwa amemuudhi Mume wake.
Baba alijaribu kusema lakini mama alivyomtazama akanyamaza na kutabasamu tu. Sijui kwa ndugu zangu wengine lakini mimi sijamkosea yeye na baba kwa njia yoyote. Kaka mkubwa alisema. Nina uhakika Mama.
Akatuuliza siku ya kuzaliwa ya baba yenu ilikuwa lini? Tukaangaliana kwa nyuso za hatia. Ilikuwa ni jana nikajibu.
Mama akasema kama nakumbuka vizuri hakuna hata mmoja wenu aliyepiga simu wala kutuma ujumbe kwenda kwa baba yenu. Kama ingekuwa ni yangu nyote pamoja na wake zenu msingeisahau na mngeirusha mitandaoni.
Na mgenipigia simu na kunitumia na kunijazia hela kwenye akaunti yangu. Nimewaangalia kwa miaka kadhaa lakini siwezi nikaachia hali hii iendelee. Baba alishangazwa sana na sababu ya mama kuitisha mkutano ule.
Kila mwezi mnanitumia hela bila kuwaomba. Lakini hamfanyi hivyo kwa Mume wangu kama vile siyo Baba yenu. Kwa ukweli acheni kunitumia Mimi tu. Namba ya Baba yenu mnayo lakini hamumpigii bali mnaniambia mpe salamu Baba.
Tukajisikia vibaya kwa sababu ya ukweli aliyotuambia. Nikakumbuka kwenye sherehe yake mama niliagiza hadi matarumbeta.
Mnafikiria ni nani alilipa ada zenu wote nyie Hadi mkahitimu vyuo vikuu. Nani alilipa kodi, alileta chakula tulichokula, aliyelipa kodi mpaka tukahamia kwenye nyumba yetu. Yeye ndiye alitafuta hela za kila kitu na Mimi nilimsaidia tu. Mnafikiria Baba yenu hapendi mapenzi na ukaribu na watoto wake. Mnadhani ni mama tu anayestahili. Mama alijifuta machozi.
Kwa hiyo mlipanga tu kusherehekea msiba wa mume wangu, kwa kununua ng'ombe kuwafanya watu wafikirie mlikuwa mnamjali sana? Mshukuru Mungu na nyie mna watoto na mtavuna mnachopanda. Msifikiri mume wangu halii na kusononeka. Au hasikii uchungu. Hamuwezi kujua.
Mama alituangalia kwa makini kabla hajajifuta tena machozi.
Sintokuwa miongoni mwa kundi la wanawake wanao watenganisha watoto na baba zao kwa kuwaambia ungo kuwa baba yao hakuwajali na hakuwafanyia lolote. Wapo Wapo wanaume wachache wasiojali lolote, lakini siongelei hao. Huyu baba yenu ni Simba wangu na katika miaka yake 75 bado anaustua moyo wangu. Sintoruhusu nyie mumdharau baba yenu.
Wakati tunatafakari mama aliondoka ghafla kwenda chumbani kwao na kurudi na funguo za gari la baba na pochi yake na kumshika baba mkono.
Twende alisema mama, na baba hakukataa na kumfuata. Mnaenda wapi? Wote tulisema kwa pamoja. Tunaenda na mume wangu kusherehekea siku yake ya kuzaliwa.
Lakini na mama.... Hakutujibu wala kutupa nafasi ya kusema lolote. Fungeni milango na geti, alimwambia Kaka mkubwa, ninao ufunguo wa akiba.
Waliingia kwenye gari na kuondoka. Watoto tukabaki na mkutano wetu. Tuliafikiana kuwa tumekosea na tukatambua kuwa hatuwezi kurudi makwetu mpaka tufikie muafaka wa suala hili. Tukawaambia Wake zetu kuwa hatutorudi kwa sababu hatujui wazazi watarudi saa ngapi. Tutalala huku.
Mama akiendesha walirudi saa 1:30 usiku. Mama hakushangaa kutukuta, ila baba alishangaa. Sote tuliomba msamaha wazazi wetu, na kuahidi kubadilika. Mama alirudi toka chumbani na Bibilia. Akafungua kitabu cha Waephesi na akasoma sura ya 6:2 inayosema "waheshimu baba na mama yako" ambayo ni amri ya pekee yenye ahadi.
"Bibilia haisemi mtukuze mama na umsahau baba yako. Uzuri wa amri hii inakuja na ahadi. Kwenye aya ya 3, inasema itakuwa vyema kwako na utaishi miaka mingi duniani.
Mama alichukua muda kufafanua aya hii katika Bibilia, na kutufumbua macho kwa ambacho hatukukifahamu. Mwisho alimtaka baba kutuombea. Alifurahi na kutusalia sala kutoka moyoni.
Hatukurudi makwetu na kuongea hadi usiku sana. Sina Budi kusema mama alitupikia chakula kitamu sana.
Mpendwa msomaji, usingojee mpaka sikukuu ya Baba au ya kuzaliwa baba ndiyo umuenzi baba yako. Nyayua simu yako na umpigie. Usimsahau katika maisha yako.
Wake waenzini Waume zenu. Msijiunge na wanawake wanaowachochea watoto wao kuwachukia na kuwatenga baba zao. Usiwageuze watoto wako kuwachukia baba zao.
Mahusiano ya familia ni ya thamani na hayana budi kuenziwa na kutunza siku zote kiendelevu. Usingoje siku maalumu kuonesha mapenzi na fadhila kwa wazazi wako. Fanya hivyo kila siku Mungu wabariki wababa wote popote walipo wakinge na vifo vya ghafla vinavyosababishwa na msongo wa mawazo .