Kwanini Taasisi za kidini zinahodhi maeneo makubwa ya Ardhi Tanzania? Wapewe wananchi

FaizaFoxy

Platinum Member
Apr 13, 2011
92,883
109,213
Siyo siri, Tanzania taasisi za kidini takriban zote, kwenye mikoa na wilaya zote zinahodhi maeneo makubwa ya ardhi ambayo hayatumiki kabisa au utakuta kwenye maeneo yao makubwa wanayohodhi kinejengwa kijumba kimoja au viwili vya kuzuga tu.

Wakati huohuo tunasikia mara kwa mara migogoro ya majeshi yetu na raia kuhusu ardhi.

Kwanini serikali isizirudishe hizo ardhi na kuwapa raia?

. Maeneo ya mashambani wapewe wenye kuhitaji kulima japo eka mbili mbili. Wawekewe miundombinu ya kilimo cha umwagiliaji.

Maeneo ya maporini wapewe wafugaji waanze kufundishwa kupanda majani bora ya mifugo kama alfalfa na mengineyo, nao wawekewe miundombinu ya kilimo cha umwaguliaji. (irrigation). Wakafuge huko badala ya kuwa wahamahamaji, kurandaranda Tanzania nzima wskitafuta majani ya mifugo yao.

Maeneo ys kuishi watu wapewe raia wajenge.

Hii utaendana vizuri na mpango wa mama Samia wa BBT.

Nawakilisha.
 
Wivu mtupu, nyie mlikuwa wapi?

Wenzenu wanatazama mahitaji yao hata baada ya miaka hamsini ijayo, ndio maana wanachukua maeneo makubwa yatakayowatosha kukidhi mahitaji yao.

Badala mkajifunze uwekezaji kwao, akili mbovu inataka wanyan'ganywe ili wote tuwe wachovu tunaofanana, mtu kuwa na fikra za kimaskini zinazoambatana na chuki, ni mbaya sana kwenye jamii, afadhali uishi na mchawi.

•Watanganyika tunazitaka bandari zetu zote mlizompa mwarabu milele.
 
Taasisi za dini zina hela. Tafuta hela

1. Unajua Magufuli amehodhi robo ya ardhi ya Jimbo la Bashungwa?

2. Unafahamu Sumaye alihodhi nusu ya ardhi ya wilaya ya Mvomero? Alinyang'anywa baada ya kuhamia chadema.
3. Unafahamu mama Anne Makindq ana mahekari ya ardhi kule Bagamoyo?
4. Unaelewa kwamba maeneo mengi yanayotwaliwa na serikali kwa fidia kubwa ili kuweka EPZ mkoani Pwani yanamilikiwa na nani?

5. Unajua kuwa rais Samia ana eneo kubwa Sana Bagamoyo?

6. Unaelewa kuwa Bashe ana maekari ya ardhi Morogoro ambayo ameyafanya kuwa ranch ya mifugo yake ?
7. Umelisikia sakata la Mpina hivi karibuni? Amehodhi ardhi ya vijiji 3.
 
Mkiambiwa pangeni mipango ya muda mrefu mnaona ni ujinga.
Mkiambiwa nendeni mpate elimu dunia iliyo bora, mnaona ujinga.

Kwa taarifa yako,taasisi za dini (Hasa Za Kikristo) ndizo zinazoongoza katika kuhudumia Watanzania wengi masikini (hasa kwenye sekta ya afya).
 
Wivu mtupu, nyie mlikuwa wapi?

Wenzenu wanatazama mahitaji yao hata baada ya miaka hamsini ijayo, ndio maana wanachukua maeneo makubwa yatakayowatosha kukidhi mahitaji yao.

Badala mkajifunze uwekezaji kwao, akili mbovu inataka wanyan'ganywe ili wote tuwe wachovu tunaaofanana, mtu kuwa na fikra za kimaskini zinazoambatana na chuki, ni mbaya sana, afadhali uishi na uchawi.
Tupo bize na Madufu.
 
Wivu mtupu, nyie mlikuwa wapi?

Wenzenu wanatazama mahitaji yao hata baada ya miaka hamsini ijayo, ndio maana wanachukua maeneo makubwa yatakayowatosha kukidhi mahitaji yao.

Badala mkajifunze uwekezaji kwao, akili mbovu inataka wanyan'ganywe ili wote tuwe wachovu tunaaofanana, mtu kuwa na fikra za kimaskini zinazoambatana na chuki, ni mbaya sana kwenye jamii, afadhali uishi na mchawi.
Unaongelea "nyie" ndiyo kina nani hao?
 
Siyo siri, Tanzania taasisi za kidini takriban zote, kwenye mikoa na wilaya zote zinahodhi maeneo makubwa ya ardhi ambayo hayatumiki kabisa au utakuta kwenye maeneo yao makubwa wanayohodhi kinejengwa kijumba kimoja au viwili vya kuzuga tu.

Wakati huohuo tunasikia mara kwa mara migogoro ya majeshi yetu na raia kuhusu ardhi.

Kwanini serikali isizirudishe hizo ardhi na kuwapa raia?

. Maeneo ya mashambani wapewe wenye kuhitaji kulima japo eka mbili mbili. Wawekewe miundombinu ya kilimo cha umwagiliaji.

Maeneo ya maporini wapewe wafugaji waanze kufundishwa kupanda majani bora ya mifugo kama alfalfa na mengineyo, nao wawekewe miundombinu ya kilimo cha umwaguliaji. (irrigation). Wakafuge huko badala ya kuwa wahamahamaji, kurandaranda Tanzania nzima wskitafuta majani ya mifugo yao.

Maeneo ys kuishi watu wapewe raia wajenge.

Hii utaendana vizuri na mpango wa mama Samia wa BBT.

Nawakilisha.
Kwani ardhi imeisha mpaka wapewe. Mbona Tanzania ardhi ipo kubwa tu ni bikra kabisa au wivu wako tu. Sasa tuzungumzia bandari imeuzwa kingese sana
 
Kuna memba humu aliwahisema Zanzibar KANISA KATOLIKI Mila pili kuwa na rdhi kubwa wakiongozwa na kesho. Lkn wamelipata kwa kufuata taratibu zote. Hivyo full document. Na hao wakatoliki nafikiri kusoma kwao ndiko kulikowapa hizo ardhi. Wana maneno makubwa tena potential kila Kona ya nchi hii. Lkn kiuhalali wala si kwa wizi.

Sent from my SM-G977B using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom