Kwanini sherehe nyingi za Kitaifa hapa Tanzania hazifanyiki katika mkoa wa Kilimanjaro (Moshi)?

Mandla Jr.

JF-Expert Member
Dec 15, 2013
3,099
630
Wanabodi,

Hapa Tanzania kuna sherehe nyingi sana za Kitaifa kila mwaka. Na sherehe hizi hufanyika katika mikoa mbalimbali ya Tanzania. Mfano siku wa watoto Kitaifa, Kumbukumbu ya Mashujaa wa Taifa, Mei Mosi Kitaifa, Kuwasha au Kuzima Mwenge Kitaifa, Siku ya Wanawake Kitaifa n.k., zipo nyingi.

Huu ni utafiti nilioufanya takribani kwa miaka minne iliyopita. Lakini kwa bahati mbaya sana, sijawahi kusikia au kuona sherehe hizi za Kitaifa zikifanyika Mkoani Kilimanjaro (Moshi).

Labda kuna tatizo huko...
 
Nenda Ofisi ya Mkuu wa Mkoa utapata orodha ya Sherehe za Kitaifa zinazotumika Moshi mosi sherehe ya siku ya Mazingira Kitaifa Moshi 2013 uwanja wa Mashujaa Moshi.
 
Sasa kilimanjaro nani atahudhuria?au mzazi gani atakubali mtoto wake aachishwe masomo akahudhurie misherehe ya CCM?
 
Hicho Kibatali Sijui Mwenye Mwisho Wake Mwaka Huu Baada Ya Hapo Atakaetaka Kukiona Ataenda Makumbusho Patakuwepo Na Kibert Pembeni Kwa Ajili Ya Kuwashia Unakiwasha Na Unakizima,
 
Mwenge ni wa CCM, chama makini hakiwezi kuweka tambara kwenye kopo na kulichoma moto kisha kukimbia nalo kama kichaa na kukesha nalo huku watu wakifanya ngono hatarishi!

Haaa ha ha ha haa Kamanda umegonga penyewe.
 
1.Nani atakuja?

2.Ni mzazi yupi atakayekubali mtoto wake aache kwenda shule audhurie mambo ya kipuuzi kama mwenge?

Viongozi wa Kitaifa na wananchi kutoka mikoa mingine!

KWA TAARIFA: Hizi sherehe huwa ni kama utalii wa ndani na kuongeza kipato kwa wakazi.

Mandla.
 
ziliwahi kufanyika miaka ya nyuma zikakosa waudhuriaji maana sherehe nyingine nizakipuuzi!!
 
Moshi Chadema ndo chama tawala na CCM ni chama cha upinzani! Meya na madiwani wengi ni wa Chadema! Hiyo ndo sababu!
 
Back
Top Bottom