Kwanini NOAH (minbus) zizuiliwe!!?

STIDE

JF-Expert Member
Sep 1, 2011
997
350
Wakuu heshima mbele.

Taarifa zilizopo hadi sasa ni kwamba gari hizi mwisho wa kufanya shughuli za kibiashara ni mwezi wa sita, sababu kuu ni kupunguza ajali za barabarani, lakini je, serikali imekosa njia mbadala kuweza kuzuia jambo hili!?

Je serikali haioni kwamba kuzuia magari haya kutaongeza kwa kiasi kikubwa vijana vijiweni ambao sasa walikuwa wamepata ajira?

Je, serikali haioni kuwa itawasababishia usumbufu wakazi wa vijijini ambako mabasi makubwa hayafiki!?

My take:
jambo hili la ajali barabarani linazuilika kama trafiki wakifanya kazi kwa uadilifu wakaacha rushwa!! Serikali iache kutunyanyasa kwa kutupandishia gharama za maisha halafu wanatuzibia hata pa kujikwamulia!!

Mjadala mezani wakuu nilipokosea rekebisheni!!
 
Nani amekwambia zinasitishwa? nyingi zimesajiliwa kama tours na c psv so naweza kuona ugumu/utata wa habari yako
 
Ni taarifa ya ukweli kabisa kwani waliozisajiri kwa biashara mikoani wameambiwa baada ya leseni kuisha hawataweza kuzisajili tena. Maana yake kila aliyesajiri mda ukiidha na biashara kwishney!
 
.Wanachosema ni kuwa gari zenye tair moja moja nyuma hazitaruhusiwa kusafirisha abiria toka wilaya moja kwenda nyingine.so tuvute subira.
 
Serikali imefanya sahihi maana noah sio basi ni gari ya kifamilia zaidi,imehalalishwa kubeeba abiria saba tu,ila angalia kwa sasa idadi ya abiria inayobeba hadi kwenye buti,na katika mazingira ya kijijini abiria mwenye mzigo hawezi safiri. Kwakuwa hamna mahali pa kuweka mzigo,pia nauli zao hazifuati viwango vilivyopangwa na serikali maana ili apate faida kutokana na idadi ya abiria lazima achaji nauli zaidi.
 
Sio gari rasmi za biashara ya uchukuzi ! Ni mambo ya kienyeji enyeji ndo yametufikisha hapo. Kamavile watu kuchukuwa malori ya zamani na kuyageuza mabasi !
 
.Wanachosema ni kuwa gari zenye tair moja moja nyuma hazitaruhusiwa kusafirisha abiria toka wilaya moja kwenda nyingine.so tuvute subira.

Kama ndivyo basi afadhali wazisitishe tuu, maana naona wana sababu nzuri kabisa. Kutoka wilaya moja hadi nyingine yatumike mabus makubwa kidogo yenye tairi mbilimbli nyuma.
 
kweli noah zime pigwa stop huwezi kuisajili tena kama gari ya biahsra ya abiri,Noah inakimbia sana balaa lake ikila mzinga kupona ni 2% mana body ni laini sana pia ziko overloaded sana.A-town ndio chanzo cha kufutwa kwa magari haya wana kula shazi la kufa mtu.
 
Ifike mahali Watanzania tutumie akili tulizopewa bure. Waliotengeneza haya magari wameweka bayana na matumizi. Sasa gari linaloenewa watu 7, mnataka kulazimisha liwe linapakia zaidi ya hiyo idadi hilo si sawa.
Ni vyema kama unataka kulitumia kibiashara basi lifanye liwe "rental car".
 
Back
Top Bottom