Kwanini nimehamia NCCR-Mageuzi na siyo chama kingine?

Wiston Mogha

Senior Member
Feb 13, 2014
149
96
IMG_20200403_170656_416.jpg

Ndugu wana habari, kwa majina naitwa Wiston Mogha niliyekuwa mwanachama wa ACT- Wazalendo.

Mnamo Machi 18, 2020 nilijivua uanachama wa ACT-Wazalendo na kuujulisha umma wa watanzania kupitia mitandao ya kijamii juu ya maamuzi yangu hayo.

Katika andiko langu la kuujulisha umma nilieleza kuwa nilikuwa kijana mdogo kuliko wote kwenye harakati za uasisi wa chama. Hicho.

Lakini pia nilieleza shukrani zangu kwa chama, viongozi na wanachama wa ACT -wazalendo kwa muda wote tuliokuwa pamoja.

Narejea kusema nimeondoka nikiwa na kumbukumbu nyingi za matumaini na masikitiko. Kubwa zaidi naondoka kutokana na kujipa fursa ya kufikiri msingi wa kesho yangu kama kijana na hatma yangu kwenye siasa za mageuzi.

Ndugu wanahabari, leo nimewaita kuueleza umma kupitia kwenu sababu tatu za kuondoka ACT:

1. Ni kweli niligombea Uenyekiti wa Ngome ya Vijana Taifa na sikushinda ila siondoki kwa sababu ya kushindwa. Isipokuwa sikuridhika na yaliyotokea kwenye uchaguzi yaliyopelekea mimi kushindwa.

Yanaweza yakawa ni mambo ya kawaida kwenye chaguzi za vyama vingine ila kwa kilichokuwa chama changu hayakuwa mambo ya kawaida ambayo tuliyataka yatokee kwenye chaguzi zetu. Hii ni kwa sababu baadhi ya misingi tuliyojiwekea wakati wa uanzishaji chama hicho ni kulinda utu na kuipigania demokrasia.

Ndiyo maana kabla ya uchaguzi nilipiga kelele sana kwenye chama nikitaka demokrasia tunayoihubiri itendeke. Kwenye nafasi niliyogombea, wagombea wote tulikuwa vijana wa chama, lakini kitendo cha viongozi wakuu kushiriki moja kwa moja kwenye uchaguzi wetu kwa kusema fulani ndiye hitaji la chama na fulani anatumika na CCM au fulani ni mtumishi wa usalama wa Taifa, Kitendo kile ni kibaya na kinatengeneza makundi kwa vijana ambao bado kwa sehemu kubwa sana tunahitajiana kesho. Sisi bado vijana wadogo na wote ndoto zetu ni kushiriki kwenye kuongoza historia ya mabadiliko ya nchi yetu.

2. Yalitokea kwenye uchaguzi yamejenga tafsiri ya wazi ya nafasi yangu kwenye chama, Mwonekano wangu kwa viongozi na taswira iliyojengwa na viongozi wakuu kwa wanachama wenzangu.

Sikuwa Na budi bali kujieweka pembeni kwa kuwa mambo haya hajaanza leo na kadri tunavyoendelea yanazidi kuchafua uanachama na utu wangu mpaka kufikia hata rafiki zangu wa karibu kuanza kuwa na mashaka na mimi.

3. Septemba 24, 2014 nilitangaza kwenye vyombo vya habari juu ya dhamira yangu kutaka kugombea ubunge katika Jimbo la Kigoma Mjini. Baada ya kutangaza tu nilifuatwa na viongozi kadhaa na marafiki wakiniomba kukaa pembeni ili kumwachia Zitto. Ilipofika mwaka 2015 baada ya Zitto kujiunga rasmi na ACT-Wazalendo, tukiwa mkoani Shinyanga kwenye ziara tulizungumza na akaniambia dhamira yake ya kugombea ubunge Kigoma mjini na akaniomba mimi nigombee udiwani ili kuendelea kujifunza kwa ukaribu. Kwa heshima na mapenzi kwa kiongozi wangu nilikubali.

Mwaka 2015 niligombea udiwani Kata ya Mwanga Kusini Manispaa ya Kigoma Ujiji lakini nilishindwa kwa idadi ya kura chache kabisa na moja ya sababu ikiwa ni viongozi wangu kumtaka mgombea wa CCM badala yangu. Viongozi walioniomba na kunishawishi wakanifanya kama chambo na njia ya kunidhalilisha kwa kuhakikisha nashindwa udiwani ili ionekane sikuwa mtu sahihi hata kuuwazia ubunge.

Mambo haya yote yamenifanya nione ni bora kuchukua tahadhari kwa kuiangalia kesho yangu na kwa sababu hizo natangaza rasmi kujiondoa ACT-Wazalendo. Kwa kuwa mimi ni mwanasiasa tena kijana ambaye bado nina maisha marefu ya kuitumikia nchi yangu, sitaweza kustaafu siasa kwenye umri mdogo nilionao. Hivyo baada ya maamuzi ya kujivua uanachama wa ACT-Wazalendo, nimeamua kujiunga na chama cha NCCR-Mageuzi.

Kwa nini NCCR- Mageuzi na siyo chama kingine?

1. Nimepitia katiba za vyama mbalimbali vya siasa na kuridhika na muundo wa NCCR-Mageuzi

2. Itikadi yao ya UTU ndiyo niliyokosa kuiona huko nilipotoka na ndicho kitu ambacho moyo wangu unataka kukiishi kwa sasa.

3. Utayari wa viongozi na wanachama wa NCCR kunipokea ili nami nitoe mchango wangu kwenye ujenzi wa chama hiki.

Hivyo NCCR-Mageuzi ni sahihi kwangu kujiunga nao.

BAADA ya tafakuri ya kina na muda wangu wa zaidi ya miaka 10 niliyokuwepo ndani ya mfumo wa vyama vingi, Kujiunga kwangu na NCCR Mageuzi itakuwa ni kupata jukwaa jipya la kuendeleza yale ninayoyamini katika siasa za UTU na uzalendo wa kweli wa kumletea maendeleo mtanzania mnyonge.

Najiunga na NCCR Mageuzi nikiwa na matumaini makubwa nipo kwenye Chama salama chenye kuwatumikia wananchi na siyo kumtumikia mtu na kutekeleza kile anachotaka badala ya maamuzi ya wote.

Naamini uwepo wangu ndani ya NCCR Mageuzi ni maamuzi thabiti yenye kuamsha hisia za kuwakomboa wanyonge, ambapo Chama hiki chini ya Mwenyekiti James Mbatia kimeamua na kina dira ya dhati ya kuwakomboa wananchi wa Tanzania.

Najivunia kujiunga na Chama ambacho tutaendelea kukijenga na chenye mwelekeo wa kuleta maendeleo hasa wakati huu kuelekea katika uchaguzi mkuu wa 2020, ambapo naamini ni wakati wa kwenda kubadilisha siasa za mkoa wetu na Taifa kwa ujumla.

Siasa za Kigoma sasa zinahitaji uwepo wa Chama mbadala, Chama cha kuwaunganisha na kuwapigania wananchi wetu na kujali shida zao ili kushiriki kwa pamoja kuzitatua.

Kigoma yetu italindwa na sisi hasa vijana ambao tunapaswa kuwa mstari wa mbele katika kusimamia maendeleo yetu na kufika mbali zaidi kutoka hapa tulipo.

Nimeshawishika kujiunga na NCCR Mageuzi nikiwa naamini nipo kwenye Chama kilicholeta mageuzi ya kweli ya siasa za ustarabu ambazo kila mtanzania anazipenda na mwelekeo thabiti wa siasa za kimaendeleo kwa wanakigoma, watanzania na si siasa za kimadaraka kama ambavyo vyama vingine vinaeleza.

Shukrani kwa kunisikiliza na
Ahsanteni sana!
 
Mkuu, kumbe umeshahama tayari!
aiseee!

Mimi ninachosisitiza; siasa za vyeo, madaraka na salio haziwezi kusaidia kitu chochote cha maana kutokea. Tutaishia kulaumiana bure tu. Sikulaumu wewe binafsi kwa kuwa hiyo ACT yenyewe naifahamu vizuri na yatokanayo lakini ni lazima tutafakari ni kwa vipi tunaweza kubadili political behaviour.

Misingi 10 iliyoanzisha ACT ilianza kuvunjwa rasimi pale Zitto na kundi lake lilivyojiunga kwenye chama hicho, hakuna alietaka tena kusikia kinachoitwa misingi Zaidi ya utamaduni ule ule wa kukimbizana na matukio, kutafuta umaarufu binafsi na kutokuwa na muelekeo maalum.Binafsi naamini tatizo la msingi liko ndani ya vichwa vya watu mmoja mmoja lakini karibu kwa kila mmoja.

Watu ndio hawa hawa na tabia zao ndio hizi hizi, kwa hiyo jambo kubwa ni 'how shall we change the behavior of political actors in Tanzania?' nje ya hapo kuhama hama sawa ila watu ni wale wale tu na unaowakimbia wanaweza kukukimbilia mkawa pamoja tena.


Halafu unazungumzia uzuri wa katiba ya NCCR, sipingi kwamba katiba ya NCCR sio nzuri ila ukweli ni kuwa hakuna chama chenye documents nzuri zilizoandikwa kama ACT na CCM. Yaani documents nyingi za ACT (Katiba, Misingi, Falsafa, n.k) ni vesion iliyoboreshwa ya CCM (ambapo ndicho chama ambacho kimekuwa na documents nzuri toka miongo na miongo). Kwa bahati mbaya kwenye siasa za Tanzania, yaliyoandikwa mara nyingi hayafuatwi na yasemwayo pia sio yanayofanywa. Dhana ya UTU unayoizungumzia kwa mfano, msingi wake umeanzia CCM. Hiyo iko kwenye misingi ya TANU.
 
Anzisha Chama chako binafsi, kama huwezi go & do farming, sbb CCM hatupokei tena wanachama wanaotaka kuja na kutafuta uongozi, tushafunga dirisha, ikiwa hutaanzisha Chama chako binafsi, unapoteza muda wako na utazeeka na usije ona ktk maisha yako hiyo demokrasia.

Demokrasia bado mdogo ww, inaelekea hujajua maana yake kiundani, unajua on papers tu.
 
Hongera inapobidi yafaa kuufuata moyo wako,lakini naomba nikuulize:
1.je ulishawahi keti chini na viongozi wako wakuu kujadili na kumaliza kero zako?
2.ukikosa cheo hapo je tutegemee Safari zaidi?
 
Ukianza 'umalaya' katika umri mdogo hivyo hadi uje ufike umri wa kina Lipumba utakuwaje ndugu?

Unadhani huko NCCR au CCM au Chadema sijui ndio hakuna changamoto? Vyama vya siasa ni kama ndoa tu, hakuna kusiko na changamoto. Komaeni hapo mlipo vijana!! Sasa wewe unasema ni mmoja wa waasisi wa chama alafu kinakiuka miiko yake unakimbia, unakimbia nini badala ya kukinyoosha, unataka nani akinyooshe chama ulichoasisi? Sema mnavutwa na pesa na usaliti na tamaa ya vyeo tu!

We malalamiko yako au points zako zote ni kushndwa uongozi wa vijana mara kushindwa udiwani mara kumpisha Zitto kugombea ubunge yaani we unahisi huwezi kuwa katika chama cha siasa bila kuwa na cheo sio? Subiri sasa huko unakokwenda utaona kama utapata cheo
 
Kwanini hayo yote uliyoyaamini usiyaseme kwenye chama chako? Na kwanini usubiri mpaka umeshindwa ndio ujitoe? Je ungeshinda huo uenyekiti ungejitoa pia?

Siasa zenu vijana za kutaka nafasi ndio zinawafanya msiwe mnaaminiwa kabisa nakuharibu taswila nzima ya wanasiasa vijana kutoaminika!!!!!!!

NCCR imekuwepo kabla ya chama chenu iweje leo sera zao zikupendeze kuliko sera mlizotunga wenyewe kwenye chama chenu tena ukiwa kama muasisi wa hicho chama?

Mimi nadhani siasa ya kweli na kusimamia misingi na misimamo unayoiamini kwa mujibu wa katiba na itikadi ya chama cha siasa. Unatakiwa uiishi kwa vitendo, tatizo vijana wengi hamna uvumilivu mnataka kufanya siasa muonekane na kujinufaisha baada ya umaarufu ila hamna itikadi wala sera mahususi mnazozisimamia na kuziamini katika kukomboa wananchi ndio maana mmekuwa mkiishi kwa kuamini watu kwenye chama kuliko kufahamu itikadi husika na utambue hivi vyama vitakuwepo tu ila watu mtaendelea kuhama hama kwakukosa misimamo nakutokujua mnachokiamini.
 
Zitto ebu msikilize kijana hapa ni kweli ulimkataza asigombee ubunge😁😁😁😁😁 nacheka kama mazuri vile ebu tusaidie tujue
 
Yaani sisi tunahangaika kufuata taratibu za wizara ya afya kuhusu corona, halafu mjinga mmoja anatuletea UTOPOLO eti anahama chama.
 
Kwahiyo ukifika huko NCCR ukakuta kuna mapungufu nako utahama? Maana ulipojiunga na ACT hadithi zilikuwa hizi hizi, labda kama wakati huo ulikuwa hujui kusoma, kisha ukajiunga kwa kupenda rangi ya chama?

Wahi haraka hilo fungu alilopewa Mbatia la kuwanunua wapinzani, ukichelewa watachukua kina Komu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom