Kwanini Mkuu wa Majeshi hapewi heshima?

Mkuu wa majeshi ana ulinzi wake maalumu toka kwa wanajeshi wa kawaida na makomandoo, kule anakokwenda pia tayari kambi za huko huwa zimetaarifiwa juu ya ziara au msafara wa mkuu wa majeshi hivyo kujipanga kutoa ulinzi.

Kumbuka ndani ya jeshi kuna kitengo maalumu cha ujasusi, kwa hivyo ni vigumu sana kumjua nani jasusi na nani siyo hata TISS ina watu wake maalumu huku jeshini.

Endapo kuna mapinduzi ya kijeshi Mkuu wa majeshi huwa ahusiki ingawa taarifa za mapinduzi huwa anazo.

Wanajeshi wenye vyeo vya chini mfano Captain, kanali ndo huwa wanapindua nchi kwa Baraka za Wakuu wa kijeshi, hao wakuu wa kijeshi kazi yao ni kuwapa taarifa wakuu wa vikosi vya zones na mikoani
Duh.. wee ndio brigedia, tunakuvua vyeo vyote... Bora uwe kuruta chan ocha
 
Au niuelewa wangu mdogo au upo tofauti na ukweli husika?

Kuna huu utaratibu wa viongozi wa kiserikali hasa hapa dar kutembea kwa masafara wa magari kadhaa ukiongozwa na pikipiki.
baadhi ni kama waziri mkuu .spika wa bunge MKUU wa mkoa na mkuu wa polisi Mara NYINGI wanapo kuwa wanapita huwa wanasafishiwa njia kabisa.

Lakini why kwa MKUU wamajeshi huwa tofauti??. Inamaaana kweli kiutendaji hawa wapo juu yake??.

Hivi nji ikipinduliwa nani anashika madaraka ya kuiongoza kama sio MKUU wa majeshi..ss kwanini hapewi heshima ??? au ndio utaratibu??.
wiki iliyopita tulinasa nae kwenye foleni bondeni alikuwa akielekea njia ya TEGETA alikuwa na msafara wa gari 1 tu ya MP ambayo ilikuwa mbele ilibidi washuke nakuanza kupangua gari ili MKUU aweze kupita.
Sababu nyingine inaweza pia kuwa anapoondoka kwenda mahali fulani, huwa haitakiwi watu wengine wajue kuwa anaelekea wapi. Zaidi ni kuwa anaweza kuwa yuko kwenye msafara barabarani halafu vijana wake wakawa wapo kikazi kwenye foleni hizo hizo za magari ambazo wewe unaziona hazina kitu, kumbe kuna information nyeti ya ki-usalama wao wanaikusanya, wapo kazini mda wote! I like these guys anyway!
 
Makomandoo wepi hao, wale wanaopasua matofali mchanga uwanja wa taifa?

Mbona wameshindwa kusaidia Kibiti?

Tunavi overestimate na kuvi over admire bure hivi vyombo vyetu vya usalama, wakasaidie Kibiti!
Vp umetembelea kibiti hivi karibuni?
 
Hahaha daah haya bana inaonekana hata jkt hujapita, ni hivi kuna utofauti mkubwa kati ya hawa Amiri jeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi na Usalama sio cheo nu Madaraka na anakua nayo Rais peke yake na sio kazima awe Mwanajeshi, vilevile Mkuu wa Majeshi yaani (CDF) ni madaraka yenye cheo cha Jenerali yaani Ngao ya bibi na bwana nyota nne na mkasi (four star General) ukibahatika kumuona CDF muangalie mabegani huyu ni Mwanajeshi100% onyo: ukimuangalia sana unaweza kuchapwa
***** ,,,,,,,,umeiva wazi???
 
Mkuu wa majeshi mzee Mabeyo naishi nae mtaa mmoja huku Tabata segerea tangu akiwa mnadhimu mkuu wa jeshi na hata muda mfupi uliopita nilikuwa na mke wake kwenye jumuiya(Mama Mabeyo)....

Akiwa anakuja huku kitaa kutokea town (kupitia njia ya tabata segerea kwenda kinyerezi) ankuwa na escort ya gari moja mbele (gari la MP) na lingine nyuma wakiongozwa na pikipiki kwa mbele (gari lake linakuwa na nyota kadhaa)....anapita bila kukaa kwenye foleni bila kusimama hata sehemu moja mpaka anafika kwake na juzi tu wanajeshi wamemaliza kumchongea barabara ya kwenda nyumbani kwake huku segerea

Labda ulimuona afisa mwingine wa JESHI na si mkuu wa MAJESHI (Mzee MABEYO) mkuu

Nawasilisha wakuu....weekend nkema

Sent using Jamii Forums mobile app
Zile pikipiki za MP au Traffic police???
 
Escort ambayo anatumia mkuu wa majeshi ni kubwa kuliko ya baadhi uliowataja. Mana wale escort yao ni polisi na mkuu wa majeshi escort ni ya makomandoo nadhani unajua tofauti aliyonayo polisi na mwanajeshi
Polisi mbele ya Makomandoo wa JWTZ anaitwa ni RAIA MKAKAMAVU!
 
Back
Top Bottom