Kwanini Mkurugenzi wa jiji la Mwanza unachelewa kulipa likizo za Watumishi bila sababu za msingi?

rsinangila

New Member
Nov 28, 2023
3
1
Ndugu zangu,

Kumekuwa na ucheleweshaji wa malipo ya pesa za nauli ya likizo za watumishi wa umma kwa jiji la Mwanza. Kwani malipo huchukua hata miaka baada ya mtumishi kuomba pesa hio ya likizo.

Kwa mfano katika jiji hili la Mwanza watumishi hususan walimu waliomba likizo kwa mwaka jana mwezi wa 12 na mwezi wa june mwaka huu bado hawajalipwa stahiki zao sijui tatizo ni lipi?

Mkurugenzi wa jiji la mwanza ambaye ndio anayehusika na kulipa malipo haya amekaa kimyaaa hatoi maelezo ya kutosha kwa watumishi. Watumishi wa umma wamebaki kunung'unika hawajui nn la kufanya .

Mkurugenzi wa jiji la Mwanza ndgu yetu tunaomba ufanyie kazi suala hili la malipo ya watumishi wa umma kulipwa stahiki zao za nauli kwa haraka kwani kuna baadhi ya mikoa na wilaya zingine wameshalipwa hizi pesa sasa kwa jiji la mwanza tatizo linakuwa wapi? Wao wilaya zingine waweze kulipa kwa nini wewe wa Mwanza huwezi kulipa? Tatizo hasa ni nini? Lipeni stahiki za wafanyakazi wa umma ili wajikwamuie kwenye matatizo yao.
 
Nimejulishwa mh. Rais SAMIA SULUHU atakuwa na ziara mkoa wa Mwanza kuanzia kesho . Nakuomba Mungu nikipata chance ya kuwepo na nafasi ya kumuuliza hili huyu kiongozi nikamuuliza.
Maana kwa nini mpaka leo hii malipo haya ya likizo za watumishi bado kulipwa?? Toka june 2023 mpka leo Januari 2024. Ni zaidi ya miezi sita(6).
 
Back
Top Bottom