Kwanini Misri inayafaidi zaidi maji ya Ziwa Victoria kuliko sisi wenye nayo?

crankshaft

JF-Expert Member
Jun 12, 2019
1,410
3,376
Tangu nikiwa shule ya msingi nimekuwa nikisikia habari za mto nile. Mto nile ndio mkubwa zaidi barani Africa na chanzo cha maji yake ni ziwa victoria. Misri wanautumia mto huo kwa kilimo cha umwagiliaji chenye tija sana kwa nchi yao.

Tija ya ziwa hili kwa nchi yetu sijawahi kusikia zaidi ya uvuvi na maneno kwamba Mungu katubariki rasilimali hii na ukifuatilia zaidi hata mikoa inayozunguka ziwa hilo huwa inakubwa na uhaba wa maji.

Kwanini hakuna sifa ya kutia fora kwa nchi yetu juu ya ziwa hili zaidi ya kujisifu tu tunalo?

Kwanini nasi tusitumie kwenye kilimo cha umwagiliaji chenye tija sana kama hao wenzetu wa misri? Shida nini huku kwetu?
 
Mbona kikwete alianzisha mradi wa kuyavuta Maji ya ziwa Victoria kufika Dodoma ila mpaka Sasa yamefika Nzega kuelekea shelui and so on. Huo mradi ulipingwa sana na Misri Hadi kutishia kutuma ndege vita kama tutaendelea mbele na mradi huo.

Unless useme tumechelewa sana ila matumizi yameshaanza na mradi ukikamilika maeneo ya Kanda ya kati yatasahau ukame.
 
Mto Nile siyo mto mkubwa kabisa Africa, hata kwenye kumi bora haupo. Ma maji yake mengi, zaidi ya asilimia 60 yanatoka Ethiopia na siyo ziwa Victoria. Nakubali kuwa tuna ufala wa kushindwa kutumia ardhi na maji tuliyopewa kufanya kilimo cha umwagiliaji.

Wanakopa pesa na kwenda kujenga daraja la kuvuka baharini ili wapate sifa 'wamependeza' badala ya kwenda kujenga miradi ya umwagiliaji. Tabia za watu limbukeni.
 
Mtoa mada, hukatanzwi kwenda kuanzisha Irrigation schemes. Si ajabu hata ziwa ilo ukawa hujaliona live achilia mbali mto.
 
Mto Nile siyo mto mkubwa kabisa Africa, hata kwenye kumi bora haupo. Ma maji yake mengi, zaidi ya asilimia 60 yanatoka Ethiopia na siyo ziwa Victoria...
Aisee, Nile sio mto mkubwa kabisa Africa wala haupo kumi-bora? Si unge-google walau kwa dakika moja kabla hujaandika?

Nikujuze tu ili uweke records zako sawa; Nile ndio mto mrefu zaidi Afrika (1st), ni wa saba (7th) kwa discharge (wingi wa maji), na ni wa tisa (9th) kwa eneo (catchment/basin area).
 
Mto Nile siyo mto mkubwa kabisa Africa, hata kwenye kumi bora haupo. Ma maji yake mengi, zaidi ya asilimia 60 yanatoka Ethiopia na siyo ziwa Victoria...
Nili like comment hii nkafuta, nikitaka ku like tena nikasita!

Kusita sita huku kumetokana na ubongo wangu kubishi kuhusu ukweli wa jiografia ya mto Nile na sifa zake!

Kuna mto mwingine Barani Afrika kuupiku kwa ukubwa, ama kuna mto mwingine wowote duniani ulio mrefu zaidi ya mto Nile?

Nimeacha shule miaka 50 iliyopita, yaweza kuwa jiografia ya dunia imesinyaa ama kupanuka!

Embu naomba nitengulie hiki kitendawili, ni mto gani ulio mkubwa na mrefu zaidi kuliko yote barani Afrika kwa sasa?
 
Nili like comment hii nkafuta, nikitaka ku like tena nikasita!

Kusita sita huku kumetokana na ubongo wangu kubishi kuhusu ukweli wa jiografia ya mto Nile na sifa zake...
Mto mrefu kuliko yote duniani ni mto Nile. Ila mto mkubwa(Ukubwa ukipimwa kwa discharge rate) haupo hata kumi bora Africa.

Afrika mto mkubwa ni Congo, na mito inayomwaga Congo kama Kasai, Ubangi, Sankuru etc, kuna Zambezi, Niger na Ogowe upo Gabon. Hapo ndiyo unakuja Nile na mtaw yake.
 
Mbona kikwete alianzisha mradi wa kuyavuta Maji ya ziwa Victoria kufika Dodoma ila mpaka Sasa yamefika Nzega kuelekea shelui and so on..
Umesema wamisri walipinga sana, tafsiri yake ni kwamba hatuna mamlaka na maji hayo hata kama yapo kwetu.

na kama wametulia maana yake pia hatuyatumii ipasavyo bado wanafaidika wao.
 
Back
Top Bottom