Kwanini mawaziri wasimame kama mawaziri kampeni za CCM?

Mar 5, 2012
92
23
Nimekuwa nikitafakari mpaka nimefikia hatuaya kuliandika hili. Mara nyingi, hususani kwenye chaguzi ndogo, unakuta wazirikwa kuwa ni mtu wa chama tawala, CCM, anakwenda kwenye kampeni na kutoa ahadikwamba wananchi wakichagua CCM atafanya mambo kadhaa. Je hii ni halali?.

Nakumbuka Dr. Magufuli alitamka hivyo Igunga, na kibaya zaidi, jana tarehe 22Machi,2012 Waziri Nagu amenukuliwa akisema ‘Mkichagua CCM nitaharakazi ujenziwa kituo maalum za biashara cha kimataifa, na akasema mkichagua upinzaniserikali itacheleweshwa. Tunaomba TUME ya uchaguzi iingilie kati muingiliano waserikali kukipigia kampeni chama tawala kupitia fedha za walipakodi. Sinauhakika, ichunguzwe pia kama wanafika huko kwa fedha za chama na si serikali.

Kwa vyombo vya habari, pengine pia ni borakumtamka mtu kama mwana CCM na sio waziri, kwani kusema waziri kunaweza piakumaanisha ni agizo la serikali kuwa wananchi wachague mtu fulani. CHADEMA piani vema sasa jambo hili likafanyiwa kazi kwa ufasaha.
 
Ni wazo zuri sana!
Swali ni kwamba nani anafanya kazi za Wassira pale ofisini kwake muda huu akiwa Arumeru?
 
Inawezekana Serikali ina ushahidi kwamba vyama vya siasa vinakwamisha juhudi za Serikali katika kuwaletea wananchi maendeleo kutokana na siasa za upotoshaji sinazofanywa na vyama vya upinzania majukwaani na hivyo kuchelewesha maendeleo ya haraka kufikiwa.
 
Ni wazo zuri sana!
Swali ni kwamba nani anafanya kazi za Wassira pale ofisini kwake muda huu akiwa Arumeru?
Ni swali zuri, ila nafikiri kazi ya waziri siyo kukaa ofisini tu, vilevile tujue kwamba Wizara zina wataalamu wake kama makatibu wakuu na wengine wengi sivyo tusifikiri kazi haziendi na ndiyo maana mwisho wa siku tunashuhudia Serikali inawasilisha bajeti zake kikamilifu bungeni kupitia mawaziri hawo.
 
Wana haki yakutetea chama chao, acha woga . Na ukifanya tathmini utaona majimbo ya upinzani yako hohe hahe kabisa, hakuna kinacho endelea. Hilo ni funzo kwa wananchi kuchagua chama chenye meno ili kitekeleze

Ni aibu kwa viongozi wetu mpaka sasa hawajui kutofautisha mambo ya serikali na vyama ktk kampeni
No wonder ata kwa kampeni anaenda na gai la serikali bila kujari kuwa huo sio utaratibu ndo maana Tunduma Vuai walitaka mpopoa na mawe
Lubuva ingilia kati apa
 
Kama kweli kazi zinakwenda vizuri bila ya MAWAZIRI KUWEPO WIZARANI je, kuna haja ya watu hawa kuwepo na kuendelea kula kodi za wa-TZ wakati hakuna wanachikifanya? Je hawa si watumishi wa SERIKALI ambao inatamkwa bayana kuwa HAWARUHUSIWI kujihusisha na SIASA? tafadhali naomba maelezo ya ziada.
 
Ni swali zuri, ila nafikiri kazi ya waziri siyo kukaa ofisini tu, vilevile tujue kwamba Wizara zina wataalamu wake kama makatibu wakuu na wengine wengi sivyo tusifikiri kazi haziendi na ndiyo maana mwisho wa siku tunashuhudia Serikali inawasilisha bajeti zake kikamilifu bungeni kupitia mawaziri hawo.

Jibu na hili: Wasira inakuwaje anaacha ofisi ya umma kwa muda wa mwezi mzima akifanya shughuli za chama na huku anaendelea kupokee mshahara wa umma? sheria za kazi zinaruhusu mtu kutofika ofsini mwezi mzima na bado ukaendelea kulipwa mshahara?
 
Hii nayo ni aina furani ya rushwa ambayo CCM wanatumia hasa kuwatapeli wananchi wakati wa chaguzi ndogo! Ikumbukwe kwamba ahadi alizotoa Magufuli kule Igunga hazijatekelezwa na kwa maana hiyo walikuwa wanafanya ulaghai kwa kutumia nyadhifa zao! Hili ni tatizo la kikatiba!
 
Ni angalizo zuri sana kwa misingi ya demokrasia, uwajibikaji na matumizi ya kodi zetu kwa ujumla. Umekosea tu hapo uliposema tuiombe TUME kuingilia hili, kwani hujui kuwa TUME ni moja ya JUMUIYA mihimu sana ya CCM. Cha kufanya ni sisi wananchi wote tulikemee hili, na kuhakikisha KATIBA ijayo inatenganisha hili na kuruhusu uwepo wa TUME HURU.
 
Haya ni mswali mazuri ya kujiuliza hata kwa tume ya taifa ya uchaguzi, kwa taratibu iliyojiwekea yenyewe ktk chaguzi zote ni makosa kwa kiongozi yeyote wa serikali kutoa ahadi kwa kutmia cheo chake kuwa atatekeleza mradi fulani mkichagua mgombea wa chama fulani wakati anajua mradi tajwa ni sehemu ya mipango ya serikali iliyopitishwa na Bunge lenye wabunge wa vyama vyote.

Nafikiri ni vyema vyama vyote vya upinzani kuchipanga na kuishtaki serikali kwa kutumia madaraka waliyopewa na wananchi kupotosha umma kupitia kwa mawaziri wake. Ilitokea Igunga kwa magufuli kudanganya wananchi kuwa atajenga daraja ndani ya muda mfupi lakini mpaka Leo hakuna kinachoendelea.

Nilikuwa Arumeru nakushuhudia magari ya serikali yamebadilishwa namba yakitumiwa na viongozi wa serikali wakipiga kampeni za magamba huku kwenye vioo vya milango ya magari yakionyesha namba zenyewe.
 
Ni swali zuri, ila nafikiri kazi ya waziri siyo kukaa ofisini tu, vilevile tujue kwamba Wizara zina wataalamu wake kama makatibu wakuu na wengine wengi sivyo tusifikiri kazi haziendi na ndiyo maana mwisho wa siku tunashuhudia Serikali inawasilisha bajeti zake kikamilifu bungeni kupitia mawaziri hawo.

Wana haki yakutetea chama chao, acha woga . Na ukifanya tathmini utaona majimbo ya upinzani yako hohe hahe kabisa, hakuna kinacho endelea. Hilo ni funzo kwa wananchi kuchagua chama chenye meno ili kitekeleze

Inawezekana Serikali ina ushahidi kwamba vyama vya siasa vinakwamisha juhudi za Serikali katika kuwaletea wananchi maendeleo kutokana na siasa za upotoshaji sinazofanywa na vyama vya upinzania majukwaani na hivyo kuchelewesha maendeleo ya haraka kufikiwa.

Akili za matahahira utazijua tu............. ndiyo maana miaka 50 baada ya uhuru bado tuna bajeti tegemezi pamoja na kuwa na siasa za ujamaa na kujitegemea. Eti wapinzani wanakwamisha maendeleo?? Sasa kama waziri mwenyewe anatamka kuwa watachelewesha maendeleo kama Wameru watachagua upinzani............. sijui sasa wewe unataka ushahidi upi kuwa si upinzani wanaoathiri maendeleo ya nchi. Kwa hiyo statement, ni thahili kuwa serikali yenyewe ndiyo kikwazo cha maendeleo ya nchi hii........... na hii inaonyesha ni jinsi gani maendeleo yamekuwa ni kikwazo na chachu ya maendeleo ya sehemu mbalimbali.
 
Ni swali zuri, ila nafikiri kazi ya waziri siyo kukaa ofisini tu, vilevile tujue kwamba Wizara zina wataalamu wake kama makatibu wakuu na wengine wengi sivyo tusifikiri kazi haziendi na ndiyo maana mwisho wa siku tunashuhudia Serikali inawasilisha bajeti zake kikamilifu bungeni kupitia mawaziri hawo.

kwa hiyo kazi za waziri ni pamoja na kupiga kampeni?
 
Ukweli ni kuwa, Tatizo kubwa tulilonalo ni Tume ya Uchaguzi kuwa upande mmoja. Wote wenye mapenzi mema na nchi wanajua hili. Ila hata katika mijadala hii, ukweli ni kuwa tunachangia maanda kutafuta uwanja sawa wa kisiasa lakini wengine mnatetea mfumo mbovu kwa kuwa mnajua katika uwanja sawa wa kisiasa hamna cha kuleza wananchi. Hata hivyo, someni alama za nyakati, tafuteni ukweli, tendeni haki.
 
Hili ni tatizo tena kubwa sana, mimi kwa masikio yangu nilisikia na nikashangazwa sana na kauli ya Wasira; alisema hivi "mimi hapa ninayezungumza ni waziri ninao uwezo wa kuhamisha pesa hata kutoka sehemu nyingine kuja huku" sasa kwa kauli hii unataka ushahidi gani kujua kwamba huyu jamaa anawapa rushwa wananchi ili wamchague mgombea wa ccm?. acha waendelee ila kunasiku isiyojulikana haya yote yatakwisha.
 
GeniousBrain ni kichefuchefu tu si kama username. Hakuna mtu mwenye jina hilo akaongea ***** kama hivyo. Hata kama ni njaa msitembee nazo kwenye mfuko wa rambo. watu wanaochumia tumbo ni wabaya na wanaweza hata kutukana wazazi wao ili wapate sahani ya pilao Halafu kwani ni lazima uchangie kama huna kitu. Aende kwenye majimbo ya upinzani akajionee mambo. halafu ameaga home eti anaenda kazini. Rudi kijijini kwenu ukaliwe na funza.
 
Inawezekana Serikali ina ushahidi kwamba vyama vya siasa vinakwamisha juhudi za Serikali katika kuwaletea wananchi maendeleo kutokana na siasa za upotoshaji sinazofanywa na vyama vya upinzania majukwaani na hivyo kuchelewesha maendeleo ya haraka kufikiwa.

Naona kama umeamua kuipeleka akili yako likizo. Hebua tuambie daraja la Mbutu kule igunga limejengwa? Miaka yote ya utawala wa ccm na ufisadi wake wameshindwa kuwasaidia watz, nani aliwazuia?

Unahitaji akili mfu kuitetea serikali ya ccm.
 
Back
Top Bottom