Kwanini madirisha ya choo hujengwa madogo?

kwanini madirisha ya chooni yajengwe madogo wadau?

Sababu kubwa ni mzunguko wa hewa ndani ya nyumba, kawaida upepo lazima uingilie penye upenyo mkubwa utokee padogo

Kwa msingi huo madirisha ya choo yakiwa makubwa yatarudisha harufu ndani ila kwa vile sebuleni na vyumba yanakua makubwa automatically harufu ya chooni itatoka nje kupitia madirisha yake ambayo ni madogo,

Nina imani kwa kiasi flani nimekujibu
 
Sababu kubwa ni mzunguko wa hewa ndani ya nyumba,kawaida upepo lazima uingilie penye upenyo mkubwa utokee padogo

Kwa msingi huo madirisha ya choo yakiwa makubwa yatarudisha harufu ndani ila kwa vile sebuleni na vyumba yanakua makubwa automatically harufu ya chooni itatoka nje kupitia madirisha yake ambayo nimadogo,

Nina imani kwakiasi flani nimekujibu
Nimeridhika kwa jibu lako mkuu, kama kuna maoni tofauti anakaribishwa.
 
Nyumba yangu madirisha ya choo ni 90cm*90cm

Its a matter of privacy by the way


Privacy..thats the most important.
Architectural proportion..huwezi kuwa na kachumba kadogo kana openings kuubwa.
Kingine ni Cultural aspect..nafikiri unaongelea kwetu tropical and hot humid climates..
Kulingana na tamaduni zetu,mchakato mzima wa maliwato umejaa staha na faragha mno,na baadhi ya tamaduni za kibantu.
kwenda haja jambo ambalo halisemwi kiivo..
Afu pia ukumbuke ni jamii chache za kiafrika tangukale zilikuwa zina Sedentary( less moving lifestyle)
So haya mambo tumetoohoa au kujifunzia mijini au with some other cultural diffusions..
Kuna jamii mpaka leo wanapiga mizigo vichakani..au kama unataka uhakika tafuta report ya Water Aid.
 
Nimeridhika kwa jibu lako mkuu, kama kuna maoni tofauti anakaribishwa.

Hiyo c sababu coz choo hakitakiwi na harufu mbaya hata kidogo kwa sababu kunakuwa na seal ya maji katika wc na floor trap hiyo yote ni kuzuia harufu kurudi ndani. Soo choo kuwa na dirisha kubwa inaweza saidia kuingiza hewa nzuri ya nje na si hewa chafu
 
Miongoni mwa sababu zinazopelekea choo kuwa na madirisha madogo hizi hapa
1. Inapunguza gharama za ujenzi (mind you 1m2 ya ukuta ni 40,000 hadi rangi wakati almn na grill inafika 180,000 kwa 1sm)
2. Dirisha huwa kubwa kuruhusu hewa nyingi kuingia na kutoka sasa chooni inategemea ataingia mtu mmoja au wawili kwa wakati mmoja so hakuna sababu ya kuwa na durisha kubwa wakati mahitaji ya hewa ni madogo ndio maana jiko linakuwaga dogo lakini dirisha kubwa sababu jiko linahitaji hewa nyingi.
3. Usiri, uwepo wa dirisha kubwa chooni inaweza kupelekea mtu wa nje akaona kinachoendelea ndani kwa urahisi zaidi.
Zinaweza kuwepo na sababu nyingine lakini kwa mimi naona hizo ni miongoni mwazo.
2.
 
Sababu kubwa ni mzunguko wa hewa ndani ya nyumba,kawaida upepo lazima uingilie penye upenyo mkubwa utokee padogo

Kwa msingi huo madirisha ya choo yakiwa makubwa yatarudisha harufu ndani ila kwa vile sebuleni na vyumba yanakua makubwa automatically harufu ya chooni itatoka nje kupitia madirisha yake ambayo nimadogo,

Nina imani kwakiasi flani nimekujibu

Hii itasaidia tu kama choo kitakuwa kina changamoto ya kunuka lakini mkuu choo kikijengwa kwa kufuata taratibu zake huwa hakitoi harufu hata kama kitajengwa katikati ya sebule, tatizo letu sie huwa tunajenga vyoo vizuri kwa muonekano yaani unakuta cha kutumia maji na kina tiles za spain (ukiingia kipo vizuri lakini kinanuka), angalia vyoo vingi majumbani kwetu unakuta lile bomba ambalo tunaliita la kutolea hewa chafu unakuta linanyooka vizuri kutoka kwenye chamber likifika usawa wa bati linapindishwa (kukwepa kutoboa bati) alafu linanyooka kwenda juu wakati lilitakiwa utoboe bati litokeze juu likiwa limenyooka liweze kuingiza oxygen na mwanga wa kutosha ili vile vijidudu hata kama havionekani viweze kufanya shughuli yao ya kila siku yaani vinahitaji Oxygen kuweza kuishi ni vina mchango mkubwa wa kuratibu zoezi zima la kuozesha kinyesi hivyo ikiwa oxygen ni ya kutosha vyenyewe vinatoa heat na carbon dioxide (hapa choo hakinuki) lakini kama bomba umepindisha na kama kuna hitilafu kidogo tu lazima choo kitanuka kwa kuwa supply ya oxygen inakuwa ndogo au hakuna kabisa na kusababisha wale wadudu watoe methane na hydrogen sulfide gas ambayo inanuka kama yai viza na hapa ndio chanzo cha harufu (refer anaerobic na aerobic). Na ndio maana unaweza ukakuta choo ni low quality by apperance ila kimefuata misingi sahihi ya ujengaji choo hakinuki alafu vile vyetu ambayo tunaamini ni vizuri vinanuka simply because mtu ameogopa kutoboa bati la SAUZI
 
nimeridhika kwa jibu lako mkuu, kama kuna maoni tofauti anakaribishwa.

Hiyo c sababu coz choo hakitakiwi na harufu mbaya hata kidogo kwa sababu kunakuwa na seal ya maji katika wc na floor trap hiyo yote ni kuzuia harufu kurudi ndani. Soo choo kuwa na dirisha kubwa inaweza saidia kuingiza hewa nzuri ya nje na si hewa chafu

Harufu inayozuiwa na floor trap ni iliyoko kwenye sewage system hilo hakuna shida, wakati anajisaidia mtu pia floor trap inazuia harufu? Hiyo ndio inatakiwa itoke nje ya nyumba kupitia dirisha dogo.

Unaposema choo kuwa na dirisha kubwa inaweza kusaidia kuingiza hewa nzuri, ikishaingia hiyo hewa Nzuri itatokea wapi kama si ndani kutafuta uelekeo wa upande wa pili wa nyumba?

Fanya utafiti mdogo chumba chenye madirisha mawili utaona upepo ukiingia dirisha Hili utatokea upande mwingine

Sasa basi kinachotokea hapa akiingia mtu kujisaidia atafunga mlango ile harufu wakati wa kutoka akifungua mlango hewa inatoka ndani kwenda nje kupitia mlango wa choo to dirisha dogo

Lakini dirisha la choo likiwa kubwa hewa itaingia ndani kwa wingi
 
Ni kweli mkuu ila inategemea na aina ya choo hasa vyoo vya shimo inashauriwa kiwe na dirisha dogo ili lisiruhusu mwanga kupita kiurahisi ndani yaani vyoo vya shimo havihitaji mwanga sana hasa mida ya mchana
gfsonwin I guess we have something in common sababu nimecheka balaa mpaka machozi. Sijaelewa mdau anamaanisha nini kuhusu mwanga kwenye vyoo vya shimo.
 
Last edited by a moderator:
Harufu inayozuiwa na floor trap ni iliyoko kwenye sewage system hilo hakuna shida,wakati anajisaidia mtu pia floor trap inazuia harufu?hiyo ndio inatakiwa itoke nje ya nyumba kupitia dirisha dogo.

Unaposema choo kuwa na dirisha kubwa inaweza kusaidia kuingiza hewa Nzuri ikishaingia hiyo hewa Nzuri itatokea wapi kama si ndani kutafuta uelekeo wa upande wapili wanyumba?

Fanya utafiti mdogo chumba chenye madirisha mawili utaona upepo ukiingia dirisha Hili utatokea upande mwingine

Sasa basi kinachotokea hapa akiingia mtu kujisaidia atafunga mlango ile harufu wakati wakutoka akifungua mlango hewa inatoka ndani kwenda nje kupitia mlango wa choo to dirisha dogo

Lakini dirisha la choo likiwa kubwa hewa itaingia ndani kwa wingi
Mechanism ya airation vyoon ni ya one direction na hii ina maana kwamba hewa haitakiwi kutoka ndani ya choo kwenda nje kwa kupitia mlango tofauti. Kadirisha kadogo kanaruhusu mlango unaposindikwa basi hewa yote ya mle ndani inatoka through hako katundu kadogo. Lakini sasa kwa modern toilets ambazo ni water closet hili swala lina apply vizuri zaidi.

Tukirudi kwenye traditional latrines ambazo ni pit, hizi kwanza mtu hujisaidia kwenye shimo ambalo digestion hufanyika humo humo, sasa basi methane bacterias wengi hawapend mwanga na kukiwa na mwanga mkubwa hushindwa kufanya kazi na nndio mana hufanya kazi vizuri zaid usiku. Lakin pia hawa hawa hufanya kazi katika elevated temps so kukiwa na dirisha dogo inamanaa kwamba kunakuwa na temp ionayostahili kwa ajili ya digestation.

wataalam wa sewage treatment wanaweza kuelezea zaid
gfsonwin I guess we have something in common sababu nimecheka balaa mpaka machozi. Cjaelewa mdau anamaanisha nini kuhusu mwanga kwenye vyoo vya shimo.
 
Sijakupinga mkuu ndio maana nimesema hapa nilipo madirisha ni makubwa, nilikuwa najaribu kujenga hoja. Maana hata mwanga una kiasi kinachotakiwa kwa eneo husika, studio nyingi zina giza kwakuwa hazina madirisha.
Nys watu wengi katika kujenga kwetu tunaona kama chooni ni sehemu ambayo haina msingi au pahali pa kawaida sana tunasahau kupahudumia kama palivyo muhimu kiuhalisia. Mazingira pia huchangia ndio maana vidirisha vya juu tofauti na chumbani. Okay labda tujadili kwanini vyoo vingi vinamadirisha madogo hapo ndio tunaweza kuja na suluhisho.

1st of all, Nilipo bold with red sio sahihi.

1. Chumba na madirisha ya chooni kuwa madogo na yakawa juu zaidi kuliko mengine it is not by mistake, ignorance or omission..Actually it is done following professional aspects in Building Design.

2. Chumba cha choo kuwa kidogo ni sababu ya matumizi yake. Hatuitaji space sehemu ambayo tunatumia asilimia chache sana ya maisha yetu tukiwa nyumbani. Huwezi kukaa 2 hours chooni, huwezi kulala, kupiga stori au vinginevyo..Jiulize pia kwann corridor za nyumba ni nyembamba (1.2 metre) ? Coz tunapita tu pale kwenda chumbani, sitting rum au chooni.

3. Madirisha kuwa madogo, yenye giza kidogo na kuwekwa juu (1.8 metres na kuendelea) Ni sababu ya ya Privacy hata mtu akiwa juu ya ghorofa asikuone, na economical aspect. Toilet is the most private space in the building.

Note: Hivyo vyote hapo juu ni standards but they can change and vary depending on " User Requirements". Mtumiaje hata akitaka choo kama sebule atawekewa tuu.
 
gfsonwin I guess we have something in common sababu nimecheka balaa mpaka machozi. Cjaelewa mdau anamaanisha nini kuhusu mwanga kwenye vyoo vya shimo.

Usicheke mkuu ni kupeana madini kulingana na uelewa, pale napoteleza unaniambia, anyway niliposema sema vyo vya shimo nilimaanisha upande wa wadudu kama nzi hasa kwenye vyoo aina ya VIP (ventilated improved pit latrine) ambavyo huwa kuna lile bomba tunaliita la kutolea hewa chafu ambapo kama mwanga ni hafifu kwenye room maana yake nzi watakuwa attracted na ule mwanga uliopo ndani ya shimo unaopitia kwenye bomba la kutolea hewa chafu / kuingizia oxygen ambalo linakuwa limenyooka na kutokezea kwenye paa na mwisho wa siku wanakuwa hawapandi juu huku kuleta usumbufu na kusambaza maambuzi (utakumbuka zamani tulikuwa tunafunika choo na mfuniko, kadri muda unavyokwenda ndivyo watu wakawa wagunduzi wakaja na hii approach ambapo nzi watabaki kwenye shimo watasaidia na funza kufanya decomposition wakati huo huo wanakuwa wanaufuatilia mwanga kwenye lile bomba ambalo juu kule linakuwa lina wavu na mwisho wa siku life span ya nzi ni fupi wengine wanakufa wanadondoka)

Wataalami wa kinyesi watakuja kutueleza maana wengine ni wazee wa kusikiliza tu (in this case sio kuwepo giza totoro bali ni ile hali ya kunakuwa na mwanga interesting kwa nzi yaani kama vile tunapokaa ndani kuna mwanga wa kutosha ila kuna kasehemu either dirishani unapenya mwanga wa jua)
 
lukelo sakafu siku hizi ana timu kubwa au ndio id nyingi.. maana ndo mfumo wake huu wa maswali
 
Last edited by a moderator:
Ili harufu ya mavi isitoke mapema chooni na watu wasitumie muda mwingi huko
 
-madirisha yana sbb nyingi zikiwemo light, ventilation, view, access, na inaweza kua false window for outdoor appearance, mfano magorofa mengi yenye curtain walls.
-kwa mazingira ya kawaida a space in a building inahitaji (ma)dirisha, katika mazingira mengine hua inakua changamoto/kwa maksudi katika kupangilia na sehemu kama choo au chumba kingine kinaweza kua bila dirisha ila lazima kutakua na means of light (artificial lights) na ventilation (extract fans nk).
-a space (a room, hall, washroom etc) hua na pyschological effect to the user interms of its shape, form, texture, colour, height etc.
mfano makanisa sana sana yaliyojengwa miaka ya zamani hua na umbo kubwa (labda kukupa hisia ukubwa wa Mungu) hua na madirisha madogo na mengine hua na vyoo vya rangi (light intensity hua ndogo labda kukupa hofu kdg, mashaka au labda kukupa faraja kua dhambi zako hazipo peupe) pia hua na ngazi/kitako kikubwa (safari ya mbinguni sio ngazi 2). ivo inawezekana kuna malengo mbali mbali kwa jinsi kanisa lilivyo.
-ukiacha spatial requirements (size ya choo, bafu, sink, kuhitaji nafasi ndogo (from 4sqm) basi pia washroom, with a water closet, washbasin and shower kua na size ndogo inaweza kua ili kujenga mazingira ya privacy. nafkir choo kingekua kikubwa kama sebule hata bila dirisha kubwa ungeweza kuhisi hauko private.
ila pia size ndogo ya chumba inaweza kua na tafsiri nyingine ikija kwenye chumba cha kwa mfano kwenye magereza.
-dirisha dogo la chooni inaweza kua kwanza kwa sababu ya proportions yani mwendano wa size ya room vs size ya dirisha, its strange kama mtoto mdogo wa 2yrs old ukimwekea sahani mezani kubwa sana inakua out of proportions. ila pia kwa mazingira ya wengi tz, madirisha mengi ni madogo pamoja na kupunguza gharama na kuongeza privacy (height huanzia 1800mm).
-labda nimesaidia kdg
 
Nauliza kitu nisaidie wadau ninarafiki yangu anamchumba wake yaani kamsomesha chuo ndo anamaliza mwaka huu mwezi wa saba.Jamaa alipeleka barua juzi lakini mama yake demu katoa nje hataki coz wakristo wote ila madhehebu tofauti na dingi yake demu haongei mama ndo last say. Halafu kinachoumiza zaidi wazazi wake wanajua jamaa kamsomesha mtoto wao. Chakushangaza walengwa wenyewe wanapendana.

Mpe pole, la muhimu hapo ni uelewa wa wazazi wa binti hasa huyo mama. Miaka yote jamaa anamsomesha walikuwa kimya, leo anatangaza nia ya kutaka kumuoa mama wa binti anakataa, siyo sahihi hata kidogo. Huyo mzazi hajiulizi, vipi endapo wangepeana mimba na masomo yakiwa yanaendelea? Ni sababu tu vijana wana heshima na wazazi washukuru katika hilo. Imani sijui madhehebu, ni ya kuyarithi tokea huko kwa wao, la muhimu ni KUPENDANA
 
Kila siku najiuliza kwanini nyumba zinapojengwa madirisha ya chooni hujengwa madogo tena yanakuwa juu?

Je sababu ni nini ?

Karibuni kwa michango yenu.

Posted by: MCHUNGUZI HURU (Associate Professor)

Ni utamaduni tu, ni utaratibu tu. Na hoja yako ya kutaka kufananisha faragha ya choo na ya chumba cha mama na baba, siyo sahihi hata kidogo. Choo kitabaki kuwa choo, na chumba cha wazazi kitabaki kuwa na umuhimu wake. Ukileta ulinganisho huo, maana yake hapo nini? By the way, lini utakuwa Professor kamili? Maana ni miaka sasa bado upo Associated tu.
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom