Kwanini kampuni au biashara yako lazima inahitaji uwe na website(Tovuti)?

Iziwari

Member
Jun 5, 2021
76
56
Karne hii kumekuwa na watu wengi wanao shauri kuwa na tovuti/website kwa ajili ya kampuni au biashara.
Sa nyingine wamekuwa wakitangaza ivo, kwa ajili ya manufaa yao binafsi. Ikiwemo kujipatia kipato kwa kupitia kutengeneza website.

Lakini wanao pokea izo kazi za website wamebaki na swali.

Kwamba ni kwa nini niwe na website ambayo haitembelewi na wateja? Ina manufaa gani?

Na Sababu kubwa ya kuwa na website ,sio nyingine, zaidi ya kuwa na mahali pa kupokea wateja wako.

Nimeamua kuandika hii ili kuwafahamisha vigezo vya kuzingatia pale unapotengenezewa website.

Vigezo ambavyo website inatakiwa kuwa navyo kabla haujaipokea.


1. Iwe inaweza kuonekana vizuri kwenye simu na kwenye computer.
2. Hakikisha ni https mfano Home Page - Swahili. Maana yake alieitengeneza awe ameweka na SSL. Hii ni njia nzuri na kuilinda website yako. For website security. Na uhakika kwa wateja wako watakao itembelea tovuti kwa mara ya kwanza.

3. Iwe na uwezo wa kukurahisishia jinsi ya kuingia na kurekebisha kitu. Maana website za kisasa anatengenezewa mteja, ili na yeye akielekezwa kitu chochote aweze kukifanya kwa urahisi.

4. Ilipiwe angalau kwa mwaka mara moja tu.

5. Hakikisha ipo kwenye hosting yenye infinity bandwidth. Bandwith kwa kiswahili ni kipimo data. Yani uwezo wa watu wengi kufikia data zilizopo kwenye kurasa za tovuti yako.

6. Ulizia kuhusu nafasi iliyotumika kuweka io website. Kama nafasi ni chini ya GB 1 na zaidi. io website itakua haiwezi kuongezewa vitu vingi.

7. Hakikisha website yako inakutangaza. Iwe na blog content. Yani kurasa za blogi ambazo watu wakizitafuta wanakupata kwa kupitia google. au Yahoo au bing.

8.Tovuti yako kabla haujaipokea, hakikisha imeunganishwa na kurasa zako za kijamii kama facebook na instagram.

9. Lazima pia tovuti yako iwe imeunganishwa na Webmaster Tools za Search engines. Ikiwemo ya google na bing. Hii ni kwa ajili ya kufanya website yako kuonekana online kwa urahisi zaidi pale watu wanapo kutafuta.

10.Hakikisha alioitengeneza website yako anakupa link ya wewe kuona idadi ya wateja wanaotembelea website yako kwa mwezi au kwa wiki. Nikimaanisha, unatakiwa kujua utendaji wa tovuti yako mara baada tu ya kukabidhiwa.

11. Tovuti yako hakikisha ina fomu zinazoweza kukuunganisha wewe na mteja ,kutokea kwenye tovuti mpaka kwenye whatsapp ,facebook yako au Email yako.

12. Hakikisha Website yako inafikiwa na wateja si chini ya 50 kwa mwezi. Wanaokuja kuangalia huduma na bidhaa zako. Na Mwenye kuitengeneza akuelekeze jinsi gani ya kuangalia idadi ya wanaoitembelea tovuti yako.

Je! Unataka kuhakikishiwa uwepo wa vitu vyote hivi kwenye tovuti yako?
Na ungependa tovuti yako iwe kitovu cha kukuletea wateja kutoka sehem mbali mbali?

Je unataka tovuti yako ikuoneshe matokeo mkononi? Kutokana na biashara unayo ifanya?

Ikiwa ni chuo au taasisi au mfanyabiashara yeyote hakikisha una pokea website/tovuti inayokutangaza vizuri.

Yenye kuonekana machoni pa watu wengi, inayofanya kazi na inayojiendesha yenyewe mtandaoni.
Tovuti sio picha mtandaoni. Bali ni njia pekee nzuri inayokusababishia upate wateja wengi kutoka sehem mbali mbali.

Na vitu vinavotumika kuwaleta hao wateja kimojawapo ni
Alt text za picha za website yako na Keywords za blog post zako.
Fanya maamuzi sahihi kwa shilingi 250,000 tu, Iziraa Web Developers tutakutegenezea tovuti yenye kila kitu kama nilivokuelekeza hapo juu. Na tutahakikisha tunakupa tovuti mkononi inayokuonesha idadi ya watu wanaokutembelea.

Tumejikita kwenye faida na matokeo ya baada ya kutengenezewa tovuti yako, Na sio kutengeneza tu tovuti.
Karibu Tupo Arusha Jengo la Equity bank Karibu na CRDB bank France Corner. AU tupigie 0756431032.
 
Nikitoa 250,000 kuna gharama zingine? Iyo ni hela ya muda gani?
 
Back
Top Bottom