Kwanini Juvenal Habyarimana alilazimisha kurudi Kigali licha ya taarifa za kiintelijensia

LIKUD

JF-Expert Member
Dec 26, 2012
15,111
27,096
Najiuliza nashindwa kupata jibu, kwanini President Juvenal Habyarimana alilazimisha kurudi i Kigali licha ya kupewa taarifa za ki intelijensia juu ya uwezekano wa kutokea hatari ? Taarifa zinasema kuwa kabla hajapanda ndege kutoka Dar to Kigali , alikuwa alerted asipande ndege siku hiyo lakini yeye akaamua kupanda ndege siku hiyo...Kulikuwa na ulazima gani wa yeye kwenda Kigali siku hiyo hiyo?
 
Mkuu hebu jaribu kumtumia swali lako kwa e-mail huko mbinguni labda atakujibu. Sisi wengine tutakuingiza chaka tu.
 
Cha Kushangaza Ni kumshawishi Rais wa mpito wa Burundi Hayati Cyprien Ntayamirwa kuondoka nae kwenye Ndege yake.
Cha kistaajabisha Familia ya Marehemu Ntayamirwa ilipoenda kudai Bima ya kifo cha Mpendwa wao Ilinyimwa kwa kuwa Hapakuwa na jina la Hayati Cyprien kwenye Manifesto ya Abiria waliokuwemo kwenye Ndege ya General Juvenal Habyarimana ambaye inasadikika Alimaliziwa Akiwa anajikokota kuelekea Nje ya Runway ya Airport ya Chigali
 
Alijaribu zari mbona Nkuruzinza alifanikiwa kufika salama Burundi licha ya hatari?
 
Ukweli ni kwamba, Rais Habyarimana hakutaka kabisa kwendaRwanda, aliyemlazimisha ni Mwalimu Nyerere ,yapo mambo mengi yalitokea Siku hiyo siwezi kuyaweka hapa yote Kwa Sababu maalumu.
ila ni mazito Sana, tuyaache tu. Nikiyawekea thread yake hapa mods watafuta.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom