Sir John Roberts
JF-Expert Member
- Mar 1, 2017
- 9,668
- 16,026
State apparatus ni vyombo vya ulinzi na usalama kwa wasioelewa kimombo. Marehemu John Pombe Joseph Magufuli katika style ya utawala wake aliunda serikali kwa kutumia "State Apparatus personell" kuanzia viongozi wa kisiasa mpaka maofisa waandamizi serikalini. Ilikuwa aidha ni major wa jeshi, brigadier mstaafu au kanali na wengine kutoka vyombo vya ulinzi na usalama: polisi, Usalama wa Taifa, TAKUKURU n.k.
Kiukweli ni Watanzania wachache walimuelewa mzee yule na style yake ya uongozi. Wengi tulilalamika utawala wa kimabavu usiojali uhuru kwa wananchi, demokrasia kwa vyama vya upinzani, uhuru wa vyombo vya habari, Bunge n.k. (Hapa Kazi tu).
Lakini miaka kadhaa baada ya kifo chake, nimeona tofauti kubwa kati ya utawala wa sasa na uliopita kwa namna serikali inavyoendeshwa. Na naweza kusema, Mh. Rais Samia, kwa aina hii ya utawala wako, ukubali na kubeba madhara yake (consequences) na uwe na kifua hasa cha kustahimili hayo yatokanayo.
Sikufundishi namna ya kuendesha nchi, ila tu nakutahadharisha Waswahili tuna msemo: "Ukicheza sana na mbwa utaingia nalo msikitini."
Watakaokuja kuchangia, tafadhali tuchangie kwa ustaarabu. Siyo mlete kejeli na mambo ya siyo na mbele wala nyuma (Watanzania tunapenda porojo).