Kwanini Friends of Simba hawacomenti chochote matokeo ya Simba? Kuna nini?

1979Magufuli

JF-Expert Member
Feb 20, 2023
438
1,752
Jana Simba imepambana sana na matokeo yameniuma sana utadhan nimefiwa na mzazi, haki tena, ila kitu kinanipa taabu sana na kunipa hofu kama kweli Umoja upo Simba, pengine ndio maana matokeo yanazidi kuwa mabaya, sare au kufungwa ndio imekuwa utamaduni wetu, kitu chenyewe ni hiki, nimejaribu kupitia kwenye kurasa za friends of Simba kuona kama wana maoni ya kupongeza timu yetu kwa kupambana jana.

Sioni kabisa wakitoa sapoti ya kuwapa hongera wachezaji kwa kupambana, yaani as if hawajui kama Simba jana ilicheza, hawa watu wabaya sana kiukweli, yaani Simba kucheza kote kule hata kutoa maoni kwenye page zao huwaoni, washabiki na wanachama wamulikeni hawa watu, hawana nia njema na Simba.

Kama mapambano yataendelea hivi nna uhakika matokeo ya sare yataendelea hata kwenye mechi ya marudiano na Wydad, wanaona Simba ikifanya vzr watakosa thamani, wanataka kutuaminisha kuwa bila wao Simba haiendi ila watambue enzi za upigaji hazipo tena.Mtabana had mtaachia.
 
Ao unao waona hawapo na Simba kwakua hawaja comment chocchote juu ya Mechi ndio wenye mapenzi na timu.

Wapongeze Nini wakati kiuhalisia una angalia mechi na kuona dhahiri timu itafungwa na ni kweli imefungwa.
Kilicho kupa wewe tumaini na usiyejua soka ni kwakua timu imefungwa dk za mwisho

Mpaka walipo amua kuanzisha kundi la friends of Simba Ina maana waliguswa na timu, na usifikiri wenyewe awa wasiliani juu ya mwendo wa timu ni kwakua hawataki Nyie mashabiki maandazi mjue wao wanafikiri Nini juu ya timu Yao.

Wanajua uwezo wa timu Yao na hawataki kuwa wanafiq kama Nyie mashabiki maandazi.
Simba haikucheza vizuri ila ilizuia vizuri kwakua viungo wote wa kushambulia na kuzuia pamoja na ma defender walikua compact.
Tatizo linakuja namma ya kutoka kwenye kuzuia na kushambulia kwa Kasi, uo kwao ulikua ni mtihani mkubwa.

Sasa mtachagua Moja apa DAR mtakapo cheza dhidi ya Wydad kama mtakaa Tena compact au mtafunguka ili mshambulie na kuacha nafasi/ kwenye maeneo yenu.
 
Wewe ni mpumbavu kumfananisha kufiwa wazazi na upuuzi wa burudani....! Wenye akili hawawezi kushangilia draw...!
 
Mpira usikufanye uwe mjinga na mpumbavu kiasi hiko. Unakuwa kama umechanganyikiwa, shabikia mpira kiasi tu. Huo ushabiki uliofikia ni mbaya sana hata mwanao anaweza kucheka kwa mambo yake, wewe ukamtandika fimbo kwa kudhani anakucheka wewe kwa kufungwa.
Huwa najitahidi sana katika hili.
 
Mpira usikufanye uwe mjinga na mpumbavu kiasi hiko. Unakuwa kama umechanganyikiwa, shabikia mpira kiasi tu. Huo ushabiki uliofikia ni mbaya sana hata mwanao anaweza kucheka kwa mambo yake, wewe ukamtandika fimbo kwa kudhani anakucheka wewe kwa kufungwa.
Mnaomtilia maanani huyu mnapoteza Muda wenu. Hapa Manula katoka golini yupo Kapombe.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom