Kwanini Dr Slaa ana chuki kubwa sana na Rais Samia?

Nauli zimepanda kutokana na kupanda kwa gharama za uendeshaji.hata hivyo nchi kama kenya kwenyewe bei zilikuwa zimepanda tangia muda tu wakati Tanzania zikiwa hazijapanda licha ya kupanda kwa bei za mafuta .
Mbona Zanzibar hakuna mifumuko ya bei ys kipumbavu kama huku bara
 
Ampende mtu aliyeshindwa kuboresha huduma ya umeme? Kama unampenda mpende kimpango wako. Watu wengi hatumpendi huyo mama laghai.
Wengi tunampenda,labda mvivu,asiyetaka kujishughulisha.Lakini kama unajishulisha,vipato viko nje nje.
 
Mamilioni ya watanzania wanampenda na kumuunga mkono Mh Rais kutokana na uchapa kazi wake ulioleta nuru kwa mamilioni ya watanzania waliokuwa wanaona giza mbele yao.
Acha kujidanganya, niko huku kijijini wasiko jielewa ila bahati mbaya wanatamani kile kipengele cha Ney wa mitego alichoimba
 
Mamilioni ya watanzania wanampenda na kumuunga mkono Mh Rais kutokana na uchapa kazi wake ulioleta nuru kwa mamilioni ya watanzania waliokuwa wanaona giza mbele yao.
Sana.Kazi za kujiajiri ni nyingi tu,ukienda baharini au kokote kwenye uvuvi wa samaki,ukichukuwa samaki kwa jumla,na kuuza reja reja,kipato kipo.Ukienda masokoni ukinunua bidhaa kwa jumla,ukauza rejareja,kipato kipo.Ukinunua maji ya chupa au juice za chupa,ukaweka kwenye ndoo na barafu,ukaenda kwenye mikusanyiko,unapata kipato kizuri tu.Ukichukuwa chubu za gari,ukazikata kata,ukauza kwa wafunga miziko,pesa ipo.Ukinunua mifuko kwa jumla,ukauza masokoni rejareja,pesa ipo.
 
Mkuu Luka, Lucas mwashambwa , siungi mkono hoja!, kwa sisi tunaomfahamu Dr. Wilbroad Slaa tangu akiwa Padri na Katibu Mkuu wa TEC, this is a person of impeccable integrity, jifunze kutofautisha hoja za mtu na kuzitengaanisha na personalities, Dr. Slaa anakosoa kwa hoja za msingi kabisa na sio hoja za chuki dhidi ya mtu yoyote!.

Nakuaminia sana mdogo wangu katika kujenga hoja, nakushauri usianze kuleta hoja za siasa za zengwe na maji taka, kwa hoja za uchimvi, uongo, fitna na majungu!.

Mfano ule Waraka wa TEC kuipinga DPW na Bandari zetu, ukisema Maaskofu Katoliki Tanzania wanachuki na Rais Samia kwasababu 1. Ni Rais Mwanamke 2. NI Rais Muislamu, 3. Ni Rais kutoka nchi nyingine ya Zanzibar 4. Asili yake sio Mtanzania halisi, ana asili ya Waarabu wa Oman!, 5. Mambo ya Intel na IQ ya Samia... utakuwa umewatendea haki TEC?. Kwenye hoja za TEC wana hoja zozote zinazoengemea hoja hizo?.

Ukiusikiliza ukosoaji wa Dr. Wilbroad Slaa, kuna kitu chochote personal amewahi kukizungumza against Rais Samia, mfano hoja hizo?,

Nakushauri usiende personal, tuendelee kukata hoja, endelea kusifu, kumfagilia na kumpigia mapambio ya Kutosha Rais Samia ili usivuke mipaka ukajikuta ni kama unamuabudu fulani na kumtukuza, ukamponza bure!. Wa kuabudiwa, kutukuzwa na kusujudiwa ni Mungu pekee!

P
Hoja yako ni dhaifu.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Haihitaji akili kubwa sana wala shahada ya chuo kikuu wala kusubiri kuambiwa wala kupewa ufunuo katika kutambua kuwa Dr Slaa Ni mtu ambaye kifua na moyo wake unaonyesha kuwa na chuki kubwa sana na Rais wetu Mh mama Samia Suluhu Hasssan. Ukisikiliza maneno ya Dr Slaa kwa nyakati na vipindi tofauti tofauti wakati huu wa Urais wa Rais Samia unaona wazi kabisa kuwa kaelemewa na hasira,kinyongo na maumivu makubwa ndani ya moyo wake dhidi ya Rais Samia.

Jaribuni ndugu zanguni kufuatilia maneno ,matamshi ,kauli , mazungumzo na hata matendo ya Dr Slaa miaka mitano iliyopita na Dr Slaa wa wakati huu wa Rais samia, ili muelewe hiki nachokiandika hapa kuwa Dr Slaa kuna jambo linamsumbua sana moyoni na akilini mwake.amebeba mzigo wa maumivu ,maumivu yakuona Rais Samia akifanikiwa kwa kiasi kikubwa na kuungwa mkono na mamilioni ya watanzania tofauti pengine na matarajio yake yeye mwenyewe.

Sasa maumivu hayo yameshindikana kutunzika katika moyo na kifua chake na sasa kaamua kutoa sauti yake.sasa anawapangia watu mambo ya kusema,sasa hataki na anaumia sana anapoona watu wakimponge Rais Samia.hataki watu wafanye hivyo maana anaumia.hataki vijana kwa maelfu yao wampongeze Rais samia baada ya kupata ajira baada ya kusota mitaani kwa miaka mingi,hataki wakulima wanaoendelea kuneeemeka na mbolea za Ruzuku pamoja na bei nzuri za mazao wampongeze Rais samia kwa juhudi zake za kuinua kilimo na mkulima.

Hataki wazazi wampongeze Rais samia baada ya kuwatua mzigo wa kulipa ada kama walivyokuwa wanafanya awali,hataki vijana wa vyuo vikuu wampongeze Rais samia baada ya kuwa sasa wote wenye sifa wanapata mikopo bila shida yoyote ile,hataki watumishi wa umma wampongeze Rais samia baada ya kuongezewa mishahara kwa 23% hasa wale wa kima cha chini baada ya kusota wakisubiri kwa miaka mingi,hataki watumishi ambao sasa wamepandishwa madaraja,kulipwa malimbikizo ya madeni na kupewa nyongeza ya mshahara kila mwaka wampongeze Rais samia.

Dr Slaa hataki na anaumia sana anapoona wafanyabiashara wakimpongeza Rais samia kwa kuweka mazingira mazuri ya biashara na uwekezaji,Dr Slaa hataki kuona Rais Samia akipongezwa kwa kuiheshimisha nchi yetu kimataifa mpaka sasa tumerudishwa kwenye mpango wa millenium challenge huku miradi ya maendeleo ikiendelea kutekelezwa kila kona ya nchi yetu.

Sasa kwanini Dr Slaa hataki tumpongeze Rais wetu? Kwanini anaumia sana? Mbona awali alikuwa mtoa sifa na pongezi mzuri sana na alituasa hata watanzania kupongeza juhudi na kazi kubwa sana iliyokuwa ikifanywa na serikali ya awamu ya tano? Kwanini leo iwe kama kosa au jinai kumpongeza Rais samia kwa kazi kubwa na uchapa kazi wake uliotukuka ulioliletea maendeleo makubwa Taifa letu ndani ya muda mfupi?

Anataka nini Dr slaa? Kwani yeye anatakaje? Anataka tuseme nini pale Rais wetu anapofanya vizuri?

Napenda kusema na kumwambia Dr Slaa kuwa Rais Samia ni mpango wa Mungu Mwenyewe,hakuinuliwa kwa mkono wa mwanadamu bali na mkono wa Mungu Mwenyewe,hivyo hawezi kushushwa na mikono wala maneno ya mwanadamu mwenye chuki zake binafsi. Atapambana sana lakini hataweza kumshusha mama yetu.ukiinuliwa na Mungu mwanadamu hawezi kukushusha.ukipewa kibali na Mungu mwanadamu hawezi kukuzuia kupita na kukubalika mahali popote pale.Mungu yupo upande wa Rais Samia na Anaendelea kumpatia njia na maarifa ya kuongoza Taifa letu.

Uzuri wa Rais wetu yeye hakatishwi tamaa wala kunyong'onyeshwa na maneno au chuki ya mwanadamu .siku zote yeye hutizama mbele kwa matumaini na ujasiri wa hali ya juu katika kuyakabili matatizo na Changamoto mbalimbali ili kuwatua mizigo Watanzania.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel mwashambwa Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742- 676627.
Dkt Slaa kama watanzania wengine wengi yaani wapiga kura hawamchukii Rais Dkt Samia bali wanachukia aina yake ya uongozi unaoruhusu ufujaji wa rasilimali za nchi, kwa hiyi chuki ipo kwenye uongozi. Na ndiyo maana watu wanatamani awamu ya 5 irudi ili umeme usikatike tena! Jibu lako wewe chawa jinga ni kuwa umeme kukatika ni moja ya hizo chuki hivyo hakuna ujinga wa kusema mvua wala nini maana aliyefariki alikuwa Dkt Magufuli peke yake sasa hawa waliobaki mbona wameshindwaaa???? Yaani una mamlaka yote hayo ya rais kazi yako kutukana stupid????? Yaani serikalini sasa kila mtu kamba
 
Crap from hopeless mind.

Hakuna anayemchukia Samia kama mwanadamu, bali anayoyafanya au Serikali yake inayoyafanya, yanaweza kumfanya apendwe au achukiwe.

Hakuna mwenye akili timamu anayeweza kufurahia na kuunga mkono ugawaji wa rasilimali kama bandari, hifadhi za wanyama na misitu kwa waarabu kwa mikataba ya hovyo.

Hakuna mwenye akili timamu anayeweza kumwunga mkono kwa danadana zake za kuwafanya watu wote hawana akili kama alivyo Mwashambwa, kwenye suala la katiba mpya ambayo inastahili kuwa mwongozo wa kila mtu katika wajibu wake.

Hakuna mwenye akili timamu, labda uwe huna akili kama Mwashambwa, anayeweza kusema anaunga mkono kitendo cha Rais aliyeapa kuilinda katiba ya nchi, na akamwomba Mungu amsaidie kukiishi kiapo chake, halafu anakuja kudharau katiba na kudai ni kijitabu kisicho na msaada wowote kwenye maendeleo (kwa maneno yake, katiba ni kijitabu. Kijitabu hakiwezi kuleta maendeleo).

Mwashambwa ufahamu kuwa watu wajinga, mliokosa upeo, akili na ukweli wa nafsi, mpo wachache. Ndiyo ninyi wajinga mnaosifia kila aina ya ujinga. Lakini ni ujinga uliotokana na uwezo duni wa kuyasimamia maisha yenu, ndio unaowafanya muamue kujitoa ufahamu, kiasi cha kuwa kama mbwa koko wanaotarajiwa kurushiwa japo mfupa, watawala wakishakula nyama.

Pole sana kwa sababu rushwa yako ya sifa za kinafiki kwa Rais Samia na Dr. Tulia haijazaa matunda uliotarajia. Na kwa sababu ya akili ndogo unaamini kuwa hujarushiwa japo kamfupa kwa sababu hawajaiona namba yako ya simu.
Hoja dhaifu.Utagawaje kitu kisichohamishika.Au kitu kinachozaana.
 
Mkuu Luka, Lucas mwashambwa , siungi mkono hoja!, kwa sisi tunaomfahamu Dr. Wilbroad Slaa tangu akiwa Padri na Katibu Mkuu wa TEC, this is a person of impeccable integrity, jifunze kutofautisha hoja za mtu na kuzitengaanisha na personalities, Dr. Slaa anakosoa kwa hoja za msingi kabisa na sio hoja za chuki dhidi ya mtu yoyote!.

Nakuaminia sana mdogo wangu katika kujenga hoja, nakushauri usianze kuleta hoja za siasa za zengwe na maji taka, kwa hoja za uchimvi, uongo, fitna na majungu!.

Mfano ule Waraka wa TEC kuipinga DPW na Bandari zetu, ukisema Maaskofu Katoliki Tanzania wanachuki na Rais Samia kwasababu 1. Ni Rais Mwanamke 2. NI Rais Muislamu, 3. Ni Rais kutoka nchi nyingine ya Zanzibar 4. Asili yake sio Mtanzania halisi, ana asili ya Waarabu wa Oman!, 5. Mambo ya Intel na IQ ya Samia... utakuwa umewatendea haki TEC?. Kwenye hoja za TEC wana hoja zozote zinazoengemea hoja hizo?.

Ukiusikiliza ukosoaji wa Dr. Wilbroad Slaa, kuna kitu chochote personal amewahi kukizungumza against Rais Samia, mfano hoja hizo?,

Nakushauri usiende personal, tuendelee kukata hoja, endelea kusifu, kumfagilia na kumpigia mapambio ya Kutosha Rais Samia ili usivuke mipaka ukajikuta ni kama unamuabudu fulani na kumtukuza, ukamponza bure!. Wa kuabudiwa, kutukuzwa na kusujudiwa ni Mungu pekee!

P
Naunga mkono hoja
 
Suala la umeme ni changamoto ya muda na baada ya hapo itabaki kama historia katika vitabu.kwa sababu mapema mwakani kuna mtambo unakwenda kuwashwa katika bwawa la mwalimu Nyerere ambapo utatupatua megawati zutakazounganishwa katika grid ya Taifa. Na hatua hiyo itakuwa ikifanyika kwa awamu mpaka mitambo yote itakamilika kuwashwa kwa mtindo huo na hivyo kupata megawati zaidi ya 2115 umeme ambao tutatumia hadi na kubakiza mwingine.huku mwingine tukiendelea kupata kwenye mabwawa yetu,mfano Mteta lenye uwezo wa kuzalisha megawati 80.
Hawana hoja,unaweza kuta mtu analalamika kuhusu umeme ,wakati ni nyumba anatoishi,anashindwa kulipia luku,anauona umeme kwa majirani tu.
 
Wewe siku zote huwa unaandika vitu kiuongo uongo na kizushi tu. Embu niwekee hapa huo ushahidi wa kusema rasilimali zetu zimegawiwa kwa waarabu. Kwani ulikuwa mgonjwa au ICU wakati mkataba mzuri uliopongezwa na mamilioni ya watanzania ulipokuwa unasainiwa? Mkataba ulioonyesha kuwa ni wa muda wa miaka 30 tofauti na nyie wapotoshaji na wanafiki mliokiea mnasema mkataba ni wa milele? Hufahamu kuwa mkataba wa sasa pia utakuwa au unakipengele kinachoeleza kuwa kutakuwa kunakuwa na mapitio ya utekelezaji wa mkataba kila baada ya miaka mitano? Hufahamu kuwa mkataba wa sasa ambao utachochea na kuongeza ufanisi pale bandarini unahusu bandari ya Dar es salaam pekee na tena ni kwa baadhi ya tu ya maeneo ya siyo eneo lote tofauti na nyie wapotoshaji ,wanafiki ,waongo na wachonganishi mliokuwa mnasema bandari zote za Tanzania Bara zimetolewa bure?

Suala la katiba japo hapa naona umeonyesha uwezo wako mdogo na kutoelewa kinachoendelea hapa nchini. Kwa kukusaidia fuatilia majadiliano na mawasilisho wakati wa uwasilishaji wa ripoti ya kikosi kazi. Upatikanaji wa katiba mpya upo katika mchakato na kila mdau na mtanzania yeyote yule anaelewa dhamira njema ya serikali ya CCM chini ya uongozi shupavu na madhubuti wa Rais samia katika kuwapatia katiba mpya Watanzania.
Wananchi tumekuelewa.
 
Ni Rais Samia mpaka 2030 .hiyo ndio kiu ya watanzania. Na lazima wapewe chaguo lao watanzania ili kukata kiu yao ya kuhitaji utumishi wa Rais samia,ambaye amefanya mambo makubwa sana ndani ya muda mfupi katika kuleta maendeleo ndani ya Taifa letu katika kila eneo
1:Mkapa alijenga uwanja wa dsm
2:Kikwete akajenga UDOM
3:Magu akajenga SGR
Hebu tuambie mama kafanya nini kiasi cha kumpamba kiasi hiki? hadi mnakera!
 
Back
Top Bottom