Kwanini Chadema/BAWACHA wanaingilia Uhuru wa mahakama suala la akina Mdee? Hawa ndio wanaimba utawala wa sheria?

chiembe

JF-Expert Member
May 16, 2015
12,012
20,685
Chadema ni wazi kwamba wanajinasibu kwamba wanapenda saaana katiba na utawala wa sheria, na wamekaza shingo na meno wakitaka katiba mpya.

Kwa nini wanataka kuingilia Uhuru wa mahakama inayosikiliza kesi ya akina Mdee na kushinikiza wao ndio wawe washindi? Yaani ili haki iwe haki basi inabidi wapewe wao?

Hizi ni tabia za kidikteta, wamezianza mapema kabla ya kukabidhiwa nchi, wakikabidhiwa nchi, ukashitakiana na Chadema lazima ushindwe.

Ndio maana sioni umuhimu wa katiba mpya wanayodai.
 
Chadema ni wazi kwamba wanajinasibu kwamba wanapenda saaana katiba na utawala wa sheria, na wamekaza shingo na meno wakitaka katiba mpya

Ndio maana sioni umuhimu wa katiba mpya wanayodai
Kiembe kwani wewe ni mmoja wa covid-19,🤔
 
Tanzania hakuna mahakama bali kuna majengo ya mahakama yanayoendeshwa na Makada wa CCM. Kenya hapo kulikuwa na kesi ya uchaguzi wa urais, imeisha muda mrefu, hapa kuna shida gani kwenye mahakama hizi za wahuni kesi haifiki mwisho?
 
Hapakutakiwa kabisa kuwepo na kesi mahakamani kuhusu hao wanawake, wameadhibiwa kwa sheria na taratibu za chama chao kama ambavyo wengine kabla yao waliadhibiwa.

Kosa lilianzia kwa Spika wa bunge kuwapa nafasi ya kwenda mahakamani huku akijua fika wameshapoteza sifa ya kuwa wabunge, ni vyema malalamiko yako ungeyaelekeza kwa Spika Tulia.

Hivyo, haya malalamiko yako uliyoleta hapa ni batili, kwanini hujauliza nini kilimfanya Spika asiheshimu maamuzi ya Chadema kama watangulizi wake walipoamua kwenye kesi kama ya kina Mdee?
 
Tanzania hakuna mahakama bali kuna majengo ya mahakama yanayoendeshwa na Makada wa CCM. Kenya hapo kulikuwa na kesi ya uchaguzi wa urais, imeisha muda mrefu, hapa kuna shida kwenye mahakama hizi za wahuni kesi haifiki mwisho?
Hiyo mahakama ya wahuni ndiyo ilimuachia Mbowe?
 
Chadema ni wazi kwamba wanajinasibu kwamba wanapenda saaana katiba na utawala wa sheria, na wamekaza shingo na meno wakitaka katiba mpya.

Kwa nini wanataka kuingilia Uhuru wa mahakama inayosikiliza kesi ya akina Mdee na kushinikiza wao ndio wawe washindi? Yaani ili haki iwe haki basi inabidi wapewe wao?

Hizi ni tabia za kidikteta, wamezianza mapema kabla ya kukabidhiwa nchi, wakikabidhiwa nchi, ukashitakiana na Chadema lazima ushindwe.

Ndio maana sioni umuhimu wa katiba mpya wanayodai.

Tatizo la kesi za kisiasa wanasubiri maelezo kutoka juu🤔
 
Hiyo mahakama ya wahuni ndiyo ilimuachia Mbowe?
Kwa taarifa yako watu tunaenda kwenye hizi mahakama za hapa nyumbani sio kwa ajili ya kuziamini, bali hatuna jinsi. Kama ingekuwa kuna uwezekano tungekuwa tunatumia mahakama za kimataifa ili kupata haki. Huwa nawaelewa sana wawekezaji kwa kuamua kutumia mahakama za kimataifa maana wanajua kiwango cha upuuzi ulioko kwenye mahakama zetu.

Mbowe aliachiwa kwakuwa hakuwa na kesi bali alibambikiwa. Na tena hiyo mahakama ingekuwa huru wala kesi ya Mbowe isingechukua hata wiki mbili. Kwenye kesi ile ndio nilijiridhisha ni kwa jinsi gani mahakama hizi zinavyotumikia siasa chafu.
 
Alipoachiwa Mbowe mlishangilia!!! Sasa shida nini?

Mkojo kwani kuna aliyeshangilia kwa kazi ya mahakama, watu walishangalia Mbowe kutofanyiwa uonevu kwa kukaa gerezani. Hakuna popote mahakama ilisifiwa maana yenyewe ilikuwa ni sehemu ya uonevu aliokuwa anafanyiwa Mbowe.

Isitoshe sio mahakama ilimuachia Mbowe, bali DPP ndio alisema hana nia ya kuendelea na kesi. Mahakama yenyewe ilikuwa inafuata inachoagizwa na serikali, na sio ushahidi uliokuwa unatolewa mahakamani.
 
Wakati mwingine inatakiwa tuwe logic kidogo;
Kesi kama ya Akina Mdee ilihitajika kuendeshwa kwa dharura na haraka kama kesi ile ya kupinga matokea ya urais Kenya.
Sababu:
1. Kuokoa gharama ambazo ni kodi ya wananchi iwapo watakutwa na hatia ya kuwa wabunge kinyume na utaratibu.
2. Kupatikana kwa wabunge sahihi ili waweze kufanya kazi za kibunge kwa ajili ya kuwaletea wananchi maendeleo.
Siyo kila kitu tunaingiza ujinga, unless kama serikali haitumii kodi ya wananchi wake kuwalipa Akina Mdee.
 
Tatizo la taifa letu ni kuwa idadi ya vilaza wenye vyeti inaongezeka kwa kasi ya ajabu. Hawa vilaza baada ya kupewa hifadhi ndani ya chama kikongwe kilichozeeka ndio hao hao watunga sheria na watafsiri sheria!
 
Back
Top Bottom