Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 1,902
- 945
MHE. KILUMBE NG'ENDA - AHOJI KWANINI BEI YA MAFUTA ISIWE MOJA KAMA UMEME NCHINI
Mbunge wa Kigoma Mjini, Kilumbe Ng’enda amehoji bungeni kwa nini serikali isiwezeshe bei ya mafuta aina ya petrol, dizeli na mafuta ya taa iwe moja nchi nzima kama ilivyo kwa bei ya umeme kwa unit.
Ng’enda ametoa hoja hiyo Jumatano Mei 31, 2023 wakati akichangia mjadala wa kupitisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Nishati kwa mwaka wa fedha 2023/2024, bungeni jijini Dodoma.