Kwani tukiacha madirisha haya ya aluminiam na PVC, ndiyo kusema sisi hohehahe hatuna madirisha yetu mengine ya kisasa jameni?

Hayo madirisha ni malumuu kwa maeneo yenye baridi mfano arusha, moshi, iringa, na mbeya hata Rukwa,

Sasa wabongo sisi wazee wafasheniiz tumejikuta mpaka maeneo ya joto tunafunga vioo kwakua tumeamua acha twende tutafanyaje Sasa

Wale walioishi nje ya inchi na ndani ya nchi maeneo yenye baridi watakuwa mashahidi maeneo ya baridi dirisha la kioo ndio mahala pake ili baridi isingie ndani

Hii sawa ya ujenzi wa nyumba

Mfano dar es salaam wangapi mmeona nyumba za matofari ya kuchoma kwa sababu ipi hakuna ni kutokana na upatikanaji wa udongo wa kufuatilia hizo tofari ni adimu sana, tofauti na Rukwa, iringa, songea na mbeya uko ndio penyewe kwa tofari za kuchoma maana udongo upo na unafaa

Sasa ni ajabu uende eneo ambalo mchanga mwingi unakomaa na kutafuta tofari za kuchoma badala ya block
Sahizi Dar kuna baridi dirisha ni sahihi kabisa sifungui ila ndani full pupwe
 
Yanaingizaje mbu?

Kati kati ya zile sliders mbili za vioo kuna upenyo mdogo, kwa mbu ni hallway ya mita 500

Ikifika saa 12 jioni inabidi ufunge, yawe sealed shut, la sivyo utalia, ndani panakua nje, bora hata nje

Ukifunga jiandae na 'suffocation' ya kutosha , ikifika saa 3 usiku uyafungue tena, ukisahau ukalala hivyohivyo bila 'AC' kuwa ON (sio feni)

Kesho asubuhi jiandae na 'kizunguzungu'
 
kati kati ya zile sliders mbili za vioo kuna upenyo mdogo, kwa mbu ni hallway ya mita 500

ikifika saa 12 jioni inabidi ufunge, yawe sealed shut, la sivyo utalia, ndani panakua nje, bora hata nje

ukifunga jiandae na 'suffocation' ya kutosha , ikifika saa 3 usiku uyafungue tena, ukisahau ukalala

iyoivyo bila 'AC' kuwa ON ( sio feni )

kesho asubuhi jiandae na 'kizunguzungu'
Hahahah asante mkuu nilitaka nithibitishe hili kumbe wewe pia ni muhanga mzee! Mie nilijiuliza sana hili swali hadi juzi nilipoamua kwenda kuchunguza mwenyewe wakati natoka kwenda kibaruani! Nikagundua kweli kuna huo upenyo maana toka yamewekwa haya madirisha nishashikwa na malari4 juzi tena nimekutwa na 3 mbu ni wengi kinyama sahizi nimeamua nayafunga tu uzuri kuna ka ubaridi sikuhizi!

Ila ikifika mwezi wa 9 ni msala joto litapoanza! Nafikiri kuna rubber ilitakiwa iwekwe pale katikati kwenye design ila wabongo hawaiweki! Sababu kwenye magari hio rubber ipo
 
Hayo madirisha ni malumuu kwa maeneo yenye baridi mfano arusha, moshi, iringa, na mbeya hata Rukwa,

Sasa wabongo sisi wazee wafasheniiz tumejikuta mpaka maeneo ya joto tunafunga vioo kwakua tumeamua acha twende tutafanyaje Sasa

Wale walioishi nje ya inchi na ndani ya nchi maeneo yenye baridi watakuwa mashahidi maeneo ya baridi dirisha la kioo ndio mahala pake ili baridi isingie ndani

Hii sawa ya ujenzi wa nyumba

Mfano dar es salaam wangapi mmeona nyumba za matofari ya kuchoma kwa sababu ipi hakuna ni kutokana na upatikanaji wa udongo wa kufuatilia hizo tofari ni adimu sana, tofauti na Rukwa, iringa, songea na mbeya uko ndio penyewe kwa tofari za kuchoma maana udongo upo na unafaa

Sasa ni ajabu uende eneo ambalo mchanga mwingi unakomaa na kutafuta tofari za kuchoma badala ya block
Ninakubaliana nawe!
 
Mtoa mada ungeweka na picha. Maana Binafsi sifahamu hayo madirisha ya PVC yapoje Au Yale ya Allminium si ndio hayo ya PVC?

Pia kuna baadhi ya maeneo kuna mchwa sana. Hivyo haya yenye kutengenezwa na Mbao yanaishia kutafunwa na Mchwa.
 
Mtoa mada ungeweka na picha ningekupenda. Maana Binafsi sifahamu hayo madirisha ya PVC yapoje?

Pia kuna baadhi ya maeneo kuna mchwa sana. Hivyo haya yenye kutengenezwa na Mbao yanaishia kutafunwa na Mchwa.
Sawa! Nikipata nitaweka picha. Kuhusu mchwa, mpaka nikaleta hii mada, ujue nilishawaza mengi sana, Kila njia ninayowaza ina changamoto zake. Ndiyo maana nikalileta jambo hili kupata mawazo mbalimbali. Penye wengi hapaharibiki neno.
 
kati kati ya zile sliders mbili za vioo kuna upenyo mdogo, kwa mbu ni hallway ya mita 500

ikifika saa 12 jioni inabidi ufunge, yawe sealed shut, la sivyo utalia, ndani panakua nje, bora hata nje

ukifunga jiandae na 'suffocation' ya kutosha , ikifika saa 3 usiku uyafungue tena, ukisahau ukalala

iyoivyo bila 'AC' kuwa ON ( sio feni )

kesho asubuhi jiandae na 'kizunguzungu'
Haya madirisha hata kwenye baridi bado ni shida, kale kaupenyo kati ya dirisha moja na jingine huwa kanapitisha baridi sana, kifupi siyapendi...
 
kati kati ya zile sliders mbili za vioo kuna upenyo mdogo, kwa mbu ni hallway ya mita 500

ikifika saa 12 jioni inabidi ufunge, yawe sealed shut, la sivyo utalia, ndani panakua nje, bora hata nje

ukifunga jiandae na 'suffocation' ya kutosha , ikifika saa 3 usiku uyafungue tena, ukisahau ukalala

iyoivyo bila 'AC' kuwa ON ( sio feni )

kesho asubuhi jiandae na 'kizunguzungu'
Hakyamungu wewe unayajua haya madude. Kha! Kweli kabisa mkuu
 
Hakyamungu wewe unayajua haya madude. Kha! Kweli kabisa mkuu

Hahahaha, nakumbuka wakati nahamia kwenye hiyo nyumba ( kitambo kidogo )

Changamoto ya mbu iliniumiza kichwa kujua wapi wanaingilia

Suspect ya kwanza ilikua chini ya mlango wa kuingilia, nikaweka tambala, jioni yake mambo yaleyale , nikasema poa nimeshindwa

Siku za mbeleni, niko dirishani kabisa napiga chabo dada flani kwa nje ( yeye hanioni ) ilikua mishale ya saa 12 ivi , ghafla naona hawa viumbe wakifanya yao kinamna hii 👇

mchoro.png

Hiyo zigzag path ni vile wanajigongagonga kwenye slider ya nje then ya ndani, ya nje, ya ndani , ya nje ya ndani huku akiongoza mbele kwa shida, uyooooooo mpaka ndani.
 
Hahahah asante mkuu nilitaka nithibitishe hili kumbe wewe pia ni muhanga mzee! Mie nilijiuliza sana hili swali hadi juzi nilipoamua kwenda kuchunguza mwenyewe wakati natoka kwenda kibaruani! Nikagundua kweli kuna huo upenyo maana toka yamewekwa haya madirisha nishashikwa na malari4 juzi tena nimekutwa na 3 mbu ni wengi kinyama sahizi nimeamua nayafunga tu uzuri kuna ka ubaridi sikuhizi!

Ila ikifika mwenzi wa 9 ni msala joto litapoanza! Nafikiri kuna rubber ilitakiwa iwekwe pale katikati kwenye design ila wabongo hawaiweki! Sababu kwenye magari hio rubber ipo
Ndivyo vitu wabunifu wetu na wahandisi wanapaswa kuvijua hivi. Mimi yananiudhi vile pande moja linaendelea kuziba dirisha miaka yote.
 
hahahaha, nakumbuka wakati naamia kwenye iyo nyumba ( kitambo kidogo )

changamoto ya mbu iliniumiza kichwa kujua wapi wanaingilia

suspect ya kwanza ilikua chini ya mlango wa kuingilia, nikaweka tambala, jioni yake mambo yaleyale , nikasema poa nimeshindwa

siku za mbeleni , niko dirishani kabisa napiga chabo dada flani kwa nje ( yeye hanioni ) ilikua mishale ya saa 12 ivi , ghafla naona hawa viumbe wakifanya yao kinamna hii 👇

View attachment 1828400

iyo zigzag path ni vile wanajigongagonga kwenye slider ya nje then ya ndani, ya nje, ya ndani , ya nje ya ndani huku akiongoza mbele kwa shida, uyooooooo mpaka ndani
Yes! Mimi naijua hii njia, Na hawa wadudu wanasense balaa. Wanafurukuta hapo mpaka wanatoboa.
 
Mleta Uzi una point sana aisee wewe ni peponi moja kwa moja now kwangu nimeweka grill tu nimetia na nyavu basi kwa sasa kwani kuna jirani yangu kayaweka anapata tabu sana fikiria umeiweka dirisha la 5×5 ukiweka hayo madrisha maana yake dirisha linakuwa 2.5
Basi ukitaka dirisha la 5.5 unajenga Dirisha la 8.5 problem solved
 
kati kati ya zile sliders mbili za vioo kuna upenyo mdogo, kwa mbu ni hallway ya mita 500

ikifika saa 12 jioni inabidi ufunge, yawe sealed shut, la sivyo utalia, ndani panakua nje, bora hata nje

ukifunga jiandae na 'suffocation' ya kutosha , ikifika saa 3 usiku uyafungue tena, ukisahau ukalala

iyoivyo bila 'AC' kuwa ON ( sio feni )

kesho asubuhi jiandae na 'kizunguzungu'
I say umenifungua macho. Mwezi uliopita nilikuwa Dodoma kwenye hoteli yenye madirisha ya aina hiyo. Basi usiku kwa kuogopa baridi nilikuwa najifungia kikamilifu. Yaani ikifika alfajiri nilikuwa nasikia kizunguzungu mpaka nikadhani labda nimepata ugonjwa fulani hivi.

Kwa kweli niliteseka kwa siku zote tano nilizokuwepo pale.
 
Pole sana bibie, fresh air ni muhimu sana, wengi huwa hatujui thamani yake kwakuwa tu ipo muda wote au hatujawahi wekewa 'mitungi ya kupumulia'

Tunapewa hewa bure then tunailimit kwa kuji-seal kwenye makontena
 
Back
Top Bottom