Kwako Waziri Ummy Mwalimu kuhusu maambukizi ya COVID-19: Watanzania tunahitaji kupewa taarifa za kila siku (Daily Updates)

M-mbabe

JF-Expert Member
Oct 29, 2009
13,203
23,020
Kichwa cha uzi kimejitosheleza.

Watanzania tunahitaji kujua kinachoendelea kuhusu hili janga. Source ya taarifa za jambo kama hili yapaswa iwe ni mamlaka husika, ambayo ni wizara inayoshughulikia masuala ya afya (hapa Tanzania wizara hii ina jina refu sana).

Upande wa pili wa muungano (Zanzibar) walau wao wanajitahidi kiasi chake. Huku Tanganyika bado sana.

Taarifa hizi ziwe zinatolewa na waziri mwenye dhamana kila siku kupitia tv stations zote kabla ya taarifa ya habari ya saa 2 usiku.

Taarifa hizi ziwe na data muhimu zifuatazo (at the minimum):

1. Tarehe ya vipimo
2. Idadi ya waliofanyiwa vipimo siku hiyo
3. Idadi ya maambukizi siku hiyo
4. Idadi ya vifo siku hiyo
5.B/down ya maambukizi kimkoa siku hiyo
6. Idadi cumulative kwa vipimo vyote
7. Idadi cumulative kwa maambukizi
8. Idadi cumulative kwa vifo
9. Idadi cumulative kwa waliopona

Hapo juu kwenye namba 2 hadi 5.... hata kama idadi yake ni "zero", itamkwe hivyo. Muhimu ni taarifa iwe public.

Ni katika kuboresha uwazi (transparency).
================================
update 21 April.... msisitizo.

sijui kama Ummy Mwalimu huwaga anapitia huku JF.

seriously speaking, tunahitaji daily updates or else hii attitude yenu CCM itawa cost vibaya sana October.

wananchi wanasikia tu rais wao kajichimbia kijijini kwake ambapo walitegemea awe mstari wa mbele katika hii vita kama tunavyoona marais wa nchi nyingine wanavyofanya.

Tanzania hali ni mbaya sana kuliko watu wanavyosikia na kuona. hii siyo exaggeration - ni fact ambayo ipo supported na numbers.

ndani ya wiki 2 tu tumeshuhudia maambukizi nchini kwetu yakioengezeka exponentially (ongezeko la 916% au zaidi ya mara 10!!)

katika global perspective, Tanzania ni moja ya nchi zilizo na the worst recovery rate ya walioambukizwa - in fact, tunazidiwa na nchi zote zinazotuzunguka, hata DRC wametuzidi.

hapa chini ni COVID-19 recovery rate hadi kufikia asubuhi ya leo kwa nchi jirani na Tanzania:

Burundi 80%
Uganda 68%
Rwanda 54%
Zambia 54%
Kenya 24%
Mozambique 20%
Malawi 18%
DRC 10%
Tanzania 4%

hii trend ni ushahidi tosha kuwa serekali yetu haina mkakati wowote kwenye hii vita. inategemea zaidi bahati na neema ya Mungu. recovery kingekuwa ni kipimo kizuri cha uthabiti wa serekali katika ku deal na hii situation.

WE NEED DAILY UPDATES UMMY!!
 
Hivi Tanzania ina mkuu kama Chief Medical Officer wa nchi yetu hii or? Why wasio wa medical ndio watoe updates na kuongea na press?

Waziri wa Afya kwanini anatumia twitter kuretweet tweets za wengine zenye info na maelekezo ambayo yeye Waziri hayasemi kwa wananchi? Ni maajabu sana
 
M-mbabe, Tanzania ni nchi ya peke, dunia nzima katika hili janga la covid nchi zote duniani ikiwemo korea kasikazini zina toa taarifa kwa raia wao kila siku kuhusu ugonjwa wa covid, maRaisi wao wanaongea na wananchi wao kila wakati , ila kwetu sijui viongozi wetu wamelala au hawajui kinacho endelea Duniani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Anavaa
Sijawahi KUMUONA Waziri huyu kavaa barakoa... Ni hatari sana kwake na watu anaokutuna nao na Wasaidizi wake pia

Jr
Screenshot_20200420-130426_Twitter.jpeg


♡♤Life belongs to all who struggle for it♤♡♧
 
Sijawahi KUMUONA Waziri huyu kavaa barakoa... Ni hatari sana kwake na watu anaokutuna nao na Wasaidizi wake pia

Jr
Siku moja Waziri wa Maliasili alienda kwa Bwana Nyuki, kufika akataka aingie aone mizinga ya nyuki bila kibali, akalazimisha kuingia akijinadi kuwa yeye ni Waziri kwani hajui hadi amwambie awe na kibali?

Dah kuingia kule ndani nyuki wakaanza kumuuma, akaomba msaada kwa Bwana Nyuki, akamjibu akamwambia Waambie wewe ni Waziri, kwani hawakujui?
 
Back
Top Bottom