Kwako Mzee Kinana; Kama kweli mmedhamiria kupambana na rushwa kwenye chaguzi za CCM basi anzeni na Kihongosi Katibu mkuu wa UVCCM

Tafakari yetu

JF-Expert Member
Apr 19, 2021
1,502
4,408
Haya nitakayoandika hapa natamani yafike mezani kwako kupitia jukwaa hili au nitaandika kwa kirefu na kukufikishia ofisini kwako na lengo la kufanya hivi ni zuri kabisa natumaini litapokelewa kwa mikono miwili.

Awali ya yote napenda kuchukua nafasi hii kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kulijalia taifa letu amani na mshikamano na zaidi ya yote namshukuru Mungu kwa afya na uhai. Nazidi kuwaombea viongozi wangu busara na hekima katika kukiongoza chama kwa mafanikio na shukrani za kipekee ziende kwenu viongozi viongozi wetu wakuu kwa miongozo mizuri inayokusudia kukiimarisha chama.

Ndugu Makamu Mwenyekiti wa CCM, umejaliwa jicho la kiungozi na kupitia jicho hilo unarekebisha palipobomoka na kujenga upya. Kupitia jicho hilo, ulipokuwa ziarani Geita ulizungumzia athari za rushwa na kuonya wanaCCM kutochagua viongozi Wala rushwa ukasema kwamba rushwa ni Sababu ya kupatikana viongozi wasiofaa.

Baada ya kusikia maneno hayo kwa upande mmoja nikafarijika na kuona sasa zile zama za rushwa kwenye chaguzi zimefika mwisho lakini hapo hapo kwa upande mwingine nikahuzunika nilipoona bado viongozi wa UVCCM wanaweza kupatikana kwa zao la rushwa. Kwa nini?

Kenani Kihongosi ambaye kwa Sasa ni katibu Mkuu wa UVCCM ambaye kwa kanuni za uchaguzi wa UVCCM ndiye mkurugezi wa uchaguzi ndani ya UVCCM ana tuhuma nyingi za upokeaji rushwa na tuhuma hizo mpaka sasa hazijasafishwa na amebaki mtuhumiwa wa rushwa. Mtu kama huyo ambaye ana makando kando ya rushwa na ndiye mkurugenzi wa uchaguzi wa UVCCM hivi tutegemee viongozi watakaopitishwa naye wasiwe Wala rushwa? Hakika ni kujidanganya wenyewe

Sina nia mbaya na Kenani Kihongosi Katibu mkuu wangu lakini daima natanguliza maslahi ya Chama na jumuiya yangu na kwa kulitazama hili naomba suala la Kihongosi liangaliwe upya na asafishwe kabla ya kupewa kupewa jukumu la kuongoza vikao vijavyo. Tuhuma za Gambo dhidi yake bado zinahitaji majibu.

Tuna imani sana na utumishi na uongozi wako ndugu makamu Mwenyekiti tunaomba ushauri wako uchukuliwe kama mwanzo wa kuzaliwa upya kwa CCM na Jumuiya zake na bado tuna nafasi ya kurekebisha na kujenga upya.

Baada ya kusema haya naomba kuwakilisha ila bado naamini tuhuma za Rushwa dhidi ya Kenani Kihongosi Katibu mkuu wa UVCCM ni kubwa na kwa heshima ya chama Cha mapinduzi apishe pembeni ili chama kisipate doa la mwenye tuhuma za Rushwa kupitisha majina ya Wala rushwa na gharama za kuchagua Wala rushwa ni kubwa kwa chama na serikali. Anzeni na Kenani Kihongosi kuonesha mmedhamiria.
 
Kihongosi mjinga Sana. Alilikuwa anachapa watu wazima viboko makalioni hadharani lilipokuwa DC Arusha kwasababu ya ubadhirifu. Wakati huohuo yetye na mkurugenzi wa jiji walipiga hela za serikali.

Kati aliyewapiga viboko ni Ndugu yangu wa karibu Sana.

Limebaki kujaza vyoo tu Lumumba.

Life tu
 
Acheni mbwembwe nyie watu. HUWEZI KUITENGANISHA CCM NA RUSHWA halafu CCM ikaendelea kuwa hai. CCM ni RUSHWA na RUSHWA ni CCM.
Ingekuwa Enzi za Nyerere, Kwa kauli Yako, wangejitokeza viongozi kupinga na kuomba ushahidi Ili washughulikie DOA Hilo.

Lakini sasa wote wapo kimya!!!! Business as usual.
 
Hakuna mtu anaangaika na vitu ambavyo havipo, mzalendo Kenani achukue rushwa laki tatu, milioni Moja hivi ni vituko, taarifa inatolewa na Gambo. Unaujua uhusiano wa Kenan na Gambo?Kama haujui endelea Kupiga kazi.
 
Hakuna mtu anaangaika na vitu ambavyo havipo ,mzalendo Kenani achukue rushwa laki tatu, milioni Moja hivi ni vituko,taarifa inatolewa na Gambo.Unaujua uhusiano wa Kenan na Gambo?Kama haujui endelea Kupiga kazi.
Uhusiano wao ukoje kwani??
 
Hakuna mtu anaangaika na vitu ambavyo havipo ,mzalendo Kenani achukue rushwa laki tatu, milioni Moja hivi ni vituko,taarifa inatolewa na Gambo.Unaujua uhusiano wa Kenan na Gambo?Kama haujui endelea Kupiga kazi.
Kwa ivo kwa kuwa Kamati Kuu ya CCM ina waislamu wengi kuliko Wakristo, basi CCM wana Udini? Unajua wewe tofauti kati ya Kabila na ukabila ama dini na udini??
Unadhani hao wakaskazini ndani ya kamati kuu ya CHADEMA wapo kwa sifa zao? Kama unafikiri hivyo unajidanganya
 
Unadhani hao wakaskazini ndani ya kamati kuu ya CHADEMA wapo kwa sifa zao? Kama unafikiri hivyo unajidanganya
Ulitaka idadi mara mambo ya sifa. Sifa ya kuwemo si kuchaguliwa ama kuteuliwa. Sasa sifa hizo hawana? Hebu wataje hao watu wa Kaskazini tuwajue. Hivi kwenye CCM hakuna watu wa Kaskazini??

RUSHWA ni CCM na CCM ni RUSHWA.
 
Kesi ya Nyama anapelekewa Fisi ?!!!

Au tuseme Kesi ya Tembo, anapelekewa mkusanya Meno....
unayempelekea Kesi apambane na Rushwa yeye mwenyewe cheo kapewa kama hongo. Vyeo vya CCM usipokuliana na mambo ya kutoa ama kupokea rushwa huwezi kupata.
 
Ulitaka idadi mara mambo ya sifa. Sifa ya kuwemo si kuchaguliwa ama kuteuliwa. Sasa sifa hizo hawana? Hebu wataje hao watu wa Kaskazini tuwajue. Hivi kwenye CCM hakuna watu wa Kaskazini??

RUSHWA ni CCM na CCM ni RUSHWA.
Hivi yule aliyesema Sasa Sasa ni zamu ya mlutheri alisema akiwa Chama gani?
 
Back
Top Bottom