Kwako mume wa huyu dada mwenye VOLKSWAGEN POLO

Naishi Dodoma ila kwa sasa nipo Dar Ukonga KMKM ambapo nimejenga makazi yangu ya kupangisha. Kama mna kumbukumbu nzuri nilileta uzi humu majuzi nikiomba ushauri wa namna ya kudeal na mpangaji wangu mmoja mjeda aliyetaka kunidhulumu kodi na wadau mkanipa ushauri murua kabisa na j3 naenda kulipwa pesa yangu.

Nikiwa naingia KMKM recreation centre kwa miguu, getini ikanipita gari aina ya Volkswagen polo kwa kasi ikiendeshwa na binti mmoja mlimbwende. Nilivyofika ndani nikamkuta bidada analia kwa uchungu, wahudumu na wateja wengine wakawa wanamshangaa! Akaagiza chupa ya wine. Nikawa namu-observe kwa takribani nusu saa. Baadaye nikamuita dada aliyemuhudumia na kukwambia nitalipia ile chupa ya wine. Mhudumu akaenda kukwambia ila dada hakujibu chochote.

Akaonekana amenipuuza na kuendelea kunywa ile wine kwa kasi. Baada ya dk 20 hivi, nikiwa nimeinamia simu yangu yule dada akahamia mezani kwangu! Tukasalimiana, akaomba kukaa nikamruhusu, kabla hajaanza kujieleza nikamwambia asubiri, nikamsihi aendelee kulia ili uchungu umtoke moyoni.

Aliyonieleza baada ya kumaliza kulia yanaogopesha. Anadai mume wake amebadilika sana, anatembea na binti mmoja wa saluni ambayo iko jirani na nyumbani kwao. Jamaa ameaga anaenda safari ya kikazi, baada ya mwanaume kupaki begi la safari, mkewe (ambaye ndio huyu dada) akakuta pair ya viatu vya kike na iphone full boxed, mkewe alikuwa anamuwekea mumewe makoti ya baridi kwasababu jamaa aliaga anaenda Arusha, wakati mkewe anaweka hayo Makoti jamaa alikuwa ametoka.

Jamaa alivyorudi mke akanyamaza. Jamaa akaondoka leo asubuhi mkewe anamuangalia tu. Sasa mchana huu huyu dada akiwa na mawazo saluni akakutana na shosti yake, shosti mtu bila kujua, akamwambia huyu dada kwamba kakutana na mume wa huyu dada Mlimani City akajaribu kumsalimia lakini shemeji mtu hakumuona wala kumsikia. Mke mtu akatoka nje ya saluni akampigia mumewe akajifanya yeye ndio kamuona, mwanaume akaanza kujikanyaga! Akazima na simu (inaelekea anajipanga kudanganya zaidi).

Kumbe baadhi ya wanawake wa pale saluni wanajua jamaa anatoka na hako kabinti ka saluni na kabinti hakakuwepo leo!!! Wafanyakazi wenzake pale saluni wakasema walikuwa wanashindwa kumwambia wakihofia kuonekana wafitini! Mke kaunganisha dots kagundua kwamba ndio maana jamaa alikuwa na pair ya viatu na simu mpya!!!

Mkuu, umeharibu huku. Kama upo JF kakiri tu kwa mkeo wala usiendelee kudanganya.

Dada kalewa sana hapa, ingekuwa enzi zangu kabla sijaokoka leo pangechimbika.

Kanipa funguo za gari na handbag yake. Sijui anapoishi ila anasema akilewa sana nimtafute bodaboda anaitwa ......hapa nje ya KMKM atanielekeza kwake.

Sisi wanaume sijui tumerogwa na nani. Mwanamke mzuri hivi, msomi, mchapakazi, halafu anasalitiwa kindezi namna hii

NGOJA iendelee kunyesha tuone panapovuja ..
Wenetu mnapotaka kuchepuka nendeni mbali sana, Kuchepuka na mwanamke wa mtaani ni kuwashushia heshima sana wake zetu.
 
Huyo binti atakuja kufa bure sababu ya binadamu mwenzake. Akifa wengine wanaendelea na maisha. Kwenye hii dunia, kitakachonifanya niumie sana ni kuugua ugonjwa kama kansa ambao hauponi, au kukosa hela hata ya kula. Mengine wala hayawezi kuniumiza kiasi cha kuharibu maisha yangu. Ukikutana naye tena umshauri asiamini binadamu yoyote kwenye dunia hii na maisha yake tana thamani kuliko kitu chochote hapa duniani.
Umezungumza kwa hisia kali sana mkuu. Kweli utu uzima dawa.
 
Utalia, utakunywa mipombe utaharibu maini yako na Figo bure uanze gharama chungu mbovu za kujitibia. Ameshachepuka , kulia kwake na kunywa pombe hakusaidii kitu wala kubadilisha kitu. Kama ana ubavu amuache huyu jamaa kama hana , arudi tu home maisha mengine yaendelee.
 
Wisdom
 
Naishi Dodoma ila kwa sasa nipo Dar Ukonga KMKM ambapo nimejenga makazi yangu ya kupangisha. Kama mna kumbukumbu nzuri nilileta uzi humu majuzi nikiomba ushauri wa namna ya kudeal na mpangaji wangu mmoja mjeda aliyetaka kunidhulumu kodi na wadau mkanipa ushauri murua kabisa na j3 naenda kulipwa pesa yangu.

Nikiwa naingia KMKM recreation centre kwa miguu, getini ikanipita gari aina ya Volkswagen polo kwa kasi ikiendeshwa na binti mmoja mlimbwende. Nilivyofika ndani nikamkuta bidada analia kwa uchungu, wahudumu na wateja wengine wakawa wanamshangaa! Akaagiza chupa ya wine. Nikawa namu-observe kwa takribani nusu saa. Baadaye nikamuita dada aliyemuhudumia na kukwambia nitalipia ile chupa ya wine. Mhudumu akaenda kukwambia ila dada hakujibu chochote.

Akaonekana amenipuuza na kuendelea kunywa ile wine kwa kasi. Baada ya dk 20 hivi, nikiwa nimeinamia simu yangu yule dada akahamia mezani kwangu! Tukasalimiana, akaomba kukaa nikamruhusu, kabla hajaanza kujieleza nikamwambia asubiri, nikamsihi aendelee kulia ili uchungu umtoke moyoni.

Aliyonieleza baada ya kumaliza kulia yanaogopesha. Anadai mume wake amebadilika sana, anatembea na binti mmoja wa saluni ambayo iko jirani na nyumbani kwao. Jamaa ameaga anaenda safari ya kikazi, baada ya mwanaume kupaki begi la safari, mkewe (ambaye ndio huyu dada) akakuta pair ya viatu vya kike na iphone full boxed, mkewe alikuwa anamuwekea mumewe makoti ya baridi kwasababu jamaa aliaga anaenda Arusha, wakati mkewe anaweka hayo Makoti jamaa alikuwa ametoka.

Jamaa alivyorudi mke akanyamaza. Jamaa akaondoka leo asubuhi mkewe anamuangalia tu. Sasa mchana huu huyu dada akiwa na mawazo saluni akakutana na shosti yake, shosti mtu bila kujua, akamwambia huyu dada kwamba kakutana na mume wa huyu dada Mlimani City akajaribu kumsalimia lakini shemeji mtu hakumuona wala kumsikia. Mke mtu akatoka nje ya saluni akampigia mumewe akajifanya yeye ndio kamuona, mwanaume akaanza kujikanyaga! Akazima na simu (inaelekea anajipanga kudanganya zaidi).

Kumbe baadhi ya wanawake wa pale saluni wanajua jamaa anatoka na hako kabinti ka saluni na kabinti hakakuwepo leo!!! Wafanyakazi wenzake pale saluni wakasema walikuwa wanashindwa kumwambia wakihofia kuonekana wafitini! Mke kaunganisha dots kagundua kwamba ndio maana jamaa alikuwa na pair ya viatu na simu mpya!!!

Mkuu, umeharibu huku. Kama upo JF kakiri tu kwa mkeo wala usiendelee kudanganya.

Dada kalewa sana hapa, ingekuwa enzi zangu kabla sijaokoka leo pangechimbika.

Kanipa funguo za gari na handbag yake. Sijui anapoishi ila anasema akilewa sana nimtafute bodaboda anaitwa ......hapa nje ya KMKM atanielekeza kwake.

Sisi wanaume sijui tumerogwa na nani. Mwanamke mzuri hivi, msomi, mchapakazi, halafu anasalitiwa kindezi namna hii

NGOJA iendelee kunyesha tuone panapovuja ..
Ingekuwa enzi zako kabla haujaokoka hahahahah
 
Somo la ndoa ni gumu sana.Ndio maana unapewa cheti kwanza halafu ndiyo uende kusoma na mitihani inafuata.
 
Back
Top Bottom