Kwako Mtangazaji wa Kike Star TV:Je, Hayo Maneno uyapendayo Umechanjiwa? Tafuta Mengine!

SHIEKA

JF-Expert Member
Dec 20, 2011
8,244
4,258
Anaitwa Sauda Mwilima na anaendesha kipindi cha Bongo Beats. Kila atangazapo lazima atumie maneno haya, hata tarehe 21/9/2013 alipotangaza Red Carpet ya Redd's Miss Tanzania aling'ang'ania hayo maneno yake ya kuchosha yasiyo na ladha! Utamsikia:
..... ili mradi basi........kwa njia moja au nyingine...........mwisho wa siku..........kuweza........
Dada, kila nikikusikiliza nachoka sana. Kwa nini hutumii ubunifu wa lugha ili uje na misemo tofauti ya kuburudisha? Kila siku ili mradi basi...... mwisho wa siku....
Badilika bwana!

Nakutakia kila la kheri dadaangu!
 
Kwel ndugu kwani lugha ina mawanda mapana mmo kama ukijua kuitumia
Kabisa ndugu yangu. Yaani angeogelea kwenye bahari ya kiswahili kama alivokuwa akifanya Ben Kiko, kipindi cha huyu dada kingenoga sana kuliko ilivyo hivi sasa na mineno yake ya kiuvivu!
 
hiyo ni chuki binafsi...kila binadamu ana maneno yake ya kuongea yaliyo karibu ndo maana haa shule kila mwalimu hpewa jina kulingana na maneno yake anayozoea kuyatumia
 
hiyo ni chuki binafsi...kila binadamu ana maneno yake ya kuongea yaliyo karibu ndo maana haa shule kila mwalimu hpewa jina kulingana na maneno yake anayozoea kuyatumia
Chuki binafsi? Hii thread haihusiani na taarab ndugu! Mtangazaji anayejijua, anachunga sana lugha anayotunia. Msikilize mathlani Salim Kikeke wa BBC. Anajaribu sana kutumia lugha inayovutia, na hang'ang'anii baadhi ya maneno kwa kuyatumia tena na tena.
Usilinganishe waalimu na watangazaji.Kwanza huyu mtangazaji wa star tv ninayemzungumzia yupo kwenye tasnia ya starehe. Lugha yake yapaswa kustarehesha pia sio hiyo michosho yake ya kila siku!
 
hiyo ni chuki binafsi...kila binadamu ana maneno yake ya kuongea yaliyo karibu ndo maana haa shule kila mwalimu hpewa jina kulingana na maneno yake anayozoea kuyatumia
Unakosea kaka kumrekebisha mtu ni kumsaidia awe bora zaidi ya awali!!
Kuna mifano ya watangazaji wengi ambao wanajitahidi kutumia lugha vutivu mfano Marina Hassan wa TBC one!!
Au kajaribu kutupia jicho watangazaji wa CITIZEN TV utapenda jinsi watumiavyo lugha yetu pendwa..
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom