Kwaheri UKAWA Kwaheri UKUTA

Izack Mwanahapa

JF-Expert Member
Apr 21, 2011
497
236
U WAPI UKAWA ULIOTUMAINIWA NA WENGI ?

Watu wataendelea kufeli tu na kufanya siasa za mitandaoni kwasababu ya kuhubiri wasiyoyatenda.

Ni hivi majuzi tu kutokana na ukweli wa dhana kwamba "Umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu" baadhi ya vyama vya upinzani viliunda umoja wao wakauita "UKAWA" lengo likiwa ni kuviunganisha vyama ili nguvu iwe kubwa kwa sababu ya ushiriki wa viongozi na wanachama kutoka vyama mbalimbali.

Ni UKAWA walioshirikiana katika uchaguzi mkuu mpaka kufikia hatua ya baadhi ya watu kuvihama vyama vyao vya awali na kujiunga na vyama vingine ndani ya UKAWA ili kutimiza matakwa fulani fulani ya kisheria.

Wakati ukawa ukiwa hai (maana hakuna tamko linalosema kwamba umekufa) kinaibuka chama kimoja toka ndani ya UKAWA na kuja na movement ya "UKUTA" movement yenye lengo zuri la kupigania demokrasia nchini lakini tayari watu wameshasahau kwamba umoja ni nguvu kwasababu suala la kuminywa kwa demokrasia si Suala la chama kimoja na safari hii hakukuwa na haja ya kuanzisha umoja Mpya bali UKAWA ule ule ungeweza kutumika kufanya movement hii kubwa kitaifa.

Sijaelewa ni jambo gani liliwaunganisha kwenye Mjadala wa katiba mpya na Uchaguzi mkuu na sasa ni jambo gani linawatenganisha kwenye UKUTA.

Ni dhahir kwamba movement hii mafanikio yake yatakuwa hafifu hata Polisi wakiamua kulala nyumbani kwasababu umoja na spirit iliyojengwa kwa watu Mwanzo kupitia ukawa imeshapotea sasa kuwabadilisha wananchi kutoka kwenye imani ya "umoja ni nguvu" ni kazi kubwa ni mpaka watakapoeleweshwa ni kwanini jambo hili la kupigania demokrasia lifanywe na chama kimoja tu ilhali linaadhari kwa vyama vyote na UKAWA haujafa au chama hicho kitangaze kwamba kimejitoa kwenye UKAWA au wasema ni kwa vipi chama hicho kimoja kinaathirika zaidi na kuminywa kwa demokrasia kuliko vyama vingine?

Mambo yakienda vibaya tarehe 1 basi mjue #KWAHERIUKAWAKWAHERIUKUTA

Mwanahapa.
 
Back
Top Bottom