Kwa yaliyomkuta Nape Nnauye na Mwita Waitara, je nini nafasi ya vijana ndani ya CCM?

Zakumi,
Mkuu sijazunguka na ndio maana hukunielewa kabisa...
China na Marekani pamoja na kwamba zote zina mifumo tofauti ya kiuchumi lakini viongozi wake wote wapo ku serve the nation. Wanataka maendeleo ya nchi yao.. adui wa Maendeleo yao yuko nje, wakati Tanzania Viongozi wetu wanataka kuboresha maisha yao wenyewe...Hivyo adui wetu yuko ndani..Yes wanachukua 10% lakini hiyo 90 unayozungumzia itabaki nchini? au hukumsoma Nnauye!..
China na Marekani 90 inabakia ndani na kuzungusha - Tanzania hiyo 90 inakwenda nje!.
Na sio kweli kwamba hawafahamu kinachotokea nchi za China na Marekani isipokuwa tatizo ni
 
Swali la kwanini nilizungumza swala la Mradi UVCCM wakati nachukua fomu limekuwa likiulizwa sana, hasa kwanini wakati huu. Ikumbukwe mimi ni mjumbe wa Baraza Kuu UVCCM(T) toka mwaka 2002, Mradi wa UVCCM ni moja ya mipango ya kazi za UVCCM kwa kipindi cha 2003/2008,kwahiyo nimekuwepo kwenye mchakato wa hili na sina tatizo na uwekezaji wa mradi huu TATIZO NI TARATIBU ZA KUFIKIA UWEKEZAJI HUU NAAMINI HAZIKUFUATWA, MBILI MKATABA HAUNA MASLAHI KWA UVCCM, CCM NA VIJANA WA CCM NA WAKITANZANIA.
Sikuanzia pale nilipochukua fomu kuupinga mkataba huu, bali nimeanza siku nyingi vikaoni sio publicly. Wakati huo nilikuwa masomoni India kila nilipokuwa nikija likizo na kuhudhuria vikao vinavyonihusu nimekuwa nikipinga Utaratibu uliotumika kumpata mwekezaji na contents za mkataba, narudia ndani ya vikao, na si kupinga tu bali kuhamasisha bila kificho wala unafiki wengine kupinga pia, nikiamini TUNAPASWA KUWA WAZALENDO ZAIDI KWA KUWEKEZA NA MASHIRIKA YETU YA UMMA KAMA NSSF,PPF NK ILI PESA WAKIPATA ZIBAKI KUJENGA NCHI YETU PIA KULIKO WAGENI WAPATAPO FAIDA HUPELEKA KWAO.
Nasikitika, baadae wakubwa wachache wakaamua kuvizunguka vikao na kuamua kusign mkataba tulioukataa baraza kuu la UVCCM na kuagiza marekebisho.
Niliwaonya mara kwa mara hawakutaka kusikiliza kwa kulewa na tu madaraka, nilipochukua fomu haikuwa mara ya kwanza kwa hili kusemwa hadharani, lilisha wahi kuandikwa na KULIKONI GAZETI, tofauti tu hapa nilitoa wanaohusika na dhuluma hii kwa UVCCM,CCM NA NCHI YETU.
NA IKUMBUKWE HAPA NDO NILIKUWA NIMERUDI TOKA INDIA MASOMONI KAMA WIKI MBILI TU, NIKAKUTA WAKUBWA WANAENDELEA NA MRADI NINAOAMINI NI WA HOVYO, NI UKWELI USIO NA MASHAKA BILA KELELE ZILE MKATABA USINGEPITIWA UPYA........sijui kama nimekidhi mahitaji yenu...

Nape karibu sana hapa, tena umeamua kujitambulisha kweupee kama akina Zitto na Dr. Slaa. Ni wachache sana hata mimi sidhubutu. Hongera sana kaka.

Lakini bado sikuungi mkono mana ishu hii nyi punje katika matatizo lukuki ambayo ningependa uyazungumzie. CCM haina dira tekelezi ya kuendeleza nchi zaidi ya ufisadi. Sema yote bwana kama uliona digrii ya Tz haikufai mpaka ukaenda India. Uliotoka nayo india njoo uyakosoe yote. Mradi wa jengo is nothing brother.... Nina hasira....
 
Kijana kutetea maslahi ya nchi ndani ya CCM ni sawa na kujichimbia kaburi; inahitaji moyo wa uzalendo sana, na watu kama akina Bwana Nnauye na Bwana Waitara wanastahili hesima na kulindwa na umma. Historia ya nchi yetu kwa wanasiasa vijana ndani ya CCM imekuwa siyo nzuri hasa pale wanaposhindana na ukiritimba ulioko ndani ya chama chao kwa msalahi ya nchi.
 
Swali la kwanini nilizungumza swala la Mradi UVCCM wakati nachukua fomu limekuwa likiulizwa sana, hasa kwanini wakati huu. Ikumbukwe mimi ni mjumbe wa Baraza Kuu UVCCM(T) toka mwaka 2002, Mradi wa UVCCM ni moja ya mipango ya kazi za UVCCM kwa kipindi cha 2003/2008,kwahiyo nimekuwepo kwenye mchakato wa hili na sina tatizo na uwekezaji wa mradi huu TATIZO NI TARATIBU ZA KUFIKIA UWEKEZAJI HUU NAAMINI HAZIKUFUATWA, MBILI MKATABA HAUNA MASLAHI KWA UVCCM, CCM NA VIJANA WA CCM NA WAKITANZANIA.
Sikuanzia pale nilipochukua fomu kuupinga mkataba huu, bali nimeanza siku nyingi vikaoni sio publicly. Wakati huo nilikuwa masomoni India kila nilipokuwa nikija likizo na kuhudhuria vikao vinavyonihusu nimekuwa nikipinga Utaratibu uliotumika kumpata mwekezaji na contents za mkataba, narudia ndani ya vikao, na si kupinga tu bali kuhamasisha bila kificho wala unafiki wengine kupinga pia, nikiamini TUNAPASWA KUWA WAZALENDO ZAIDI KWA KUWEKEZA NA MASHIRIKA YETU YA UMMA KAMA NSSF,PPF NK ILI PESA WAKIPATA ZIBAKI KUJENGA NCHI YETU PIA KULIKO WAGENI WAPATAPO FAIDA HUPELEKA KWAO.
Nasikitika, baadae wakubwa wachache wakaamua kuvizunguka vikao na kuamua kusign mkataba tulioukataa baraza kuu la UVCCM na kuagiza marekebisho.
Niliwaonya mara kwa mara hawakutaka kusikiliza kwa kulewa na tu madaraka, nilipochukua fomu haikuwa mara ya kwanza kwa hili kusemwa hadharani, lilisha wahi kuandikwa na KULIKONI GAZETI, tofauti tu hapa nilitoa wanaohusika na dhuluma hii kwa UVCCM,CCM NA NCHI YETU.
NA IKUMBUKWE HAPA NDO NILIKUWA NIMERUDI TOKA INDIA MASOMONI KAMA WIKI MBILI TU, NIKAKUTA WAKUBWA WANAENDELEA NA MRADI NINAOAMINI NI WA HOVYO, NI UKWELI USIO NA MASHAKA BILA KELELE ZILE MKATABA USINGEPITIWA UPYA........sijui kama nimekidhi mahitaji yenu...

Nnauye Jr:

Kwanza nakupa pongezi kwa ujasiri wako. Lakini vilevile lazima tuambiane ukweli.

Pamoja na juhudi zako za kutaka kuleta mabadiliko kuna vitu vichache vijana mlioingia kwenye siasa hamvifahamu. Kitu cha kwanza mafanikio yanatokana na role definitions.

Role ya chama cha kisiasa na jumuia za kisiasa za vyama hivyo zibakie kwenye siasa. Na kama kuna gharama za uendeshaji basi ni wajibu wa wanachama wa vyama hivyo kuingia gharama katika za michango.

Miradi ya uwezekaji inayoendeshwa na vyama vya siasa na jumuia zake haifanyi vyama au jumuia kufikisha malengo yake ya kisiasa. Kwa maneno mengine CORE VALUES ya UVCCM ni siasa. Na kama mnataka kufanya biashara basi kuweni full time business entities Kama vile ippmedia, mohamedi enterprises etc.

Kama kuna uwezekano naomba UVCCM warudisha mali za taifa, kwa sababu tulilazimishwa kuchangia umoja huo wakati wa mfumo wa chama kimoja. Na baadaye UVCCM ijiendeshe kama political entity ndani ya sisiemu na tuone kama migogoro ya kiuchumi na wawekezaji kama itatokea.
 
Kijana kutetea maslahi ya nchi ndani ya CCM ni sawa na kujichimbia kaburi; inahitaji moyo wa uzalendo sana, na watu kama akina Bwana Nnauye na Bwana Waitara wanastahili hesima na kulindwa na umma. Historia ya nchi yetu kwa wanasiasa vijana ndani ya CCM imekuwa siyo nzuri hasa pale wanaposhindana na ukiritimba ulioko ndani ya chama chao kwa msalahi ya nchi.

Afadhali kidogo na Waitara amefanya kazi na imeonekana. Aliongeza kura kadhaa kwa CHADEMA ijapokuwa kuchagua chadema sio kujenga nchi ila ametia chachu.

Kichuguu; Nape amefanya nini? kwa nini alisema hadharani wkt wa kuchukua form? si angetutumia kwa JF kabla au si angempa FMES. Hawajuani? maslahi ya taifa yapi? Kama ni jengo basi apiganie majengo yote ya CCM na viwanja virudi serikalini hapo ndo ntaelewa. Marehemu Wangwe alipigania ruzuku iende wilayani ina maana alipigania kodi? au maslahi ya chadema? Vipi bwana, huyu Nape kama umeamua kutetea maslahi, tumia elimu yako useme yote nasi tutakufuata. Nchimbi na timu yake unaijua vzr kuliko mimi. SEMA YOTE TUJUE DIRA YAKO. TUKUFUATE AU TUKUPIGE CHINI...
 
Zakumi,
Mkuu sijazunguka na ndio maana hukunielewa kabisa...
China na Marekani pamoja na kwamba zote zina mifumo tofauti ya kiuchumi lakini viongozi wake wote wapo ku serve the nation. Wanataka maendeleo ya nchi yao.. adui wa Maendeleo yao yuko nje, wakati Tanzania Viongozi wetu wanataka kuboresha maisha yao wenyewe...Hivyo adui wetu yuko ndani..Yes wanachukua 10% lakini hiyo 90 unayozungumzia itabaki nchini? au hukumsoma Nnauye!..
China na Marekani 90 inabakia ndani na kuzungusha - Tanzania hiyo 90 inakwenda nje!.
Na sio kweli kwamba hawafahamu kinachotokea nchi za China na Marekani isipokuwa tatizo ni

lol:

Nimemsoma Nnauye lakini na yeye anachemsha kubaki CCM. Kama hachemshi, atueleze kuwa hizo mali walizonazo UVCCM walianzia wapi kama sio kwa kuwachangisha watanzania kwa nguvu kabla ya mfumo wa vyama vingi?

UVCCM wana-behave kama watoto wanaogombania urithi ambao hawakuufanyia kazi.

Warudishe mali kwa taifa na wao waanze kama vijana wa Chadema au CUF. Wakianza upya kama vijana wa Chadema au CUF, ni hapo ndipo tutaona viongozi wa kweli wa kisiasa kwa sababu they have to make things from nothing.

ASP na TANU ni vya vilivyokuwa vya kisiasa bila kuwa na investment yoyote zaidi ya michango ya wanachama na mafanikio yao yalikuwa makubwa. CCM, UVCCM, UWT acheni umachinga na fanyeni siasa na mtalisaidia taifa.
 
Jamani kwani nini kilitokea kwa Mwita Mwikwabe. Huyu ni jamaa yangu wa zamani sana, nilikuwa nae kwenye shule za public, kisha yeye akaanza mlimani mimi nikasema thanks but no thanks nikatafuta maisha kwingine.

Mwita alikuwa leader since shule, siku zote nafurahia utashi wake. I think alifanya makosa kujoin CCM at the beggining.

Mimi binafsi nimesha challenge vijana wengi wanaowaza kufungua Matawi ya CCM hapa USA. Swali langu kubwa kwao ni why CCM? Kusema kweli wote huwa hawana majibu.

CCM ni sawa na Mafia, you need super connection ili uwe mstari wa mbele.
Thanks but no thanks to CCM
 
Swali la kwanini nilizungumza swala la Mradi UVCCM wakati nachukua fomu limekuwa likiulizwa sana, hasa kwanini wakati huu. Ikumbukwe mimi ni mjumbe wa Baraza Kuu UVCCM(T) toka mwaka 2002, Mradi wa UVCCM ni moja ya mipango ya kazi za UVCCM kwa kipindi cha 2003/2008,kwahiyo nimekuwepo kwenye mchakato wa hili na sina tatizo na uwekezaji wa mradi huu TATIZO NI TARATIBU ZA KUFIKIA UWEKEZAJI HUU NAAMINI HAZIKUFUATWA, MBILI MKATABA HAUNA MASLAHI KWA UVCCM, CCM NA VIJANA WA CCM NA WAKITANZANIA.
Sikuanzia pale nilipochukua fomu kuupinga mkataba huu, bali nimeanza siku nyingi vikaoni sio publicly. Wakati huo nilikuwa masomoni India kila nilipokuwa nikija likizo na kuhudhuria vikao vinavyonihusu nimekuwa nikipinga Utaratibu uliotumika kumpata mwekezaji na contents za mkataba, narudia ndani ya vikao, na si kupinga tu bali kuhamasisha bila kificho wala unafiki wengine kupinga pia, nikiamini TUNAPASWA KUWA WAZALENDO ZAIDI KWA KUWEKEZA NA MASHIRIKA YETU YA UMMA KAMA NSSF,PPF NK ILI PESA WAKIPATA ZIBAKI KUJENGA NCHI YETU PIA KULIKO WAGENI WAPATAPO FAIDA HUPELEKA KWAO.
Nasikitika, baadae wakubwa wachache wakaamua kuvizunguka vikao na kuamua kusign mkataba tulioukataa baraza kuu la UVCCM na kuagiza marekebisho.
Niliwaonya mara kwa mara hawakutaka kusikiliza kwa kulewa na tu madaraka, nilipochukua fomu haikuwa mara ya kwanza kwa hili kusemwa hadharani, lilisha wahi kuandikwa na KULIKONI GAZETI, tofauti tu hapa nilitoa wanaohusika na dhuluma hii kwa UVCCM,CCM NA NCHI YETU.
NA IKUMBUKWE HAPA NDO NILIKUWA NIMERUDI TOKA INDIA MASOMONI KAMA WIKI MBILI TU, NIKAKUTA WAKUBWA WANAENDELEA NA MRADI NINAOAMINI NI WA HOVYO, NI UKWELI USIO NA MASHAKA BILA KELELE ZILE MKATABA USINGEPITIWA UPYA........sijui kama nimekidhi mahitaji yenu...

Kwanza naomba nikupongeze kwa kujiunga na forum ya kweli. Ni wazi ya kwamba wana CCM wengi sana wanaona JF ni kama gang of killers.

Nikweli hatua uliyochukua kuchallenge maamuzi ya CCM ni kubwa sana. Majority ya vijana wa kitanzania wanaangalia sana maslai binafsi pindi inapofika kwenye maamuzi mambo ya kichama.

CCM is like poison. sorry kwa language yangu, but it is there to kill people who are against with their ideologies. Hii imekuwa hivyo since TANU, and i don't see any changes kwa muda huu. I think you take a good move, eventhough you put you life on the sleeve.

God will award you for that.
 
Nape chukua hatua, vaa ujasiri. Unaweza kutumika vizuri zaidi kwingineko kuliko huko CCM. Ningekuelewa enzi za chama kimoja ambapo hapakuwa na alternative, lakini leo hii, hapana. I know you, you're bigger and bolder than CCM. Nakwambia hao jamaa zako CCM watakuzesha na kukupa magonjwa ya moyo bila sababu za msingi. You will never change them, they will only change you!Take a step comrade, join the dream team that wants to change the country for the better. You will never regret!
 
Zakumi,
Ndio maana nimehoji kuwepo kwake CCM akifikiria kwamba unaweza kuleta mabadiliko ndani ya CCM...
Nijuavyo mimi mapambano yoyote dhidi ya Udhalimu ni lazima uwe nje ya udhalimu huo lakini ukiwa part ya udhalimu na kufikiria kwamba wewe unaweza kuwa Mtume, binafsi naamini wakati huo umekwisha. Sana sana U become part ya hao wadhalimu ama utatemwa.
Kwa vijana wote wa JF ambao ni wanachama wa CCM kina Field marshall ES, nakuombeni fikirieni upya...
Nitarudia kusema, ni vigumu sana kuweza kuleta mapinduzi ya kweli ukiwa ndani ya CCM, nasema hivi nikifikiria kuwa hivi kweli wazazi wetu waliopigania Uhuru wangeweza kuleta Mabadiliko wakiwa wanachama na wapambe wa Mkoloni?..Sina maana kuwa CCM ni mkoloni, ila Uongozi wajuu DOLA umeshikwa na Monarch fulani...
 
Magabe, et al.,

Niliwahi kuandika article ikielezea, pamoja na mambo mengine, kwa nini vijana kama Nape wanaendelea kubaki CCM. Hebu jaribu kuisoma hapa chini uone kama inajibu baadhi ya hoja zako.
_________________________________________________________________

CCM ya Nape ni nadharia, ya Nchimbi ndiyo iliyopo

na
Kitila A. K. Mkumbo (Tanzania Daima, 24 Septemba 2008)

NIMEFUATILIA, kama ilivyo kwa Watanzania wengine, ‘mgogoro’ wa kifikra na mtazamo kati ya aliyekuwa mgombea wa nafasi ya uenyekiti katika Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Nape Nnauye na mwenyekiti anayemaliza muda wake katika umoja huo, Emmanuel Nchimbi.

Hata hivyo nikiri mapema kabisa kuwa sielewi mantiki ya mgogoro huu na hatimaye mjadala uliofuata na unaoendelea.

Nisichoelewa hasa ni msingi wa dhamira ya Nape katika hoja yake ya kupinga mkataba wa mradi wa ujenzi wa jengo la makao makuu ya UVCCM, ambayo imevuta hisia za watu wengi, ndani na nje ya CCM.

Najiuliza maswali mawili. Mosi, je, Nape ameibua hoja ya kupinga mkataba ‘haramu’ wa mradi wa ujenzi wa jengo la UVCCM kama karata na turufu ya kumwezesha kushinda kiti cha uenyekiti wa umoja huo?

Pili, ni kweli kwamba Nape ni miongoni mwa wana CCM wachache ‘waliokoka’ na kujiunga na kundi kubwa la wananchi wanaochukizwa na kukerwa na mwenendo wa ufisadi miongoni mwa viongozi waandamizi wa CCM na serikali yake?

Kama msingi wa hoja ya Nape ni ule wa kwanza, wa kutumia hoja yake kama turufu ya kuvuta hisia za wana UVCCM wenzake ili wamchague kuwa mwenyekiti wao, ni wazi kuwa amekwishashindwa kabla hajaanza.

Kwa msingi huu, anachojaribu kufanya Nape ni kuvunja misingi mama ya kanuni za ushindani ndani ya CCM.

Nape anataka achaguliwe kwa misingi ya hoja za kimantiki, uadilifu, ustaraabu, ukweli, uwazi, uhuru na kujitegemea katika kufikiri, zaidi ya yote, kutanguliza utaifa dhidi ya uchama na ukada.

Yote hii ni misingi mizuri, lakini si misingi ya CCM na ndipo upofu wa Nape ulipo. Kwa hoja zake, Nape anajaribu kuweka mlo safi katikati ya jalala la taka.

Hautanoga na wala hataufaidi mlo huo, zaidi ya yote anajiweka katika mazingira hatari ya kuambukizwa vijidudu hatari vitakavyompelekea augue ugonjwa hatari wa matumbo!

Anachofanya Nape ni kupingana na misingi ya kanuni za msingi za kutafuta madaraka ndani ya CCM, ambazo kwa uchache kabisa ni pamoja na ubabaishaji, uzandiki, ujanjaujanja, njia za mkato, unafiki, ghiliba, kujipendekeza, kuiba wajumbe na kuwaficha.

Muhimu zaidi kuliko zote, kutanguliza ukada na uchama dhidi ya uwezo wa kiuongozi na kiutendaji na uzalendo kwa nchi. Hii ndiyo CCM ambayo Nape anajaribu kuibomoa na ambayo Nchimbi na wenzake kina Makamba wanaipigania.

Kwa hiyo utaona kwamba CCM ambayo Nape anajaribu kuipigania haipo, ni nadharia. Iliyopo ni ile CCM ambayo Nchimbi na Makamba wanajaribu kuilinda kwa mafanikio makubwa.

Niliwahi kuwa mwanachama na kada mwaminifu wa CCM kwa muda kidogo na nilijaribu kugombea nyadhifa kadhaa katika UVCCM, kwa bahati nzuri nilishindwa zote!

Kwa uzoefu nilioupata ni kwamba hushindi uchaguzi ndani ya CCM kwa kuwa na uwezo au kwa kujenga hoja za kimantiki zinazoweka maslahi ya nchi mbele.

Unashinda uchaguzi ndani ya CCM kwa kujifanya wewe ni kada kuliko mwingine yeyote, kwa ujanja ujanja, kwa kujipendekeza na kujipitishapitisha kwa baadhi ya wakubwa wanaoingia kwenye vikao muhimu vya CCM kurubuni wajumbe wa vikao, ikiwemo kuwaficha wajumbe wa vikao hivyo.

Ukitaka kushindwa kirahisi katika uchaguzi wa CCM, uonyeshe uwezo na utangulize mambo ya taifa mbele badala ya ukada. Kama kuna kiongozi wa CCM aliyeshinda uchaguzi ndani ya chama hicho kwa kujenga hoja za kutetea masilahi ya taifa dhidi ya ukada awe wa kwanza kujibu makala hii.

Nape, wana CCM wengine makini wanajua vizuri kwamba ingekuwa ni suala la uwezo na kutanguliza masilahi ya taifa, Rais Jakaya Kikwete asingewashinda Salim Ahmed Salim, Mark Mwandosya na hata Frederick Sumaye.

Pamoja na mambo mengine, sifa kubwa iliyomfanya Rais Kikwete awashinde wenzake katika kinyang’anyiro cha kugombea urais ni ukada wake wa muda mrefu katika CCM.

Kwa hiyo katika CCM ukada ndiyo sifa mama na kigezo muhimu cha kuweza kuchaguliwa. Ndiyo kusema Nape anapojaribu kutanguliza utaifa, tena kwa kuzomea ufisadi, ambayo ni nguzo muhimu ya kuwepo kwa CCM, kama turufu ya kutaka achaguliwe kuwa mwenyekiti wa UVCCM, anajaribu kukata mbuyu kwa wembe. Hataweza, atajikata mwenyewe na kuuacha mbuyu umesimama kidete.

Pengine tumpe Nape, ile Waingereza wanaita: “The benefit of doubt”. Kwamba Nape ni miongoni mwa wana CCM wachache waliookoka hivi karibuni, ameamua kujitoa mwili na roho katika kujiunga na majemadari wa vita dhidi ya ufisadi.

Kuokoka kupo si tu katika siasa na dini, lakini pia katika nyanja nyingine za maisha ya kijamii. Lakini unapoamua kuokoka lazima ujue na uzingatie misingi ya wokovu, vinginevyo utaanguka tena.

Kuokoka kisiasa na kidini kunahitaji ujasiri wa kukubali kusutwa na kuacha mazoea. Ili ukamilishe wokovu lazima ukubali kubadilika kimwili na kiroho.

Ninachokiona hapa ni kwamba Nape amekwisha kutoka CCM kiroho, kiakili na kisaikolojia lakini bado amebaki kimwili. Hili ni tatizo linalowakumba wana CCM wengi.

Ninaamini kuna wana CCM wengi waliokwisha kukihama chama chao kiroho, kiakili na kisaikolojia, lakini wameendelea kubaki huko kimwili kwa kukosa ujasiri au kwa sababu zingine, ikiwemo kuamini kwamba ipo siku CCM itabadilika.

Nikiri kuwa mimi ni mmojawapo, ambaye ilinichukua takriban miaka mitano kuhama CCM kimwili. Nilikuwa nimeachana na CCM kiroho, kiakili na kisaikolojia tangu mwaka 2000, lakini ilinichukua miaka mitano hadi 2005 nilipoamua kujitoa hadi mwili na kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Binafsi nilijitoa CCM baada ya kujiridhisha bila shaka kuwa CCM imefikia hatua ya usugu, na haiwezekani kubadilika. Ni hatua ambayo vyama dada kama KANU, ZANU-PF na UNIP vilipitia na ambayo ni wananchi pekee wenye uwezo wa kuibadilisha.

Kama kweli tumechoshwa na madhira ya CCM, ikiwemo ufisadi, inabidi tufike mahala tukubali kuachana na CCM. Kuendelea kuibakisha CCM madarakani ni kukubaliana kwamba, pamoja na kwamba tumeumia kama nchi, bado tunaweza kuendelea kuwavumilia CCM, hatujaumia vya kutosha.

Kufikiri kwamba CCM inaweza kubadilika ni njia nzuri ya kujiridhisha kisaikolojia baada ya kushindwa kuitoa madarakani, lakini haisaidii kubadili hali ya mambo katika nchi yetu.

Kwa hiyo, Nape ana mambo mawili ya kuchagua. Mosi, anaweza akaendelea kubaki CCM kimwili na kuisaliti dhamira yake ya ndani na akaendelea kupiga kelele za ufisadi, ambazo zitazidi kumtenga na wenzake ambao ‘hawajaokoka’ katika CCM, na hivyo kuendelea kuonekana kituko! Pili, anaweza akauvaa ujasiri kwa kuamua kuutoa mwili wake kutoka CCM na kuupeleka kule ambapo akili na roho zipo. Uamuzi ni wake.

Inapatikana pia hapa: CCM ya Nape ni nadharia, ya Nchimbi ndiyo iliyopo

Kaka Kitila,

Asante sana kwa kuitundika hii hapa jamii forum. Nilipokuwa naanzisha hii thread niliweka pia hii makala kwenye mawazo yangu huku pia nikikumbuka uamuzi wako wa kutoka CCM na kuhamia upinzani.

Nadhani kuna challenge kubwa sana vijana wengi tunakutana nayo leo hii. Mimi binafsi CCM walikataa ombi langu la kujiunga nao (sort of) pamoja na ushawishi mwingi uliofanywa na baadhi yao kuwa walikuwa tayari kubadilika na kukubali mawazo pingamizi.

Wakati ambapo vijana wengi wenye damu ya siasa wanajiuliza wafanye nini au wajiunge na chama gani, na wakati ambapo wana ccm wengi marekani na sehemu zingine wanajaribu kuwashawishi vijana kujiunga na chama chao bila mafanikio, nafikiri hii thread itapanua mawazo na mwelekeo wa maamuzi hayo.

Asante
 
Jamani kwani nini kilitokea kwa Mwita Mwikwabe. Huyu ni jamaa yangu wa zamani sana, nilikuwa nae kwenye shule za public, kisha yeye akaanza mlimani mimi nikasema thanks but no thanks nikatafuta maisha kwingine.

Mwita alikuwa leader since shule, siku zote nafurahia utashi wake. I think alifanya makosa kujoin CCM at the beggining.

Mimi binafsi nimesha challenge vijana wengi wanaowaza kufungua Matawi ya CCM hapa USA. Swali langu kubwa kwao ni why CCM? Kusema kweli wote huwa hawana majibu.

CCM ni sawa na Mafia, you need super connection ili uwe mstari wa mbele.
Thanks but no thanks to CCM

Ni kweli Nape anastahili kupongezwa kwa hatua aliyofikia, lakini afahamu kuwa ni hatua ndogo sana katika ukombozi wa taifa hili. Kama nia yake ni kuleta mabadiliko, si dhani kuwa sehemu ya kuanzia ni ccm! Sababu iko wazi, kuwa huwezi kuanza kazi ya kuvunja msitu wa kuibadili ccm ambayo tayari isha lemaa, ni wazi utavunjika wewe kabla ya wao. Kama unavyoona viongozi wakuu wa ccm wakigwaya kuwajibishana, basi nawe ujiangalie kama alivyosema mwenzangu kuwa "ni sawa na kaa anaetamani kumsaidia kaa mwenzie ambao wote wapo ndani ya kapu kusubiri kukaangwa"

Kuhusu vijana wengi kupenda kujiunga na ccm hasa ughaibuni, ni jambo jepesi tu. Wengi wao walijikuta wako huku majuu kupitia wazazi/ndugu zao ambao wako ccm, na hivyo wanajaribu kujenga hisia kuwa wanahitaji kuwekeza ndani ya chama ili wakirudi nao waambulie japo.

Wengine wanakuwa na mawazo ya kujijengea nafasi, kuwa unapokuwa huku nje kiongozi wa kitaifa anapotembelea huku (Si mnafahamu kama JK alivyokuwa anapitapita), basi unakuwa na nafasi ya kuonana nae na kwa kuwa uko ulaya, basi uwezekano kuwa wewe kuonekana uko ulaya na umetoa mchango kwa chama, basi ukirudi nyumbani untapewa nafasi (Upuuzi tu).

Kwa maana hiyo, ukiangalia kiujumla ni mambo ya kibinafsi na ufisadi wa nafsi kuliko kulipenda taifa. Mimi nadhani, maslahi ya taifa yanatakiwa yawe mbele na sio kuwa nini itakuwa nafasi yangu nitakaporudi Tanzania nikitokea Marekani au Uingereza. Tunatakiwa kutoa michango yetu kwa harakati za kuiendeleza Tanzania, na sio kuwaza kuwa mie nafasi yangu ya uongozi ndani ya chama na serikali itakuwa ipi.
 
Mkuu Nono,

Nakubaliana nawe kabisa isipokuwa kwenye hiyo last para yako. Argument hapa sio kuwa vijana wanataka nafasi za uongozi au la, issue kubwa ni hoja na mapendekezo ya vijana (mwita alidai/omba mafisadi ndani ya chama chake cha ccm washughulikiwe na Nnauye alipinga mazingira ya mkataba wa jengo la UVCCM).
 
Kwa vijana wote wa JF ambao ni wanachama wa CCM kina Field marshall ES, nakuombeni fikirieni upya...
Nitarudia kusema, ni vigumu sana kuweza kuleta mapinduzi ya kweli ukiwa ndani ya CCM,

Nape chukua hatua, vaa ujasiri. Unaweza kutumika vizuri zaidi kwingineko kuliko huko CCM. Ningekuelewa enzi za chama kimoja ambapo hapakuwa na alternative, lakini leo hii, hapana. I know you, you're bigger and bolder than CCM. Nakwambia hao jamaa zako CCM watakuzesha na kukupa magonjwa ya moyo bila sababu za msingi. You will never change them, they will only change you!Take a step comrade, join the dream team that wants to change the country for the better. You will never regret!

Matatizo ndani ya vyama ni ya kawaida sana, ndio maana marehemu Wangwe alijaribu kusahihisha akiwa ndani ya chama chake, lakini haikifanyia chama kile kua kibaya au anything, na kushinda jimbo moja la uchaguzi haiwezi kuwa sababu ya kukimbia vyama vyetu vya siasa,

Wakuu Bob na Kitila, asanteni sana labda tukikutanisha mabadiliko ya kutoka kwenu huko Chadema na sisi kutoka ndani ya CCM, basi tutalisaidia sana taifa, lakini haiwezekani wote tukahamia huko Chadema, sasa hatutakua na competition nationally, maana kama ni mafisadi ukweli uko wazi kabisa kuwa hata wao wanawa-admire sana kina Mwakyembe na the likes, maana wanajua kuwa ni viongozi wenye nguvu kisiasa na wanaoheshimika sana na wananchi, maana nasikia huko Tarime at one point Komba aliambwia ashuke jukwaani maana ni fisadi,

Juhudi zote za Mkamba kutaka wabunge kina Mwakyembe na the likes kwenda huko Tarime, zilipokwamba alimtumia ujumbe rais kuwa hakuna ushindi huko, maana wananchiw engi wa Tarime walimfahamsiha Makamba mapema kabisa kwamba bila wabunge wanaopinga mafisadi CCM haitapata kitu huko,

Kwa hiyo wakuu heshima mbele wkamba mmeshinda Tarime, lakini huko mbele tutakutana tu maana very soon CCM tutakubali kwamba hatuwezi kushinda na ufisadi na tutakubali mabadiliko.
 
Nape karibu ukumbini....Umezungumzia Utaifa kwanza kabla ya itikadi,...Safi sana...Ila wote tunajuwa hiyo siyo DNA ya ccm....Its just not in their DNA...Ama ukitaka nitakwenda ku copy and paste ile hotuba ya Makamba Bungeni.

Siyo nia yangu kusema kuwa ni vyema uhame chama...Lakini based na kauli yako ya Taifa kwanza....Then this is how i look at it...

First of all...Kwamba kwasasa due to the limitations za itikadi kwanza...Bado uko kwenye mgogoro wa jengo(Maslahi ya uvccm kama sijakosea) Zakumi yeye anadai kuwa ni pesa za wananchi kwani ndizo zilitumika kuanzisha hiyo institution...Huko sina haja ya kwenda kwasasa kwasababu all in all ni mali ya watanzania wote.

Sasa kwa upana zaidi...Kuna TANGOLD,KIWIRA,BUZWAGI,EPA....etc. Utakuwa na wigo mpana zaidi wa uhuru wa kuyazingatia maslahi ya Taifa kama uta take another step now baada ya hilo jengo sasa tunaendelea na the rest.

Kama walivyoonyesha wana jf wengi hapa...Tuna appreciate resolve uliyoionyesha...Hiyo ni one step...Kama kichwa cha habari cha mada hii kinavyoweka wazi kuwa vijana wengi wamekata tamaa na chama chenu.

What further steps are you intending to overcome that obstacle?

Ndani ya ccm UFISADI ndiyo main agenda..

Sasa ufisadi wa mkataba wa jengo mbinde hivyo...EPA na Kiwira na Tangold ingekuwa vipi?

Ni kivipi vijana watakuwa na uwezo wa kuyazungumzia maslahi ya Taifa wakiwa ndani ya ccm bila maisha yao a kisiasa kuwa hatarini?
 
Field Marshall ES,
Matatizo ndani ya vyama ni ya kawaida sana, ndio maana marehemu Wangwe alijaribu kusahihisha akiwa ndani ya chama chake, lakini haikifanyia chama kile kua kibaya au anything, na kushinda jimbo moja la uchaguzi haiwezi kuwa sababu ya kukimbia vyama vyetu vya siasa,
..
Mkuu ujumbe mzuri sana huu isipokuwa tunapopishana ni malengo ya Ukombozi wako.. Chacha Wangwe alikuwa na nia ya kubadilisha mwelekeo mzima wa baadhi ya makosa ndani ya Chama, wakati hapa mimi, wewe na huyu Nnauye tunazungumzia makosa makubwa zaidi ambayo yanalihusu Taifa zima yaliyotokana na fikra za kizazi kilichopita...
Wangwe ni sawa kabisa na kina Mwakyembe ambao wanajaribu kuleta mabadiliko ndani ya chama, baadhi ya vitu vilivyofanywa kinyume ya maadili ya chama kwa hiyo kulihitaji marekebisho.
Kwa hiyo, ikiwa kweli Mwakyembe and the likes are more than just regulator na wameona jinsi chama kinavyokwenda mrama Kitaifa, then watafanya kama walivyofanya Wachina.. Kuungana na wanafunzi (wananchi) kuwatia ndani viongozi wa juu wa chama (China iliwaweka the big four rumande) kisha kutazama mrengo mpya na uongozi mpya!..Hili haliwezekani na wala sio kabisa lengo la Mwakyembe isipokuwa kurekebisha baadhi ya matendo sio watu ili kurudisha hadi ya chama...
Maandiko yako mengi humu JF mkuu yamekuwa sumu ya dira ilnayochukuliwa sasa hivi na Utawala uliopo madarakani na huwezi kubadilisha Msahafu kirahisi bila kuitwa wewe mchawi.. Ndio maana nikasema wakati wa Utume umekwisha.. umepitwa na wakati kwani mitume walikuja kati yetu kuwaongoza WATU WOTE waliokwisha potoka ktk Imani na matendo yao na kuwapa msahafu mpya wenye mwanga zaidi..
Leo hii, sio kila mtu amepotea, sio kila mtu anafuata msahafu bandia, kwa hivyo ni muhimu ushindi upatikane kwa wewe ku join the right side ili kuongeza nguvu ya mapambano kwani competition sio mimi na wewe ila ni sisi sagainst hao wazee mafisadi wakoloni weusi..
Mkuu Leo hii hapa kwetu Conserative wameshinda tena uchaguzi! na kosa kubwa lililofanyika ni utengano kati ya Liberal na Democratic (NDP) ambao hawana tofauti kabisa ktk sera na malengo yao isipokuwa tofauti za Kipumbavu..
UMOJA ni NGUVU mkuu
 
Magabe, et al.,

Niliwahi kuandika article ikielezea, pamoja na mambo mengine, kwa nini vijana kama Nape wanaendelea kubaki CCM. Hebu jaribu kuisoma hapa chini uone kama inajibu baadhi ya hoja zako.
_________________________________________________________________

CCM ya Nape ni nadharia, ya Nchimbi ndiyo iliyopo

na
Kitila A. K. Mkumbo (Tanzania Daima, 24 Septemba 2008)

NIMEFUATILIA, kama ilivyo kwa Watanzania wengine, &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];mgogoro' wa kifikra na mtazamo kati ya aliyekuwa mgombea wa nafasi ya uenyekiti katika Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Nape Nnauye na mwenyekiti anayemaliza muda wake katika umoja huo, Emmanuel Nchimbi.

Hata hivyo nikiri mapema kabisa kuwa sielewi mantiki ya mgogoro huu na hatimaye mjadala uliofuata na unaoendelea.

Nisichoelewa hasa ni msingi wa dhamira ya Nape katika hoja yake ya kupinga mkataba wa mradi wa ujenzi wa jengo la makao makuu ya UVCCM, ambayo imevuta hisia za watu wengi, ndani na nje ya CCM.

Najiuliza maswali mawili. Mosi, je, Nape ameibua hoja ya kupinga mkataba &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];haramu' wa mradi wa ujenzi wa jengo la UVCCM kama karata na turufu ya kumwezesha kushinda kiti cha uenyekiti wa umoja huo?

Pili, ni kweli kwamba Nape ni miongoni mwa wana CCM wachache &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];waliokoka' na kujiunga na kundi kubwa la wananchi wanaochukizwa na kukerwa na mwenendo wa ufisadi miongoni mwa viongozi waandamizi wa CCM na serikali yake?

Kama msingi wa hoja ya Nape ni ule wa kwanza, wa kutumia hoja yake kama turufu ya kuvuta hisia za wana UVCCM wenzake ili wamchague kuwa mwenyekiti wao, ni wazi kuwa amekwishashindwa kabla hajaanza.

Kwa msingi huu, anachojaribu kufanya Nape ni kuvunja misingi mama ya kanuni za ushindani ndani ya CCM.

Nape anataka achaguliwe kwa misingi ya hoja za kimantiki, uadilifu, ustaraabu, ukweli, uwazi, uhuru na kujitegemea katika kufikiri, zaidi ya yote, kutanguliza utaifa dhidi ya uchama na ukada.

Yote hii ni misingi mizuri, lakini si misingi ya CCM na ndipo upofu wa Nape ulipo. Kwa hoja zake, Nape anajaribu kuweka mlo safi katikati ya jalala la taka.

Hautanoga na wala hataufaidi mlo huo, zaidi ya yote anajiweka katika mazingira hatari ya kuambukizwa vijidudu hatari vitakavyompelekea augue ugonjwa hatari wa matumbo!

Anachofanya Nape ni kupingana na misingi ya kanuni za msingi za kutafuta madaraka ndani ya CCM, ambazo kwa uchache kabisa ni pamoja na ubabaishaji, uzandiki, ujanjaujanja, njia za mkato, unafiki, ghiliba, kujipendekeza, kuiba wajumbe na kuwaficha.

Muhimu zaidi kuliko zote, kutanguliza ukada na uchama dhidi ya uwezo wa kiuongozi na kiutendaji na uzalendo kwa nchi. Hii ndiyo CCM ambayo Nape anajaribu kuibomoa na ambayo Nchimbi na wenzake kina Makamba wanaipigania.

Kwa hiyo utaona kwamba CCM ambayo Nape anajaribu kuipigania haipo, ni nadharia. Iliyopo ni ile CCM ambayo Nchimbi na Makamba wanajaribu kuilinda kwa mafanikio makubwa.

Niliwahi kuwa mwanachama na kada mwaminifu wa CCM kwa muda kidogo na nilijaribu kugombea nyadhifa kadhaa katika UVCCM, kwa bahati nzuri nilishindwa zote!

Kwa uzoefu nilioupata ni kwamba hushindi uchaguzi ndani ya CCM kwa kuwa na uwezo au kwa kujenga hoja za kimantiki zinazoweka maslahi ya nchi mbele.

Unashinda uchaguzi ndani ya CCM kwa kujifanya wewe ni kada kuliko mwingine yeyote, kwa ujanja ujanja, kwa kujipendekeza na kujipitishapitisha kwa baadhi ya wakubwa wanaoingia kwenye vikao muhimu vya CCM kurubuni wajumbe wa vikao, ikiwemo kuwaficha wajumbe wa vikao hivyo.

Ukitaka kushindwa kirahisi katika uchaguzi wa CCM, uonyeshe uwezo na utangulize mambo ya taifa mbele badala ya ukada. Kama kuna kiongozi wa CCM aliyeshinda uchaguzi ndani ya chama hicho kwa kujenga hoja za kutetea masilahi ya taifa dhidi ya ukada awe wa kwanza kujibu makala hii.

Nape, wana CCM wengine makini wanajua vizuri kwamba ingekuwa ni suala la uwezo na kutanguliza masilahi ya taifa, Rais Jakaya Kikwete asingewashinda Salim Ahmed Salim, Mark Mwandosya na hata Frederick Sumaye.

Pamoja na mambo mengine, sifa kubwa iliyomfanya Rais Kikwete awashinde wenzake katika kinyang'anyiro cha kugombea urais ni ukada wake wa muda mrefu katika CCM.

Kwa hiyo katika CCM ukada ndiyo sifa mama na kigezo muhimu cha kuweza kuchaguliwa. Ndiyo kusema Nape anapojaribu kutanguliza utaifa, tena kwa kuzomea ufisadi, ambayo ni nguzo muhimu ya kuwepo kwa CCM, kama turufu ya kutaka achaguliwe kuwa mwenyekiti wa UVCCM, anajaribu kukata mbuyu kwa wembe. Hataweza, atajikata mwenyewe na kuuacha mbuyu umesimama kidete.

Pengine tumpe Nape, ile Waingereza wanaita: "The benefit of doubt". Kwamba Nape ni miongoni mwa wana CCM wachache waliookoka hivi karibuni, ameamua kujitoa mwili na roho katika kujiunga na majemadari wa vita dhidi ya ufisadi.

Kuokoka kupo si tu katika siasa na dini, lakini pia katika nyanja nyingine za maisha ya kijamii. Lakini unapoamua kuokoka lazima ujue na uzingatie misingi ya wokovu, vinginevyo utaanguka tena.

Kuokoka kisiasa na kidini kunahitaji ujasiri wa kukubali kusutwa na kuacha mazoea. Ili ukamilishe wokovu lazima ukubali kubadilika kimwili na kiroho.

Ninachokiona hapa ni kwamba Nape amekwisha kutoka CCM kiroho, kiakili na kisaikolojia lakini bado amebaki kimwili. Hili ni tatizo linalowakumba wana CCM wengi.

Ninaamini kuna wana CCM wengi waliokwisha kukihama chama chao kiroho, kiakili na kisaikolojia, lakini wameendelea kubaki huko kimwili kwa kukosa ujasiri au kwa sababu zingine, ikiwemo kuamini kwamba ipo siku CCM itabadilika.

Nikiri kuwa mimi ni mmojawapo, ambaye ilinichukua takriban miaka mitano kuhama CCM kimwili. Nilikuwa nimeachana na CCM kiroho, kiakili na kisaikolojia tangu mwaka 2000, lakini ilinichukua miaka mitano hadi 2005 nilipoamua kujitoa hadi mwili na kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Binafsi nilijitoa CCM baada ya kujiridhisha bila shaka kuwa CCM imefikia hatua ya usugu, na haiwezekani kubadilika. Ni hatua ambayo vyama dada kama KANU, ZANU-PF na UNIP vilipitia na ambayo ni wananchi pekee wenye uwezo wa kuibadilisha.

Kama kweli tumechoshwa na madhira ya CCM, ikiwemo ufisadi, inabidi tufike mahala tukubali kuachana na CCM. Kuendelea kuibakisha CCM madarakani ni kukubaliana kwamba, pamoja na kwamba tumeumia kama nchi, bado tunaweza kuendelea kuwavumilia CCM, hatujaumia vya kutosha.

Kufikiri kwamba CCM inaweza kubadilika ni njia nzuri ya kujiridhisha kisaikolojia baada ya kushindwa kuitoa madarakani, lakini haisaidii kubadili hali ya mambo katika nchi yetu.

Kwa hiyo, Nape ana mambo mawili ya kuchagua. Mosi, anaweza akaendelea kubaki CCM kimwili na kuisaliti dhamira yake ya ndani na akaendelea kupiga kelele za ufisadi, ambazo zitazidi kumtenga na wenzake ambao &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];hawajaokoka' katika CCM, na hivyo kuendelea kuonekana kituko! Pili, anaweza akauvaa ujasiri kwa kuamua kuutoa mwili wake kutoka CCM na kuupeleka kule ambapo akili na roho zipo. Uamuzi ni wake.

Inapatikana pia hapa: 古書の買取はどこでやるのがお得?昨今の買取事情をまとめてみました

Prof ulioa mbali..
 
Back
Top Bottom