Jamani mie hio sheria za kazi ninazo hapa na hakuna mahali ilipoandikwa kuwa MADAKTARI au KADA YA AFYA HAWARUHUSIWI KUGOMA ila imeandikwa HUDUMA ZA AFYA za DHARURA ndio hawataruhusiwa kugoma!Umeanzisha kitu kizuri mkuu na umetoa hoja nzuri tu. Ila sijaridhishwa na heading yako. Ni vema ungekaribisha hata wale wale wanaounga mkono huu mgomo ili uweze kuzipima hoja zako dhidi ya wale wanaounga. Binafsi siungi mkono kwa sababu
1. Hii sekta hawatakiwi kugoma kwa mujibu wa sheria kama ilivyo sekta ya maji
2. Mahakama imezuia. Kama nchi yoyote ile lazima kuwe na ORDER ili mambo yaende
3. Kima cha mshahara cha 3m ni kikubwa kwa nchi maskini kama tz. Hoja ya kwamba wabunge wanalipwa hivi, mara vile haitoshi kuwa kigezo. Mazingira magumu ya kazi ni katika sekta nyingi sana. Walimu, polisi n.k.
Mimi nawachukulia kama wahaini na serikali katika hili inyooshe makucha ili watu waheshimu mamlaka
Sasa hapa naomba tusipotoshane kama mnataka kujenga!! Hata PINDA NA MWINYI nao wamejaribu kupingisha ukweli kama mnavyofanya nyie. Tusiwe DHAIFU hadi kujenga hoja!
Madaktari wana haki ya kudai maslahi yao na tangu wadai siku zaidi ya 90 zimepita na Mahakama haina ubavu wa kufanya lolote kwani haiwezi kuforce daktari kutibu.
Hilo la uhaini hakuna sheria yoyote inayomlabel mtu aliyegoma kuwa MHAINI labda Muitunge leo!!!
Na kwa jinsi mlivyo DHAIFU sidhani kama hili litawezekana!!!!