Kwa wote tunaopinga mgomo wa madaktari

Mi nawasapoti madaktari. Hospitali zenye huduma ni za Dar tu. Huku mikoani ndo balaa zaidi
 
Ujue mi nashindwa kuelewa hivi ni kweli tuna serikali dhaifu kwa kiwango hiki?Haiwezekani wakawa wanarudia makosa yale yale kila siku wakati wanaelewa madhara yake.Ni kwanini hawatekelezi makubaliano yao ya awali,then wakae kwa hayo ambayo hawajakubaliana
 
umesema vyema jkusikia upande wa pili ili uweze compare mkuu, naomba ufahamu kila mtu akifanya kosa haimaanishi si kosa au kuhalalishwa kwa kosa na kuna tofauti kati ya james rashida na john, polis walimu wanamazingira magumu haimaanish wameridhika na utofauti katika kudai au kushughulikia matatizo yao upo wazi, umewahi kufikiri nn chanzo cha kushuka kwa kiwango cha elimu kwa kiasi cha kutisha? umewahi hata tafakari kwann rushwa na matendo maovu kukithiri katika watu hawa walinda usalama?
ni rahisi sana kutupia lawama lakin kama usemavyo kuna pande mbili maana kisababishi na kinachotendeka, umewahi kuugua ndugu yangu? umewahi kulazwa kwenyehospitali ya umma? naamin waz aliyewahi lazwa katika hospitali hiz atakuwa shahid ya hali ya kusikitisha lakin wagonjwa hawalalamiki na haimaanishi wanafurahishwa ni lwa kuwa huwez enda kudai kitanda wakati una maumivu makali na zaid kuwa ni sehemu ya muda mfupi, hvyo basi kuna mtu anapaswa kuyasemea haya na madaktari hawakupaswa kuwa watu sahihi wa kuyasemea lakin "bubu hutaka kusema mambo yanapomzidia"
nikukumbushe ndugu yangu katika kila kazi na chochote katika maisha ufanyacho evaluation ni jambo la msingi, kuangalia success ya any means ulotumia katka kufanya kitu hapa nataka nikuenlight kuhusu kurudi mazungumzoni, matatizo sekta ya afya hayakuanza leo mfano mdogo tu hiki tunachokiona kilianza mwez january kama sio desemba unahisi kwa miez mitano ya mazungumzo bado kuna success?????? walimu unaowasemea wameingia lini mazungumzon? kuna lolote walopata katika hayo mazungumzo?????? hadi leo hii wewe umekiri wana hali ngumu u still believe hali yao itabadilishwa na mazungumzo??
naungana nawe kuwa mgomo si njia sahihi ya kutafuta suluhu and tunaongelea maisha ya watu hapa, trust me huwezi jua thaman ya hewahadi siku ukipata pumu coz kila siku ipo na hujawahi fikiria kuhusu hewa ya kesho, ndugu zetu wanafariki na kuteseka sana pasipo na mgomo kuliko pakiwa na mgomo, nmeshashuhudia wagonjwa wakiambiwa 'hatuna lakufanya zaid mama kwasababu kitu fulani hakuna labda uende regency' mtu huyo hana chochote akafanye kipimo cha laki 3, tamadun yetu ni kuwa ili nijue unaumwa ni either ulalame au nikukute umelala, uil neva be trusted unaumwa endapo unaendelea na shughuli zako, so bila kupiga kelele hakuna anaelewa hali iliyopo mahosptalini
maoni yangu tujikite zaidi katika kutafuta suluhu kwa kutoa alternatives na sio kulaumu, hakuna kilichofanikiwa katika mzungumzo then nn kifanyike next
 
umekosea bro taaluma zote hazitegemeani bali zote zinategemea uhai? na katafute definition ya kiwa "too demanding"
 
kumbe we mwanajeshi. Siku zote mtu akiingia jeshini huwa anaacha akili zake getini zinaendelea kuoza. Hivi unadhani bajeti anayopelekewa marina inatosha kununua ct? Mbona umesahau kwamba hospitali za wilaya zinaagiza dawa msd miezi sita bila kuletewa? Siku zote mkishakuwa kwenye neema huwa mnasahau wenye shida. Hivi hayo mazungumzo yanawezekana leo na walikuwa na miezi mitatu? Kwa nini waje kuanza kuomba mazungumzo dakika za mwisho? Huu ni utani na udhaifu ambao hatutaki wauendeleze.
sio daktari huyo mamluki tuuuuu
 
Umeanzisha kitu kizuri mkuu na umetoa hoja nzuri tu. Ila sijaridhishwa na heading yako. Ni vema ungekaribisha hata wale wale wanaounga mkono huu mgomo ili uweze kuzipima hoja zako dhidi ya wale wanaounga. Binafsi siungi mkono kwa sababu
1. Hii sekta hawatakiwi kugoma kwa mujibu wa sheria kama ilivyo sekta ya maji
2. Mahakama imezuia. Kama nchi yoyote ile lazima kuwe na ORDER ili mambo yaende
3. Kima cha mshahara cha 3m ni kikubwa kwa nchi maskini kama tz. Hoja ya kwamba wabunge wanalipwa hivi, mara vile haitoshi kuwa kigezo. Mazingira magumu ya kazi ni katika sekta nyingi sana. Walimu, polisi n.k.
Mimi nawachukulia kama wahaini na serikali katika hili inyooshe makucha ili watu waheshimu mamlaka

Mbona wanajeshi wanalipwa mapesa mengi tu. Yaana mwanajeshi anamzidi mwalimu. Koplo amzidi mwalimu. Nije nkatumia maneno ya mbunge wangu bure, keshasema.
 
sio daktari huyo mamluki tuuuuu
Two mistakes will never make one right.Unapunjwa mshahara halafu unaua watu na unajisifu kabisa.
Hatuwezi kubadili mfumo kwa kuua watu maskini kwa ajili ya kutetea maslahi tukifanya hivyo hatuna tofauti na Al Qaida au Israel ambayo iko radhi kuteketeza familia nzima kwa ajili ya kumsaka mtu mmoja.
Very unfortunate mgomo huu unaendeshwa na MAT lakini tujiulize na tuwekeane takwimu haa kuonyesha MAT ilivyo reprimand Madaktari ambao wamekosa maadili.
Hii inaonyesha ya kuwa maadili hakuna na inadhihirishwa na kauli zinazoandikwa hapa ambapo watu wanajinasibu kabisa kuona watu wakifa katika mazingira ya hospital ambapo ideally tunakimbilia ili kusogeza siku za uhai wetu.
 
Serikari iwabadilishie kazi madaktari na kada zingine, kwa mfano; wanasheria waende wakatibu na madaktari waende kusimamia kesi mahakamani. Au manurse wapelekwe hotel za kitalii na mahotelier waende kutundikia wagonjwa maji na kuwapa vidonge.
Imesemwa kada zote ni muhimu, hivyo kazi ya madaktari inaweza kufanywa hata na polisi au walimu kwa vile ndio waliowafundisha madaktari.
Wabunge na mawaziri wanahitaji kuongezewa mishahara na posho ili wawatumie viongozi wa dini kuzuia watu kuugua.
Serikari yetu ni sikivu nainajali, natumaini maoni yangu itayafanyia kazi.
 
Kwa mtazamo wako Daktari, ni kheri mtu akate roho usipokuwepo kuliko akikata roho ukiwepo? Hii ndiyo itakuwa nafuu yako? Huoni kuwa ukiwepo kuna jambo unaloweza kulifanya kuokoa maisha ya mtu. Kuna wakati daktari anaweza kuokoa maisha ya mtu hata bila kutumia kifaa chochote bali utaalam wake tu. Kazi ya daktari ni kumuondolea mgonjwa shida aliyonayo kwa wakati ule kwa jambo alilo na uwezo nalo lakini sio vinginevyo. Hakuna mtu yeyote atakayekulaumu kwa jambo usilokuwa na uwezo nalo. 'Play your part it can be done'. Wakati mwingine vifaa kama Urine bags vinakosekana kwa sababu Uongozi dani ya Hospitali husika ambao unajumuisha madakitari kutokuweka vipaumbele vya vifaa wanavyohitaji. Hapa sio watu wakada nyingine wanaosababisha upungufu ni madaktari wenyewe. Dawa zingine huhamishwa na wafamasia na kuzipeleka kwenye Pharmacy zao binafsi, leo nao wamo kwenye mgomo wakiilaumu serikali kusababisha upungufu wa vifaa. Hii sio haki. Ni kweli kuna upungufu wa vifaa, lakini dawa yake haiwezi kuwa ni kugoma. Dawa ya tatizo haiwezi kuwa ni kuongeza tatizo. Ikiwa mgonjwa anaumwa malaria dawa yake haiwezi kuwa ni kumwongezea vichome ili vyote vitibiwe kwa pamoja. Nadharia hiyo ya madaktari inajengwa katika msingi potofu. Rudi kazini kutatua tatizo lililopo wakati suluhisho la matatizo mengine. Ningewaunga mkono madaktari kama wangesema kuanzia sasa HATUTATOA MEDICAL REFERRAL KWA WAKUBWA KWENDA KUTIBIWA NJE MPAKA HOSPITALI ZETU ZITAKAPOPATIWA VIFAA VYA KUTOSHA. Adhabu hii ni sahihi kwa sababu ingekuwa inawalenga wahusika na sio wanyonge hohehahe ambao pia wanawalalamikia watunga sera haohao kwa kujilimbikizia mali kupitia matibabu huku fedha hizo kiduchu zingeweza kuboresha huduma hospitalini. Nina imani watanzania wengi na hata mataifa mengine wangewaunga mkono. Fedha ambayo ingeokolewa kwa sinikizo hilo ingenunulia vifaa tiba na dawa nyingi tu
 
Umeanzisha kitu kizuri mkuu na umetoa hoja nzuri tu. Ila sijaridhishwa na heading yako. Ni vema ungekaribisha hata wale wale wanaounga mkono huu mgomo ili uweze kuzipima hoja zako dhidi ya wale wanaounga. Binafsi siungi mkono kwa sababu
1. Hii sekta hawatakiwi kugoma kwa mujibu wa sheria kama ilivyo sekta ya maji
2. Mahakama imezuia. Kama nchi yoyote ile lazima kuwe na ORDER ili mambo yaende
3. Kima cha mshahara cha 3m ni kikubwa kwa nchi maskini kama tz. Hoja ya kwamba wabunge wanalipwa hivi, mara vile haitoshi kuwa kigezo. Mazingira magumu ya kazi ni katika sekta nyingi sana. Walimu, polisi n.k.
Mimi nawachukulia kama wahaini na serikali katika hili inyooshe makucha ili watu waheshimu mamlaka
Na wao wagome kama wana umoja walionao madaktari, hii nchi haiheshimu kabisa kazi za taaaluma, siungi mkono hoja yako wala hoja ya muanzisha uzi.

Ukisema hii nchi ni masikini, watu wanaojua na kufikiri watakushangaa, wao wanagawana kila kinachopatikana kila uchao, uwezo wa kuwaongezea maslahi wafanyakazi wanao, lakini kutokana na uchoyo wao na kutojali wenzao wameamua kwa makusudi kula na kuvimbiwa wakati wenzao wanalala njaa.

Go Drs Go, saa ya ukombozi wa wafanyakazi ni sasa, onyesheni mfano.
 
Kwa mtazamo wako Daktari, ni kheri mtu akate roho usipokuwepo kuliko akikata roho ukiwepo? Hii ndiyo itakuwa nafuu yako? Huoni kuwa ukiwepo kuna jambo unaloweza kulifanya kuokoa maisha ya mtu. Kuna wakati daktari anaweza kuokoa maisha ya mtu hata bila kutumia kifaa chochote bali utaalam wake tu.
Hebu fafanua hapo kwenye red, kama hakuna dawa daktari atampa nini mgonjwa apone hata kama utaalamu anao, mgonjwa anahitaji oxygen daktari atampulizia pumzi yake, daktari na utaalamu wake kuna vitu ambavyo hawezi kugundua mpaka afanye vipimo, kama reagents za kufanyia vipimo hakuna, anafanyaje kazi.

Naomba muache ushabiki na kuangalia reality, juzi nilikuwa kwenye hospitali moja ya wilaya, mgonjwa amekuja anataka kujifungua, hana gloves na hospitali hazipo kwa kuwa pesa hakuna, nurses wakabaki wanamuangalia wafanye nn, wewe ungetaka wamsaidie kwa mikono ili wao wapate ukimwi na hepatitis B. Hakuna mtu anaweza kuhatarisha uhai wake kwa uzembe na kutojali kwa serikali yako inayoongozwa na viongozi DHAIFU
 
Hebu fafanua hapo kwenye red, kama hakuna dawa daktari atampa nini mgonjwa apone hata kama utaalamu anao, mgonjwa anahitaji oxygen daktari atampulizia pumzi yake, daktari na utaalamu wake kuna vitu ambavyo hawezi kugundua mpaka afanye vipimo, kama reagents za kufanyia vipimo hakuna, anafanyaje kazi.

Naomba muache ushabiki na kuangalia reality, juzi nilikuwa kwenye hospitali moja ya wilaya, mgonjwa amekuja anataka kujifungua, hana gloves na hospitali hazipo kwa kuwa pesa hakuna, nurses wakabaki wanamuangalia wafanye nn, wewe ungetaka wamsaidie kwa mikono ili wao wapate ukimwi na hepatitis B. Hakuna mtu anaweza kuhatarisha uhai wake kwa uzembe na kutojali kwa serikali yako inayoongozwa na viongozi DHAIFU
hata kum position mgonjwa kunaweza kuokoa maisha yake achilia mbali maarifa mengine mengi tu.Unataka kuonyesha ya kuwa aliyeandika haelewi kitu lakini si kweli.
Hospitali ya wilaya iliyokosa gloves kaangalie DMO ni nani na Mo in charge ni nani na pia katafute matumizi ya basket na revolving funds na utajua ni nani anayesababisha vifaa vikosekane.
Tatizo la sasa ni kuwa hata diagnosis ya ectopic preganacy mpaka ulta sound na kama ultra sound ni mbovu mgonjwa.
Hitimisho,kuweni wazi mnapigania maslahi yenu au vitendea kazi?Mkipewa vifaa bila nyongeza mtarudi kazini?
 
hata kum position mgonjwa kunaweza kuokoa maisha yake achilia mbali maarifa mengine mengi tu.unataka kuonyesha ya kuwa aliyeandika haelewi kitu lakini si kweli.
Hospitali ya wilaya iliyokosa gloves kaangalie dmo ni nani na mo in charge ni nani na pia katafute matumizi ya basket na revolving funds na utajua ni nani anayesababisha vifaa vikosekane.
Tatizo la sasa ni kuwa hata diagnosis ya ectopic preganacy mpaka ulta sound na kama ultra sound ni mbovu mgonjwa.
Hitimisho,kuweni wazi mnapigania maslahi yenu au vitendea kazi?mkipewa vifaa bila nyongeza mtarudi kazini?
vyote kwa pamoja, hivi kwa nini huamini kwamba hata gloves zinakosekana kwenye hospitali za wilaya? Ni lini ulifika huko, mgonjwa anaeumwa nini ukimpozisheni anapona, positioning itafungua njia ya hewa tu, lakini kama tatizo la msingi halijatatuliwa atakufa tu baada ya muda mfupi wa kupumua
 
Siungi mkono mgomo wa madaktari kwa sababu waathilika ni walala hoi. Siungi mkono serikali kujifanya ndio vidume vya maisha yetu.

Madaktari wanafahamu madhara lakini wafanyeje kama maisha yao yanategemea ajira yao? Ng'ombe hana kawaida ya kuuma mtu lakini walipofika madaktari, hakuna jinsi. Nasikitika lakini sina namna ya kuwashauri wasigome, ni kumwomba Mungu aingilie kati Mawaziri leo na kesho waumwe matumbo ya kuharisha non-stop kama adhabu ya kutotujali wananchi.

Serikali kutotekeleza mahitaji ya madaktari sio kuwakomoa maDR bali walalahoi wetu.

Mungu tuokoe na uongozi huu




L
Nashukuru umenielewa.
Naomba upitie michango yote kwa umakini na utagundua udhaifu mkubwa kwa Watanzania.
Kwanza nimeanzisha thread kwa wanaopinga migomo lakini pro mgomo wameingia na hawa ni wale ambao hata instructions katika mitihani hawasomi.
Jambo la pili ni kuwa watu wanaamini ya kuwa ukuiacha watu wafe,watu wataichukia CCM na serikali itaanguka,hilo linaweza kuwa kweli kwingine lakini si Tanzania.Tumeshuhudia watu wakiuza kitambulisho cha kupigia kura kwa shilling elfu mbili tu.
Tatu ni kuwa tuna generation ambayo ni egocentric na myopic.Watu wanaamini ya kuwa watakaoumia hawamhusu,this is very unfortunate.
Tuna madaktari ambao hawana moral na ethical principles na pia hawana ujasiri kwani kesho wakiitwa Ikulu watakwenda na wakitoka hapo watatangaza wenyewe kuwa tumefuta mgomo.
Tayari mmeshailegeza serikali basi acheni vitisho nendeni mkaongee mkiwa na hoja na ushahidi wa maneno yao nasi tutakuwa nyuma yenu.
Siku njema kwa wachangiaji woteeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
 
Hata kabla ya Mgomo watu wanakufa ili Madaktari wahudumie wagonjwa na tupate matokeo mazuri tunatakiwa tuwalipe vizuri watu wanao hudumia wagonjwa na Dawa na Vifaa tiba viwepo na viwe sahihi na vinavyofanya kazi vizuri, kuwa na watoa huduma wanaolipwa kidogo na kukosa vifaa tiba ni sawa 2 na kutokuwa na watoa huduma za afya na watu watakufa sawa na vile ambavyo wapo kazini. Rai yangu kwa serikali iwape thamani sitahiki watoa huduma wa afya kwa kutimiza madai yao na serikali ipeleke dawa na vifaa tiba kwenye hospitali na vituo vya afya. inashangaza kusikia serikali imetumia 5bn kununua dawa na 7bn kulipa wagonjwa waliokwenda kutibiwa nje ya nchi ni kuwa ua watanzania wengi ambao hawaendi India kutibiwa. Mbunge 10,000,000/ kwa mwezi na Dr 950,000/ ni kupuuza dhamani ya watu muhimu zaidi kama tunathamini uhai wawatanzania
 
Tumefanywa kuwa sugu kutokana na mazingira magumu ya kazi........... trust me, ungekuwa ni dokta ungenielewa, hakuna kitu kinachoumiza kama mgonjwa kukata roho mikononi mwako kwa sababu hamna adrenaline na wakati ulikuwa na uwezo wa kuokoa maisha yake!!! hatutaki vizazi vijavyo vya madokta wa tz wawe kama sisi thats why tunalia kila siku hali ibadilike
Mimi nitawashangaa sana mkirudi nyuma. Mgomo wenu waweza kuonyesha njia ya ukombozi si kwa madaktari tu, bali watanzania wote. Mleta mada anasema tuogope siku mtu wa chini akiamua kuchukua hatua. Mimi nasema kama mgomo huu unaweza kumchocheaa huyo mtu wa chini hadi kuamua kuchukua hatua, kazeni buti. Tungekuwa na huduma za afya tusingewasikia kila siku wakipishana kwenye corridor za mahospitali India. Mabadiko tunayahitaji sote si nyie madaktari tu. You have the support of every patriot.
 
Tarehe 3/6/2012 Jumapili Ndugu yangu amefariki mikononi mwa Daktari Hospital ya Rufaa ya Temeke kwa kukosa oksjeni masaa 3 Manesi na Dr hawana cha kumsaidia mgonjwa , Hakuna hata Drip za maji tulikwenda kununua pale temeke, Dr 1 manesi wawili wako zamu ajali jumapili ile zilitokea 3 wagonjwa wa ajali 8. Waanze yupi wa mwache yupi, Gari la kupeleka wagonjwa lipo 1, nesi wakusaidia kupeleka mgonjwa rufaa muhimbili hakuna wako 3 hospital temeke usiku. Ni kweli Serikali hii imepuuza Afya za watanzania. Tusidanganywe na maneno ya wanasiasa wanaojifanya wanahuruma na sisi eti Madaktari wawe na huruma. wao ndo ilikuwa wawe na huruma kwa kuipa kipaumbele sekta ya afya ambayo hata bajeti hii imepungua kuliko ilivokua mwaka jana kwenye bajeti. Hivi wananchi wakiulizwa nani alipwe kati ya Mbunge na Daktari watasema nani alipwe? Kweli Taifa langu linaangamia kwa kukosa Maarifa
Tumefanywa kuwa sugu kutokana na mazingira magumu ya kazi........... trust me, ungekuwa ni dokta ungenielewa, hakuna kitu kinachoumiza kama mgonjwa kukata roho mikononi mwako kwa sababu hamna adrenaline na wakati ulikuwa na uwezo wa kuokoa maisha yake!!! hatutaki vizazi vijavyo vya madokta wa tz wawe kama sisi thats why tunalia kila siku hali ibadilike
 
zomba
Kwa sababu kazi yao haiwaruhusu kugoma kisheria. Na mahakama imetoa ufafanuzi.

Kama wanaona kazi hiyo haina manufaa watafute kazi zingine za kufan

Kazi nyingine gani na wao ni Madaktari wetu? Halafu sisi tutatibiwa na nani? Vipi Mkuu? Unaelewa maana ya kuletewa madaktari kutoka nchi nyingine wakachezea afya zetu na kutufanya sisi kama ngurubai (guinea pigs)? Hoja ya madaktari siyo nyongeza tu ya mishahara bali pia kuondosha mazingira mabovu ya kazi yanayopelekea hata kushindwa kutoa matibabu ya kueleweka kwa wagonjwa anaowatibu. Ukosefu wa dawa na vitendea kazi na mahali pazuri pa kulaza wagonjwa anaowahudumia. Tatizo la viongozi wetu ni kupotosha hoja za msingi. Niulize tu: Ni Daktari gani anapenda kuona mgonjwa anamfia mikononi na huku akijua kwamba angeweza kumnusuru kama vifaa vya drip na dawa zake zingekuwepo? Kwa nini asidai uwepo wa vitendea kazi kwanza ili awe na uhakika wa kutibu vizuri wagonjwa wake? Hoja inayoletwa na wakubwa inataka kupaka rangi ya kuwepo kwa ukatili kwa Madaktari wetu ilihali Madaktari wanatetea hali nzuri na salama katika kuhudumia wagonjwa wao. Vilevile wanadai uwapo wa vifaa vya kujikinga wakati wa kuhudumia wagonjwa na mambo mengi tu yasiyo binafsi. Swali: Kwa nini wakubwa hawaelezei kuboreshwa kwa hospitali zetu?
 
Tuwaunge au tuwapinge tutajijua wenyewe wananchi tuko kama matahira madaktari wanasema hospitali hawana hata tochi za kuchunguzia masikio,machine za x-ray hazifanyi kazi gozi za kufungia vidonda hazitoshi dawa za kuzuia wanawake wasimwage damu baada ya kujifungua hazipo,nyuzi za kushonea hakuna vitambaa vya kufunga midomo yao au gloves za wao kusambaza maambukizi kati ya mgonjwa na mgonjwa hakuna sisi hatuoni na lwetu tufeeee tu ,hatujielewi hatujui wanachokisema ni shauri yetu mpaka hapo tutakapojitambua tutajua wanamaanisha nini
 
Back
Top Bottom