Kwa wazazi: hii kitu inamsaidia nini mtoto?

Ndibalema

JF-Expert Member
Apr 26, 2008
10,956
4,649
Naomba kuuliza kwa wale wenye watoto.
angalia picha hapo chini.
Mkono wa huyo mtoto amevalishwa kamba nyeusi.
Nimewaona watoto wengi hasa uswahilini huvishwa hiyo kitu.
Ni urembo kwa mtoto au hiyo kitu inamaana gani kwa mtoto?
NB: Pichani ni msanii wa bongo fleva na producer maarufu, Bob Junior akiwa na familia yake.
Hapo ilikuwa katika hafla ya kufuturu. ni hafla ya kiimani zaidi.
attachment.php
 
Attachments

  • Bob-Junior-na-familia-yake-800x533.jpg
    Bob-Junior-na-familia-yake-800x533.jpg
    60.1 KB · Views: 2,125
Ni kweli mkuu hii ipo sana tu . Nakumbuka wakati flani mama mmoja mwanae aliugua basi alipomfikisha kituo cha afya dr akaiona hiyo kamba nyeusi akamwambia mzazi arudi tu nyumbani kwani mtoto tayari ana dawa haitaji dawa nyingine. Ilibidi mama yule amvue mwanae hiyo kamba na ndipo alipopatiwa matibabu. Wazazi inapasa tubadilike hii kitu haina nguvu
 
Mimi kwangu naona ni ushirikina zaidi wanaamini ni ulinzi wa watoto dhidi ya wachawi na mambo yanayofanana na hayo.
 
Haimsaidi chochote bali ni urembo tu.
Mila za kizamani
Wengine wanatia mbegu za bangi na kufunga fundo, wakiamini mtoto hawezi kuaribiwa na jini.
Sababu jini hapendi bangi.
 
Imani na more often ni destructive. Nakumbuka dada yangu alijifungua huko Morogoro, majirani wakampa hayo madude. Alivyokuja nyumbani Tabora na mtoto, baba akamuuliza ni nini hiyo. Akaanza kujikanyaga na kujieleza alivyoelezwa, baba akalikata hilo kamba, na kumwambia mbona wewe umekuwa na hukuvalishwa hayo madude.
Nikiangalia tabia ya huyu mtoto, yaani ni kama she is posessed hivi.
 
..alafu cha ajabu wazazi wenyewe hawavai hayo makamba wanawavisha watotot wao tuu!
Nilifikiri kwa kijana wa kisasa hawezi kuendekeza hizo habari lakini nimeshangaa kumwona kijana hapo pichani ana'entertain hizo makitu.
 
Yaani my ndugu umenichekesha sana
 
Kiukweli hii haina maana yoyote hata ukiifikilia kwa akili ya kawaida. Dawa imefungwa kwenye kamba na wala haina uhusiano na damu wala ngozi je itamponyaje mgonjwa? Ingekuwa chanjo pengine tungesema imeingia ndani ya damu kupambana na ugonjwa. Sasa hii inamlinda mtoto kivipi wakati haigusani na ngozi? Jamani mbona kusema inamlinda mtoto asiugue ni sawa na kujenga uzio wa makaratasi ya mfindi?

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Yaani my ndugu umenichekesha sana
It is very true, yaani nikitafuta source za tabia za ajabu ajabu za niece wangu hata sipati zaidi ya devil's work. So huenda kwa kumvalisha hayo mahirizi (kamba) kunakuwa na convenant fulani inakuwa imefanyika sema watu hawajui tu.
 
ni kumkabidhi mtoto kwa shetani akulindie, sasa sijui alipokuwa tumboni nani alikuwa anamlinda.
 
..alafu cha ajabu wazazi wenyewe hawavai hayo makamba wanawavisha watotot wao tuu!
Nilifikiri kwa kijana wa kisasa hawezi kuendekeza hizo habari lakini nimeshangaa kumwona kijana hapo pichani ana'entertain hizo makitu.

Labda yeye haoni tofauti iwepo wala isiwepo lakini wifi anataka, kwanini asifanye kumridhisha?
 
Haisaidii chochote zaid.....kumbebesha mtoto mzigo.
Imani zaid,wengine eti mtoto asilie.
 
Back
Top Bottom