Kwa watumiaji wa Gesi za majumbani.

Triple A

JF-Expert Member
Sep 4, 2011
766
147
Mambo vp wana jf, jamani huwa najiuliza mara kibao lkn sipati jawabu, issue yenyewe iko hivi, hivi ukienda kununua gesi utajuaje kama imejaa ktk mtungi ulioununua? Mimi naona kama tunaibiwa kwani sijawahi kuona mtungi wa gesi una geji ya kuonyesha gesi iko kiasi gani, hili jambo huwa linanichanganya sana naombeni mniweke wazi kwa wanaofaham zaidi.
 
Kwahyo unauziwa kwa kilo siyo,kwa mfano mtungi unakilo 50 utajuaje kiwango cha gesi na mtungi empty?
 
Niliwahi kuona tangazo linasema wakati unanunua hakikisha inapimwa uzito. Uzito wa mtungi pamoja na gas umeandikwa kwenye mtungi, kama sikosei upande wa kulia. Kushoto kuna namba nyingine.
 
Mie nikiona mzito tu najua umejaa na hivo hakuna gauge za kuonyesha uko full
 
Niliwahi kuona tangazo linasema wakati unanunua hakikisha inapimwa uzito. Uzito wa mtungi pamoja na gas umeandikwa kwenye mtungi, kama sikosei upande wa kulia. Kushoto kuna namba nyingine.

Exactly! Hata mimi nimewahi kuona hilo tangazo. Ila ukienda kwa wakala, issue inakuwa simpler. Wanakuonesha weight wakati ikiwa empty na baada ya kujaza! Na kwenye mitungi kuna alama zinazoonesha uzito unaotakiwa in both cases!
 
Kuna mizani ya kupima gesi na ili kujua kama huibiwi angalia hiyo mizani inaonyesha kwenye screen kg ngapi.Halafu compare na gross weight ya mtungi wako.Elewa kwenye gross weight ni total ya net weight na tare weight.Net weight ni ule ujazo halisi wa gesi kwenye mtungi unaweza ukawa kg 15 au 6 kg.Na tare weight ni uzito wa chuma lenyewe.Nadhani utakuwa umenisoma kidogo kama sio sana
 
mfano mtungi wa kg 15 empty ukiwa na gas unakuwa kg 30, kg 6 unakuwa na kg 12 .

jambo la muhim tumia mizan ya muuzaji kujua uhalisia
 
We nunua tu gesi ukatumie kwako,ukijidai unataka na mtungi upimwe kesho yake utakujakuta mizani imechakachuliwa na unaibiwa kwa kwenda mbele.I love my country Tanzania...
 
Mambo vp wana jf, jamani huwa najiuliza mara kibao lkn sipati jawabu, issue yenyewe iko hivi, hivi ukienda kununua gesi utajuaje kama imejaa ktk mtungi ulioununua? Mimi naona kama tunaibiwa kwani sijawahi kuona mtungi wa gesi una geji ya kuonyesha gesi iko kiasi gani, hili jambo huwa linanichanganya sana naombeni mniweke wazi kwa wanaofaham zaidi.

Uwe unatingisha kuona kama imejaa
 
Kuna mizani ya kupima gesi na ili kujua kama huibiwi angalia hiyo mizani inaonyesha kwenye screen kg ngapi.Halafu compare na gross weight ya mtungi wako.Elewa kwenye gross weight ni total ya net weight na tare weight.Net weight ni ule ujazo halisi wa gesi kwenye mtungi unaweza ukawa kg 15 au 6 kg.Na tare weight ni uzito wa chuma lenyewe.Nadhani utakuwa umenisoma kidogo kama sio sana

mkuu mzinga huku nilipo sijawahi kuona mizani nakuta tu mitungi imefungiwa sehem moja mikubwa na midogo ukimwuliza muuzaji atakwambia hana mizani sasa si uwizi huu jamani?
 
Exactly! Hata mimi nimewahi kuona hilo tangazo. Ila ukienda kwa wakala, issue inakuwa simpler. Wanakuonesha weight wakati ikiwa empty na baada ya kujaza! Na kwenye mitungi kuna alama zinazoonesha uzito unaotakiwa in both cases!

hiyo mitungi inapoonyesha alama kwani mitungi iko transparents?
 
Back
Top Bottom