Elungata
JF-Expert Member
- Jan 28, 2011
- 40,205
- 33,226
Nimekuwa ni msomaji zaidi kuliko mchangiaji kwa muda mrefu lakini nimekuwa nikishangaa sana watu wanapokuwa wanaongea vitu wasivyovielewa ama kwa ushabiki au kwa kutokuelewa, mfano watu wameandika sana kuhusu uwezo wa Dr John Pombe magufuri kuwa anafaa kuwa rais wa jamhuri ya muungano watanzania kwa kutumia vigezo dhaifu sana kuwa kila anapopewa wizara hufanya vizuri nafikiri hicho si kigezo tosha kabisa cha mtu kuwa rais
Kwa wasio mjua Mh. magufuri nilitaka leo wamfahamu kwa ufupi tu kidogo ili na wao wapime kama kweli anafaa kuwa kiongozi wa nchi ktk nafasi kubwa km ya urais.
Magufuri ni mtu mwenye visasi sana na yu tayari kuumiza uma wa watu katika kulipa visasi kwa wasio mjua mh. magufuri alipata kugombea ubunge jimbo la biharamulo mara mbili bila kupita mara zote aliangushwa na kina marehemu phares Kabuye kwa kura nyingi sana ,aliweza kupata ubunge pale tu wilaya ya biharamulo ilipogawanywa majibo mawili yaani Biharamulo Magharibi na Biharamulo mashariki Hivyo akafanikiwa kuin gia bungeni kwa rushwa kubwa sana na kuwa mbunge wa Biharamulo mashariki wakati upande wa Biharamulo magharibi akiwa Mh. Choya.
Baada ya kupata ubunge Aliapa kiapo kama atahakikisha Biharamulo mashariki inakufa, kipindi hicho Magufuri alipata unaibu waziri hivyo alitumia nafasi hiyo kuivuruga Halmashauri ya Biharamulo na na kwa influence miradi yote mikubwa ya wilaya ikawa inaenda jimboni kwake moja kwa moja bila hata kupitia Halmashauri watu wote walitishwa makao makuu ya wilaya na hakuna aliyeweza kusema lolote kama manakumbuka vizuri alifikia kugombana na mbunge mwenzake wa mashariki aliyefikia kusema kama magufuri anatumia uwaziri wake kumhujumu jimboni mwake (kitendo kilicahomluudihi sana magufuri na kuhakikisha nakufanikisha Mh.Choya anadondoka ktk ubunge wa Biharamulo Magharibi. Alifikia kuwa analeta wageni wakitaifa direct jimboni kwake hata bila kupitia makao makuu ya wilaya lakini nia ikiwa ni kiapo alichokiweka kuwa lazima ataiua biharamulo Magharibi kwa kumnyima ubunge mara mbili hapa nataka kuwaonyesha kiongozi huyu mcheshi mchapa kazi lakini mwenye visasi vyenye kuleta maafa kwa wazee wanawake na watoto.
Je mtu huyu anaweza kuwa kiongozi wa umma?
Mwaka uliofuatia mheshimwa Magufuli alipita bila kupingwa baada mgombea mwingine aliyekuwa tishio kwake (jina nalihifadhi) kufanyiwa mizengwe wakati wa kurudisha form mpokea form alijificha na alijitokeza wakati mda wa kurudisha form umekwisha akaonekana mrudisha form amerudisha form too late lakini Mh. Magufuli alikuwa ameisha watisha viongozi wa chama na serikali wilayani biharamulo atakaepokea form za Bwana huyo basi yeye ni naibu waziri atahakikisha hana kazi watu wakatii na wakafanya dhuruma ya kumpitisha magufuri bila kupingwa.Je mtu huyu anaweza kuwa kiongozi wa umma?
Mwaka 2005 kijana mdogo anaitwa nahifadhi jina lake kupitia chama cha CUF ambaye alikuwa katibu wa wilaya wa CUF wilayani biharamulo alichukuwa form kugombea jimbo la biharamulo mashariki kwa magufuri huku akiwa na suport kubwa sana ya vijana na alikuwa anaenda kumwamgusha mh. Magufuli katika kinyanganyiro hicho, alichofanya Mh. Magufuli alimteka kijana huyo na kumpakia kwenye gari hadi mwanza kutoka mji mdogo wa Buseresere walimpelekea mke wa huyo bwana pesa wakampatia simu aongee na mme wake wakimshawishi waende hadi Mwanza wampatie pesa aondoe jina kwani pesa kidogo ya matumizi wameishamwachia mke wake yule bwana. Alipofika mwanza akapandishiwa dau hadi milioni 60 akubali kutorudisha form za ubunge ikiwa hapo imebaki siku 4 kabla form kurudishwa kijana akakabidhi form zake kwa Magufuli wakaenda nae hadi bank kijana kabaki kwenye bench mh. waziri akaingia ndani akatoka akamwambia account yake pale haina pesa waongozane hadi Dar es salaam. Wakapanda ndege hadi Dar kijana akafikishiwa kwenye 3 star hotel kwa bili ya mheshimiwa siku tatu bila kuonanana Mh. Magufuli.
Siku ya nne kijana anaona kwenye TV Magufuli amepita bila kupingwa akashtuka kaulizia hadi ofisini kwa waziri kafika akakaribishwa Mh. kama hamjui akamuuliza shida yako nini akasema nipe pesa zangu mh. akamwambia unakuja kuniomba rushwa nikuachie ubunge wewe kijana huna adabu kabisa. Mkifuatilia CUF, hiki kisa wanakijua vizuri kwani walipelekewa taarifa kama kuna mgombea wao ameenda kuuza ubunge kwa Magufuli ikabidi Green GUARD ya CUF iende kum-arrest na kumpeleka Buguruni makao makuu na kurudi Biharamulo kwa aibu kubwa lakini baadae alimtafutia kazi kwenye mgodi huko Tulawaka anafanya kazi kumziba mdomo kwa sababu kijana alikuwa ameapa kumfanyizia.
Huyu ndiye Magufuli, je anaweza kuwa kiongozi wa nchi katika uhuni wa namna hii?
Sinema ya Magufuli haiishi hapo; kile kiapo chake cha kulipa kisasi Biharamulo Magharibi kiliendelea alipolazimisha kupindisha barabara ya lami kuingia Chato toka Mwanza kwenda Bukoba kupitia Biharamulo makao makuu ya wilaya akaipindidhia Chato nyumbani kwake na kuua makao makuu ya wilaya ya Biharamulo.
Huyohuyo magufuli ndo anafaa,