Kwa wasiomjua Magufuli, Je, anafaa kuwa Rais?

Status
Not open for further replies.
Nimekuwa naamini kuwa kati ya dhambi kubwa marais wa Nchi hii wanafanya ni kutompa Magufuli uwaziri mkuu. Najua ana mapungufu mengi lakini ni mtu anayependa sana kupata sifa kwa kufanya jambo fulani la manufaa kwa wananchi, sio sifa za bure. Watanzania tuna tatizo la kutotekeleza majukumu yetu tusiposimamiwa kwa karibu. Na hicho Magufuli anaweza, kusimamia ishu mpaka akakukera! Na kiongozi wa namna hiyo ndio anahitajika Tizii. Naomba nisiwe mnafiki, asiposimama Slaa 2013, kura ntampa Magufuli au Lowasa (CCM) wakimsimamisha mmoja wao. Kinyume cha hapo ntapiga kura ya diwani na Mdee tu.

Hicho cha kukera ndicho watanzania hawakipendi,wanapenda kiongozi anayeweza cheka nao na kazi ikalala.kiukweli kiboko ya wavivu ktk hii nchi ni Dr Magufuli na kama akipata nafasi watapiga mbizi sana watanzania na hapo ndipo maendeleo yatapatikana
 
lol! hahahahah unarukaruka tu huku na kule bila kujibu maswali yangu. Mara natumia maneno yasiyo na staha, mara Magufuli anapendwa sana, yuko juu sana, anafuata sheria lakini huna hata mfano hai mmoja wa kuthibitisha unachoandika, bali unabwabwaja tu. Endelea kumpigia debe fisadi Magufuli labda atakukumbuka nawe akupe hata kacheo mahali utanue kwa raha zako.
nitaendelea kusimamia hilo,mkielezwa ukweli huwa mnakimbilia kwenye vyeo,elewa kuwa hampendi viongozi wanaofuata sheria hili lipo wazi na ndio maana kelele ni nyingi kwa Dr Magufuli na hii baada ya kusikia tetesi kuwa anaweza gombea,kwanini unamwogopa? kama ni mvivu wa kutenda kazi si uombe kutumika?
mimi sihitaji cheo kama nilivyokueleza mwanzo na kama unaona umeme kwako ni tatizo basi tuwasiliane,nitakuuzia solar kwa bei inayoendana na ubora,sio mnalalamika fake kila siku huku hamtaki kununua vitu vyenye ubora.we sogoa tu humu,wenzako wanasonga mbele na ndio maana tunamwomba Dr Magafuli agombee urais ili kupambana na nyie vijana watoa lawama mkisubili kazi toka serikalini.hivi ungezaliwa India ungemlalamikia nani? maana idadi ya watu haiendani na kazi zilizopo.
komaeni vijana,acheni kelele na lawama,Dr Magufuli akipewa nafasi na chama chake 2015 ndio atakuwa Rais wa nchi hii na atakomaa sana na wavivu wasiopenda sheria zichukue mkondo wake.
 
Magufuli ni fisadi tu na ushahidi wa ufisadi wake nimekuwekea hadharani lakini wewe unaendeleza kauli zako hewa "yuko juu sana" "anafuata sheria" na "anapendwa na wengi sana" bila uthibitisho wowote ule bali kubwabwaja. Hata kuukemea ufisadi uliokithiri Serikalini kumemshinda kwa sababu anajua yeye mwenyewe ni fisadi. Hafai kabisa huyu fisadi kuiongoza Tanzania.
 
Nimekuwa ni msomaji zaidi kuliko mchangiaji kwa muda mrefu lakini nimekuwa nikishangaa sana watu wanapokuwa wanaongea vitu wasivyovielewa ama kwa ushabiki au kwa kutokuelewa, mfano watu wameandika sana kuhusu uwezo wa Dr John Pombe magufuri kuwa anafaa kuwa rais wa jamhuri ya muungano watanzania kwa kutumia vigezo dhaifu sana kuwa kila anapopewa wizara hufanya vizuri nafikiri hicho si kigezo tosha kabisa cha mtu kuwa rais

Kwa wasio mjua Mh. magufuri nilitaka leo wamfahamu kwa ufupi tu kidogo ili na wao wapime kama kweli anafaa kuwa kiongozi wa nchi ktk nafasi kubwa km ya urais.

Magufuri ni mtu mwenye visasi sana na yu tayari kuumiza uma wa watu katika kulipa visasi kwa wasio mjua mh. magufuri alipata kugombea ubunge jimbo la biharamulo mara mbili bila kupita mara zote aliangushwa na kina marehemu phares Kabuye kwa kura nyingi sana ,aliweza kupata ubunge pale tu wilaya ya biharamulo ilipogawanywa majibo mawili yaani Biharamulo Magharibi na Biharamulo mashariki Hivyo akafanikiwa kuin gia bungeni kwa rushwa kubwa sana na kuwa mbunge wa Biharamulo mashariki wakati upande wa Biharamulo magharibi akiwa Mh. Choya.

Baada ya kupata ubunge Aliapa kiapo kama atahakikisha Biharamulo mashariki inakufa, kipindi hicho Magufuri alipata unaibu waziri hivyo alitumia nafasi hiyo kuivuruga Halmashauri ya Biharamulo na na kwa influence miradi yote mikubwa ya wilaya ikawa inaenda jimboni kwake moja kwa moja bila hata kupitia Halmashauri watu wote walitishwa makao makuu ya wilaya na hakuna aliyeweza kusema lolote kama manakumbuka vizuri alifikia kugombana na mbunge mwenzake wa mashariki aliyefikia kusema kama magufuri anatumia uwaziri wake kumhujumu jimboni mwake (kitendo kilicahomluudihi sana magufuri na kuhakikisha nakufanikisha Mh.Choya anadondoka ktk ubunge wa Biharamulo Magharibi. Alifikia kuwa analeta wageni wakitaifa direct jimboni kwake hata bila kupitia makao makuu ya wilaya lakini nia ikiwa ni kiapo alichokiweka kuwa lazima ataiua biharamulo Magharibi kwa kumnyima ubunge mara mbili hapa nataka kuwaonyesha kiongozi huyu mcheshi mchapa kazi lakini mwenye visasi vyenye kuleta maafa kwa wazee wanawake na watoto.

Je mtu huyu anaweza kuwa kiongozi wa umma?

Mwaka uliofuatia mheshimwa Magufuli alipita bila kupingwa baada mgombea mwingine aliyekuwa tishio kwake (jina nalihifadhi) kufanyiwa mizengwe wakati wa kurudisha form mpokea form alijificha na alijitokeza wakati mda wa kurudisha form umekwisha akaonekana mrudisha form amerudisha form too late lakini Mh. Magufuli alikuwa ameisha watisha viongozi wa chama na serikali wilayani biharamulo atakaepokea form za Bwana huyo basi yeye ni naibu waziri atahakikisha hana kazi watu wakatii na wakafanya dhuruma ya kumpitisha magufuri bila kupingwa.Je mtu huyu anaweza kuwa kiongozi wa umma?

Mwaka 2005 kijana mdogo anaitwa nahifadhi jina lake kupitia chama cha CUF ambaye alikuwa katibu wa wilaya wa CUF wilayani biharamulo alichukuwa form kugombea jimbo la biharamulo mashariki kwa magufuri huku akiwa na suport kubwa sana ya vijana na alikuwa anaenda kumwamgusha mh. Magufuli katika kinyanganyiro hicho, alichofanya Mh. Magufuli alimteka kijana huyo na kumpakia kwenye gari hadi mwanza kutoka mji mdogo wa Buseresere walimpelekea mke wa huyo bwana pesa wakampatia simu aongee na mme wake wakimshawishi waende hadi Mwanza wampatie pesa aondoe jina kwani pesa kidogo ya matumizi wameishamwachia mke wake yule bwana. Alipofika mwanza akapandishiwa dau hadi milioni 60 akubali kutorudisha form za ubunge ikiwa hapo imebaki siku 4 kabla form kurudishwa kijana akakabidhi form zake kwa Magufuli wakaenda nae hadi bank kijana kabaki kwenye bench mh. waziri akaingia ndani akatoka akamwambia account yake pale haina pesa waongozane hadi Dar es salaam. Wakapanda ndege hadi Dar kijana akafikishiwa kwenye 3 star hotel kwa bili ya mheshimiwa siku tatu bila kuonanana Mh. Magufuli.

Siku ya nne kijana anaona kwenye TV Magufuli amepita bila kupingwa akashtuka kaulizia hadi ofisini kwa waziri kafika akakaribishwa Mh. kama hamjui akamuuliza shida yako nini akasema nipe pesa zangu mh. akamwambia unakuja kuniomba rushwa nikuachie ubunge wewe kijana huna adabu kabisa. Mkifuatilia CUF, hiki kisa wanakijua vizuri kwani walipelekewa taarifa kama kuna mgombea wao ameenda kuuza ubunge kwa Magufuli ikabidi Green GUARD ya CUF iende kum-arrest na kumpeleka Buguruni makao makuu na kurudi Biharamulo kwa aibu kubwa lakini baadae alimtafutia kazi kwenye mgodi huko Tulawaka anafanya kazi kumziba mdomo kwa sababu kijana alikuwa ameapa kumfanyizia.

Huyu ndiye Magufuli, je anaweza kuwa kiongozi wa nchi katika uhuni wa namna hii?

Sinema ya Magufuli haiishi hapo; kile kiapo chake cha kulipa kisasi Biharamulo Magharibi kiliendelea alipolazimisha kupindisha barabara ya lami kuingia Chato toka Mwanza kwenda Bukoba kupitia Biharamulo makao makuu ya wilaya akaipindidhia Chato nyumbani kwake na kuua makao makuu ya wilaya ya Biharamulo. Huyu ndiye kiongozi anayeweza kuongoza watu?

Mh. Magufuli alipigana na kulobby kwa nguvu zote kuhakikisha Chato inakuwa wilaya ili Biharamulo Magharibi wasifaidi mapato ya ziwa ambalo yanapatikana upande wa Chato na Nyamirembe na ndiyo kilichokuwa chanzo kikuu cha mapato cha wilaya ya Biharamulo lengo ikiwa ni katika kuendelea kulipa visasi kwa nini upande wa magharibi walikuwa hawampi kura kwa mihura takribani miwili alifaulu na Chato ikawa wilaya mpya toka Biharamulo.

Alipojikuta amesahau kuwa mgodi wa Tulawaka upo Biharamulo na haupo Chato alianza kuharasi uongozi wa wilaya ya Biharamulo kuwa ule mrahaba wa mwisho wa mwaka unaotolewa na migodi kwenye halmashauri za wilaya migodi ilipo alitaka Biharamulo igawane nusu kwa nusu mrahaba wake na wilaya ya Chato. Huyu ndiye Mh. Magufuli, je rais anaweza kuwa na tabia hizi chafuchafu namna hii?

Iliposhindikana akiwa waziri wa ardhi Mh. magufuri kwa makusudi kabisa alibadilisha mawe ya mpaka kwa amri kama waziri wa ardhi kuiingiza Tulawaka ndani ya wilaya ya chato hivyo siku si nyingi chato itadai Tulawaka ipo kwao na watapola haki ya wana biharamulo swala hili lipo wazi kabisa halmashauri ya wilaya kupitia baraza la madiwani limelalamika sana kuhusu ushenzi huu wa magufuri huyu ndiyo mtu anaweza kuwa raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania?

Mwaka jana katika mpaka mwingine wa biharamulo na chato kijiji cha biharamulo kinachopakana na chato huko kata ya Runazi wanakijiji waligundua kuna dhahabu na kuna wachimbaji wadowadogo Mh. magufuri yupo analazimisha kubadili mipaka ili hiki kijiji kihamie wilayani chato na kumekuwa na mgogoro wa kiutawala unochochewa na yeye Huyu ndiyo Mh. Magufuli anaepigiwa debe humu ndani kama anaweza kuwa rais rais huangaliwa pande zote mafanikio na madhaifu kwangu mimi madhaifu ya magufuri ni mengi kuliko mafanikio mtakumbuka kilio cha nyumba za serikali lakini huyu jamaa mkumbuke ni bingwa wa kusimamia wakandarasi na kutaka viwango kktk ujenzi lakini yote tisa kumi mh. anajenga ghotofa pale kwake anapoishi Osterbay yeye nendeni mkaone maajabu ya mussa wajenzi mafundi mchundo hata ramani hazijapitishwa sababu wachoraji ni watu wa mitaani na mafundi ni ni vibaruwa mchundo huyu ndiyo Mh. Magufuli.

Lakini skendo kubwa ya huyu bwana ambayo waandishi wangefuatilia kumjua vizuri ni jinsi alivyochezea mipaka ya wilaya ya Biharamulo kubadilisha DN za vijiji na kusogezwa mawe yalioizinishwa na serikali bila hata serikali kujua kuzipeleka Chato hii ni hujuma kubwa na anastahili kujiuzulu waandishi nendeni mkawahoji wananchi na viongozi wa wilaya biharamulo mjue huyu mtu kitu alichofanya mtu namna hii hawezi kuwa kiongozi kabisa

Huko jimboni kwake wafanyakzi wa serikali wote walio against naye amewaumiza sana wengine hata kufunga vibiashara vyao vidogovidogo ili tu wakubaliane naye kifupi hajawahi kupita bila kupngwa ila amekuwa akipita kwa hila kubwa.

Naomba kuwakilisha ili tumpime kwa pamoja. Je, tabia hizi zinaweza kumpa urais kweli?

TUMPIME KWA PAMOJA HAYO NI MAONI YANGU TU

Mkuu nyuzi yako imejawa na hila zaidi. Kwani kuna mbunge gani ndani ya CCM ambaye hana hatia ya hayo uliyo mnenea Mh. Magufuri ?. Mimi nahisi umetumwa kumchafua ili kumsafishia njia aliyekutuma. Hizi ni mbinu za wagombea urais 2015 ndani ya chama tawala. Mimi siko hapa kumpigia debe Mh. Magufuri hata kidogo, lakin ni ukweli ulio wazi kuwa ukilinganisha na wengi ndani ya chama tawala udhaifu wake ni mdogo sana, na umesababishwa na mfumo uliopo ndani ya chama tawala. Dr.Magufuri ana mambo mengi ya kusifiwa kiutendaji pamoja na kuwa chini ya mfumo dhaifu wa kiuongozi.
 
This time tunataka kiongozi wa nchi atoke kanda ya ziwa hata mngemponda kwa propaganda zipo magufuli huyo ndiyo tumtakae. na hapo ndo tutawaonyesha how serious we are. mchague kimoja, magufuli kwa ccm au cdm kwa slaa. sorry for small letter. mchina at work.
 
Kwa suala la Magufuli tupo pamoja ila suala la Ndugai tunatofautiana,Ndugai hana msaada wowote kongwa
kweli jamaa yangu weqwe mlengo wa pembeni sasa hili ndio kosa la kumyang'anya Ubunge sasa mbadala wake mna uhakika atakuwa na Che o hicho aua hata uwaziri? au ni chuki.
Dodoma ni vigumu kuapata hizo nafasi hasa Kongwa
 
Magufuli anajua kucheza na vyombo vya habari hivi mjiulize kwanini mashine za kuuzia risiti pale fery pamoja na kununuliwa mpaka leo bado hazijaanza kutumika pia kila nikikatisha kwenye barabara ambazo zina manundu na kulinganisha na jinsi anavyojisia nasikia kichefuchefu
Na jinsi alivyosimamia zoezi la kuuza nyumba za serikali na kuwapa hadi ndugu zake na leo hii serikali bado inaweka watu hotelini kwa kukosa nyumba
Kuna mengi yanayomhusu kama kubomoa kituo cha mafuta mwanza na baadae mwenye kituo akalipwa fidia
 
Mimi binafsi ndan ya ccm nimebakiwa na iman na watu 3 tu. Magufuli, Lowassa, Mwakiembe. Najua kuna wanaoweza kunitilia mashaka kuhusu Lowassa, kile mimi ninachoweza kusema huyu naona ni siasa tu imetumika kumchafua ila ukwel anao uwezo wa kiutawala. Mwakiembe nae ni mtu mzuri mtendaji na ana msimamo, Magufuli nae kama mwakiembe. Mtu mwingine mzur ambaye ninahc amekaa mno kijamaa ni mzee Salim Ahmed Salim. Na jambo lingine ambalo nahc watanzania wengi hawajaliona ni kuwa nchi hii haitaji uwe umesoma sana ili uweze kutawala. Panaitajika mtu mwenye maono, msimamo, uthubutu na kufanya maamuz sahihi kwa wakati, bila kuacha elimu japo sio ile kubwa kiivyo, coz huitaji elimu kubwa kujua idara ya usalama wa taifa imegeuka kuwa idara ya usalama wa mafisadi. kuna jamaa yangu mmoja anauza cm mpaka za Tshs milion 150 per day lakn halipi hata mia serikalin unakuta anauzia store. Sasa ukiangalia hawa watu wa jinsi hii ndio idara yetu ya usalama ingetakiwa kuhakikisha wanakamatwa. Wao wanachojua nikutengeneza video feki et Lwakatare ni gaidi.
 
Kimsingi John Pombe hafai,kwa sababu ni mwoga mara zote hutenda kinyume na utashi wake kwa ajili ya chama na serikali,mapenzi makubwa aliyonayo kwa wananchi ni wakati wa kuomba kura kipindi cha uchaguzi,lakini baaada ya hapo mapenzi yake huamia kwenye serikali na chama.
 
Absolutely right!!! jamaa mbinafsi mkabila na mpenda kulipiza visasi hakika hii ni dhuluma aliyowafanyia wananchi wa Biharamulo na leo hii Biharamulo imekuwa ngome imara ya CHADEMA kama mtetezi wao
 
apana! mkulu mnamwonea tu ni maneno ya vijiwen hayo yasio na mana yoyote, uyo magufuli gamba tu ayo ni kweli hana mana, mwachen mkulu akastaafu kwa aman kafanya meng kwa vtendo amejitaid, kama ni mabest zake ata wewe ungekaa pale ungewabeba acha uzush

kweli wewe popobawa, mheshimiwa tunajua ninyi ndio mnaosabisha nchi hii iwe ya mafisadi wachache na magamba,hakuna maneno ya kijiweni hapo,nibora magufuli kisilani na anatenda kazi kulingana na nafasi alionayo,kuliko huyo umkulu ambaye anashindwa kutoa maamuzi hata kwenye vitu vidogovidogo tu,unasematumuache astafu kwa amani tmahakama ya kimataifa inamngoja labda serikari hii apewe membe.anamengi ya kujibu baada ya 2015.
 
shilingi siku zote huwa ina pande mbili.. siamini kama kuna binadam duniani ambaye ni mkamilifu kwa 100%, ni marehem tu ndiye ambaye husifiwa.. Jina lolote unalolijua kutoka chama chochote ukiliweka hapa wapo watakaokuelezea upande hasi na wapo watakaokuelezea upande chanya.. Huyo ndiye binadama hana tofauti na shilingi, siku zote ana pande mbili
 
shilingi siku zote huwa ina pande mbili.. siamini kama kuna binadam duniani ambaye ni mkamilifu kwa 100%, ni marehem tu ndiye ambaye husifiwa.. Jina lolote unalolijua kutoka chama chochote ukiliweka hapa wapo watakaokuelezea upande hasi na wapo watakaokuelezea upande chanya.. Huyo ndiye binadama hana tofauti na shilingi, siku zote ana pande mbili

Na upande wa pili ndio huo ambao jamaa anejitahidi kuuzima
 
Naona kijana povu limemtoka weee sasa kamaliza magufuli au lowassa mmoja wao ndio rais wa 2015:::::::::::tunafunga mjadala huo tumemaliza hilo.
 
kweli wewe popobawa, mheshimiwa tunajua ninyi ndio mnaosabisha nchi hii iwe ya mafisadi wachache na magamba,hakuna maneno ya kijiweni hapo,nibora magufuli kisilani na anatenda kazi kulingana na nafasi alionayo,kuliko huyo umkulu ambaye anashindwa kutoa maamuzi hata kwenye vitu vidogovidogo tu,unasematumuache astafu kwa amani tmahakama ya kimataifa inamngoja labda serikari hii apewe membe.anamengi ya kujibu baada ya 2015.

acha jazba wewe mzembe! kama ni the hugue alitakiwa aanze aliemtangulia mana yule ndo aliegeuza ikulu(mahali patakatifu) kua gulio, sasa uyo mkulu kakosa nini? kama kaz anafanya sote tunaona madhaifu madogomadogo kila mtu anayo ata wewe pengine ungekua mla rushwa na mtesi usie na mfano dunian kama ungekua pale magogoni.
kama kuna ishu challenging tumsaidie kwa mawazo mbadala na sio kulaan tu kila kitu utadhan toka aingie ameket anaponda raha hafany kaz achen chuki zisizo na sababu.
 
Bila kuathiri kanuni za JF, nashauri mtoa tuhuma hizi ajitokeze "Verified user" na kwakuwa shutuma hizi ni nzito aziweke hadharani katika vyombo husika vya kiuchunguzi na hapo atakuwa ameisaidia jamii kwa ujumla wake na atakuwa ni shujaa katika nchi yake.

Kumbuka akina Steven Biko, Nelson Mandela na wengine wengi katika old school walivyopigania haki kwa uwazi.

Vinginevyo kubaki kimya na tuhuma nzito kama hizi eti unazi post hapa JF ni uwoga, umajungu na ukuwadi.:shut-mouth:
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom