Kwa wasiomjua Magufuli, Je, anafaa kuwa Rais?

Status
Not open for further replies.
Yaani nawaonea huruma sana nyie mnao mtetea magufulii kwa kweli usilolijua ni sawa na usiku wa gizaa, kwa wale wachache wanaomjua vizuri magufuliii ( tangu akiwa "mission town" pale mitaa ya mwanza adi alipo ukwaa uheshimiwaa) hawawezi kukubali huyu jamaa agombee hata udiwanii kwa jinsi alivyo dictator, fisadi, opportunistic, tena wanahurumia sana wana chato ambao bado wamelala usingizi wa pono wakati huyu jamaa anawaleta akina Odinga na mwana falme wa.... kuja kumiliki ardhi na mashamba makubwa ya Chato na kuwakabidhi title deed za miaka isiyopungua 100 wakati wana chato hawana ata hati za kimila,

Anakataa boti zlizokuwa zinakuja mwanza zisipitishwe kwenye barabara ya Dar-Mwz, baada ya wiki moja anaruhusu Gyratory Crusher la Barrick liende Tulawaka, almost through the same route aliyoikataa boti zisipitishe ( wakati hiyo karasha uzito na ukubwa wake ni 5 zaidi ya viboti).

Muulizeni mpiganaji general Ulimwengu anavyo jua machungu aka kajamaa, yaani kanajua kweli kweli kuuma na kupulizia nyie jaribu kukapa.
 
Acha majungu na porojo wewe. Sisi tunaangalia nini alichofanya kwa taifa na siyo nini alichofanya Biharamuro. Inawezekana wewe umetumwa na mafisadi kuanza kumchafulia Mhe. Magufuli. Waambie waliokutuma kwamba tumekung'amua.

Kwa taarifa yako, hakuna mwanadamu aliyemsafi. Kinachotazamwa hapa ni uthubutu wa kiongozi kuchukua maamuzi makubwa na magumu kwa maslahi ya umma. Kwa sifa hiyo, niambie ni nani anayeweza ndani ya baraza la mawaziri la sasa, kama siyo Mhe. Magufuli?? Ebu tuondolee porojo zako humu jamvini zisizo na mashiko.
nashkuru cnalakuongeza...
 
Kamanda! Thank you. Ur speaking volumes.
 
Shukrani za dhati mkuu Burigi na wengine waliochangia hii mada huku ndani. Haya madudu ya Mh. Magufuli kwenye jimbo lake la uchaguzi na lile la awali ni kama trailer tu. Sinema yenyewe ipo katika wizara alizowahi kuongoza mpaka sasa. Scratch beneath the media whoring, utauona utendaji wake usio na dira, kufuata malengo ya muda mrefu na upindishaji wa kanuni mbalimbali. Tafuteni wakandarasi wa barabara waliojenga wakati wa awamu ya kwanza ya Magufuli wakueleze mlolongo wa malipo ya kazi zao umefikia wapi. Ni kinara wa kuweka saini mikataba bila ya kuwa na fedha za kuitekeleza, kwenye wizara ya ardhi madudu yake yaliumiza wengi sana.

Nilishamsema toka awali huyu bwana ni mzuri wa kutengeneza PR ila ufanisi wa utendaji wake wa kazi leaves a lot to be desired
 
Huyu Mh. Sasa hivi anampango wa kuhalalisha baadhi ya visiwa vya wavuvi vilivyopo Geita na Sengerema kumilikiwa na halimashauri ya Chato. Kwa vile visiwa hivi vinaingiza mapato mengi sana kwa halmashauri husika. Huyu Mh. hatukatai kuwa hanamatendo maovu bali tunasema ni mtu ambaye anakula na kukumbuka wananchi wanyonge kwa kuwapa haki yao. Mimi ni wa maeneo hayo hayo nafahamu mambo haya yote ni ya ukweli mtupu.
 
Nakumbuka kuna mwaka tulimuona Lyatonga Mrema kama mkombozi wetu. Tukampamba, tukasukuma gari lake na wale wote waliotuambia, chonde chonde, tuliwaona wasaliti. Leo hatutaki hata kusikia jina lake na baadhi tunashukuru hakushinda ule uchaguzi ingawa tulimpigia kura!
Baadae, tukamfanyia hivyo hivyo rais wetu wa sasa. Tukamsifia na kumtungia ngojera. Kwa mara ya kwanza wamisheni na wenye misikiti wakaona wamepata mkombozi. Vile vile walikuwepo waliotuasi twende taratibu lakini kama kawaida yetu tukawaona wasaliti na wasioitakia mema nchi yetu. Leo hatutaki kumsikia mtu akimsifia.

Lakini kama kawaida yetu ya kupenda majibu mepesi na kutafuta mwenye silva bulet kwa ajili ya matatizo yetu, watu mmeanza kututangazia mamasia watakaotukumboa ( Magufuli, Mwandosya n.k.). Na kama sikio la kufa hamtaki kusikia criticism yeyote juu ya wapendwa wenu. Atakayediriki kufanya hivyo, mnamuandama kwa kejeli na hata matusi.

Tukumbuke kuwa tunayempendekeza ndiye atakayekuwa na jukumu la kutuongoza kwa miaka mitano kwa hiyo tuna haki ya kumpima kwa kila namna. Badala ya kukejeli wanaotoa shutuma dhidi yao, tuzipime na kuzichunguza na zikionekana hazistahili hapo ndipo tuziweke pembeni. Lakini si kabla ya hapo. Kwa mfano kuna shutuma hapa kuwa Mheshimiwa huyu alipindisha barabara kwa sababu zake binafsi na kuipitisha kwenye jimbo lake. Hii kweli tutashindwa kupata ukweli wake? Barabara si ipo? Watu wanaoishi sehemu hizo si wapo? Kama ni majungu kwa nini tusiwaumbue kwa kuwaonyesha ukweli ulivyo?

Amandla......
 
Ni muhimu kupata taarifa kama hizi kwa watu wanaofikiriwa kuwa viongozi wetu, na si vizuri kuwakatisha tamaa wanaotoa taarifa hizi na kuwapa watu fulani utakatifu wakati pengine hawana.

Nakumbuka mwaka 2005 watu walivyokuwa wamepagawa kwenye forum ya uchaguzi.com (kama JF ya leo), ulikuwa huwezi kusema neno lolote watu wakaelewa na ulikuwa unaitwa majina yote ya usaliti hapa duniani ukimkosoa mgombea wao kipenzi. Niliandika makala kuhusu sababu 15 kwa nini CCM wamteue SAL-ngumi, mateke na matusi niliyopata kutoka kwa wana uchaguzi.com siwezi kusahau, na leo ndiyo hao wanaoongoza kumpiga mawe aliyekuwa mgombea wao kipenzi.

Sasa tusirudie kosa tulilofanya mwaka 2005 kwa kuendekeza ushabiki wa kijinga na kudharau watu wanaotupatia taarifa za upande wa pili wa wale wanaotaka kuwa viongozi wetu. Huu sio muda wa ushabiki na ubazaza usio na mantiki.

Lazima kila kiongozi tumpime vya kutosha na lazima tugeuze kila jiwe.

Kweli kabisa...ili kuweza kujenga watu wajadili kwa hoja, huku wakichunguza kwa umakini yote yanayotolewa...kushabikia tu ni hatari sana..tunayashuhudia madhara ya kushabikia bila kufanya tathmini ya kina yanavyodumu.....'Majuto Mjukuu'.
 
Acha majungu na porojo wewe. Sisi tunaangalia nini alichofanya kwa taifa na siyo nini alichofanya Biharamuro. Inawezekana wewe umetumwa na mafisadi kuanza kumchafulia Mhe. Magufuli. Waambie waliokutuma kwamba tumekung'amua.

Kwa taarifa yako, hakuna mwanadamu aliyemsafi. Kinachotazamwa hapa ni uthubutu wa kiongozi kuchukua maamuzi makubwa na magumu kwa maslahi ya umma. Kwa sifa hiyo, niambie ni nani anayeweza ndani ya baraza la mawaziri la sasa, kama siyo Mhe. Magufuli?? Ebu tuondolee porojo zako humu jamvini zisizo na mashiko.

Bwana Gosbert Gudluck Jenga hoja kumsafisha Magufuli wako kwa evidence usisipige kelele. Argue don't shout.
 
Mi nafikiri kuna haja ya kufanya uchunguzi juu ya tuhuma hizi.
Inawezakana kabisa kweli huyu ndo Pombe, let us wait watafiti wafanye kazi yao.
Imenishitua sana maana anavyochukuliwa katika jamii ya watz ni tofauti kabisa.
Kuna mwenye kujua kuna madiwani wangapi wa CCM huko Chato???
 
uMSEMA VYEMA... HAPO KWENYE RED PATAMU SANA

HIVI TUJIULIZE KWELI, HIVI MAGUFULI KAMA NI MBAYA HIVI... CCM INASIMAMAJE CHATO?? Kwa waliohudhuria msiba wa binti yake watasema kama magufuli anapendwa au hapendwi chato
 
Kitila, Thanks for sharing your experience na pia kwa angalizo...

Burigi ana rights za kutoa maoni yake na mtazamo wake kama tulivyo wengi ndani ya JF.... lakini nachelea kusema kwamba the guy is biased.

Nimeona kama vile ameamua kuwa m-biharamulo peke yake na kutuacha watanzania wengine wote ambao tumefaidika na Magufuli. Pia nadhani ni vyema kukubali kwamba hakuna kiongozi yoyote asiye na kasoro na kibaya zaidi hajawahi kutokea kiongozi yoyote duniani ambaye hana visasi, kwani kisasi ni nini?? ina definition lakini wengu wetu hutumia baadhi ya maneno kufikisha ujumbe tu.

Mimi na wewe tuna visasi na watu wasiopenda maendeleo au kufanya kazi; mimi nina visasi na watu wanaodhani ati watanimaliza tu simply because i differ with them, siwezi kuwa mnafiki niseme sina visasi wakati najua wakinikama watanimaliza.... NADHANI UMENISOMA MAANA YA "VISASI" NILIVYOITUMIA HAPO

Magufuli is way beyond comperation na watu kama Mrema, JK nk... najua ana kashfa zake kama ile ya Sundi Malomo, yule shemeji wa Bujiku na hata ya pesa na nk... hizo ni kashafa, kwangu hazijathibitika na siwezi kumuondoa kwenye top list kwani siwezi kumlingalisha na lowassa, mwandosya, rostam, mkuchika, kinana, nchimbi, makamba, Jk nk

Burigi anasahau kwamba anakanyaga kila kilomita kwenda kwao biharamulo kwa faida yake na tunada ma magufuli, ni burigi huyuhuyu anashindwa kuelewa kwamba huyo magufuli ameacha positive impact kila alipopita na hasa kwenye kudai na kutetea haki na sheria kufuata mkondo wake.

Kwa sisi tunaoishi kimbiji, zile sleepless nights zimerudi na wavuvi harmu tuna wasiwasi wanatumia mabomu ambayo hata wanajeshi hawana (makubwa sana) ... ni wkasababu ile wizara ya vitoweo, imerudia kuwa wizara ya vitoeo... na utaona tutakavyokwisha sasa

Sijui nisemeje au niiweke vipi post yangu, lakini nasikitika sana burigi ameamua kutulazimisha tumjue magufuli kwa kupitia biharamulo pekee wakati yeye magufuli hatumii hata 5% ya muda wake huko

Hilo la kusema anakuja na wageni hapiti wilayani, nasema inategemea purpose ya visit, kama ni ya kiserikali au kisiasa... TUSILAZIMISHE WATU WAFANYE TUTAKAVYO ILI NA SISI TUWE WA MAANA

TO ME BURIGI IS A TYPICAL TANZANIAN, GOOD IN DEFAMING PEOPLE, FOR A FEW COINS AND VERY BAD IN PERFORMING HER/HIS DUTIES

THIS THREAD ONCE AGAIN HAS UNEARTHED TYPICAL WA-TZ... KUSEMANA SEMANA KAMA WATU (AS INDIVIDUALS) BADALA YA KUWA GREAT MINDS KUDISCUSS ISSUES

SHAME ON BURIGI AND SHAME ON US WHO ALWAYS WISH TO DISCUSS PEOPLE INSTEAD OF ISSUES

MTM umetulia sana leo! Good analysis broda lazima hapa nikupe Tots kadhaa za blue label. Tunashida kubwa sana sisi ya kufata mikumbo, kuna sehemu mchangiaji ameandika sijui alichukua mke wa mtu jina kapuni ....Kweli jamani? Mtu akikuchua mkeo wewe ni dhaifu jamani tuache fitina. Tuangalie mazuri Tanzania ni zaidi ya Biharamulo na Chato
 
MTM umetulia sana leo! Good analysis broda lazima hapa nikupe Tots kadhaa za blue label. Tunashida kubwa sana sisi ya kufata mikumbo, kuna sehemu mchangiaji ameandika sijui alichukua mke wa mtu jina kapuni ....Kweli jamani? Mtu akikuchua mkeo wewe ni dhaifu jamani tuache fitina. Tuangalie mazuri Tanzania ni zaidi ya Biharamulo.
Wabongo tupo kimajungu zaidi.... hatuangaliii overall impact ya mtu kwa taifa

Tunakumbuka akina Mao, Akina Lincoln, Mandela mwenye (mzee wa totoz), hata Ben, Clinton nk hao wote walikua na personal life ambayo kama ingeangaliwa pekee basi wasingeweza kufika walipofika.

Mtu na akili timamu anataka kuchagua baya basi akomae nalo tena si ajabu kwa dola mia tatu tu; yale akina sheikh mtopea... to me Burigi is a hypocrite na unaweza kukuta kesho anampokea begi magufuli na kujifanya anamjua sana

We need a leader, visionary and results driven like Pombe kuliko kiongozi wa kufurahisha watu wakati taifa liko below sea level
 
Mi nafikiri kuna haja ya kufanya uchunguzi juu ya tuhuma hizi.
Inawezakana kabisa kweli huyu ndo Pombe, let us wait watafiti wafanye kazi yao.
Imenishitua sana maana anavyochukuliwa katika jamii ya watz ni tofauti kabisa.
Kuna mwenye kujua kuna madiwani wangapi wa CCM huko Chato???

Hizi ni mbinu za wanaotafuta urais 2015 kupitia CCM. Hawa jamaa wako kazini tayari wanaJF kaeni macho wanatutumia kuwapa umaarufu. Narudia CCM hatuwataki Tanzania bara, tumechoka.
 
mimi binafsi nisingependelea kumjadili mtu yeyote kutoka ccm kuja kushika nchi hiii tena tuwe na muda na mawazo yetu yote tuwaangalie chadema na kujiuliza baada ya slaa atakuwa nani? Lakini tukiwa na muda wa kuwatafakali wazee wa ccm sioni kama ni sahihi wandugu chama kimesha poteza dira kuna sababu gani ya kujadili maswala yao wakati miaka mitano ijayo tunamtarajia raisi kutoka kwenye chama makini, habari za magufuri tupeni kapuni na kwa sababu tumeshajua kuwa afai basi tutakapo shika nchi hii tutamshughulikia kwa mujibu wa sheria kwa vitu alivyo vifanya kama atakuwepo lakini kwa sasa hivi utakuwa unatwanga maji kwenye kinu,
 
akihamia chadema atakua anafaa??
 
This is boorish and irrevant! Inahusiana nini na Magufuli hii kitu. Usiwe bendera kufata upepo. Huwezi linganisha uchapa kazi wa Lowassa na Mkwere, sifa mbaya ya Lowassa ni ufisadi. Ila yule anadhubutu. Mengine hayo yako

...sjakwelewa mkuu, "boorish and irrevant" ndo unamanisha nin? Sjakwelewa pia, kwamba UNAMKUBALI EL na ufisadi wake kwa kuwa mchapakaz??
 
akipewa wizara anaangalia wadhaifu ili kuwasulubu na kupata sifa ok waccm ni waccm tu kama ilivyo wa moja havai mbili....wote naona walewale tu....msinitie hasira.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom