Kwa wasiomjua Magufuli, Je, anafaa kuwa Rais?

Status
Not open for further replies.
Acha majungu na porojo wewe. Sisi tunaangalia nini alichofanya kwa taifa na siyo nini alichofanya Biharamuro. Inawezekana wewe umetumwa na mafisadi kuanza kumchafulia Mhe. Magufuli. Waambie waliokutuma kwamba tumekung'amua.

Kwa taarifa yako, hakuna mwanadamu aliyemsafi. Kinachotazamwa hapa ni uthubutu wa kiongozi kuchukua maamuzi makubwa na magumu kwa maslahi ya umma. Kwa sifa hiyo, niambie ni nani anayeweza ndani ya baraza la mawaziri la sasa, kama siyo Mhe. Magufuli?? Ebu tuondolee porojo zako humu jamvini zisizo na mashiko.

kaka acha jazba huyo magufuri unayemuona wewe kuwa ni malaika ndiye huyo aliyemnadi jk jimboni kwake kuwa ni kiongozi safi,..we unaamini hivyo??na angekuwa anafaa asingekuwa ccm,..trust me when i say,hakuna msafi ccm,huyu magufuli si ndo aliyejiuzia nyumba ya serikali pale o'bay na kuweka lami barabar iendayo nyumbani kwake,..kikwete mlimuona hivyo hivyo
 
Hivi kuna walaka wa Watanzania unaosema Magufuli ni Rais 2015???????? Nashauri tusijadili swala hili. Tuzungumzie ukame unaokuja, vita dhidi ya ufisadi, njaa, elimu duni nchini n.k.
 
Mgombea mzuri kwa 2015 ni yule atakayetoka nje kabisa ya CCM. Akishachaguliwa abadili KATIBA apate mawaziri nje ya BUNGE. Maghufuli anatembea na Tv mgongoni kwa malengo haya mnayoyajadili. Ni mtaalamu sana wa kutengeneza "shouting headlines" kwenye vyombo vya habari.
 
Mr. Burigi napenda nikushukuru kwa maelezo yako mazuri,
Wiki nzima nilikua chato kwa ajili ya kazi ya shirika nilibahatika kuongea na watu kadhaa kuhusu magufuli kwa kweli ulichokisema nami ndio nilichokipata
Ni bingwa wa kuongeza mipaka hasa akiona kuna rasilimali sehemu ya Biharamulo kwa mfano kata ya Kanazi kuna hifadhi ya taifa ilikua biharamulo kwa ubabe wake akaongeza mpaka na kuiweka iwe upande wa chato
Pia alishajenga kanisa kiubabe bila kushirkisha uongozi wa kanisa la katoriki waumini wamemgomea kulitumia lile jengo saiz lipo kama gofu

Kwa hali ya kisiasa mwaka 2015 nafikiri chato wanaweza wakamkoa ktk ubunge wake
Nafikiri watu wote tujadili hoja zilizotolewa.
 
Kwa mtazamo wangu, kama utampima kwenye mizani, basi positive side yake itaishinda ile negative side. Naamini anaweza kuwa Rais mzuri kama ataingia madarakani bila kupitia mgongo wa chama chochote cha siasa (mgombea binafsi). Katiba inayobana mamlaka ya Rais ndio jibu la mapungufu ulioyaelezea (Kama kweli yapo).
 
Magufuli anafaa sana kwa kazi za kutumwa, ila kwa maoni yangu hawezi kuwa rais mzuri. He is too photogenic!
 
Haya maelezo ya kupikika bila vielelezo huwa ni majungu! btw mbona unajichanganya marav Mh Magufuli anataka Biharamulo Mashariki ife mara Biharamulo Magaharibi ife! hueleweki inaonyesha usivyo makini
 
Sipingi madai ya Burigi na wala siwezi kuthibitisha Magufuli ni binadamu kama binadamu mwingine na zaidi ni mwanasiasa kama walivyowanasiasa wengine ni waroho wa madaraka na wagumu kukubali kuachia madaraka yao, lakini moja kubwa ambalo nakubaliana na Burigi ni kuwa Magufuli is not a Presidential Figure! licha ya uchapakazi wake, historia inaonesha watendaji wazuri hasa katika eneo dogo ( like wizara) kama magufuli huwa hawahwezi ku deliver Good deeds wanapopewa eneo kubwa zaidi la kiutendaji, mfano mzuri ni Mheshiwa Keenja alifanya vizuri sana alipokuwa Mkurugenzi wa jiji, lakini aliboronga vibaya alipopewa wizara ya Chakula, the same applied to A.L Mrema, so nafikiri The far magufuli can go katika safari yake ya uongozi wa kisiasa ni Uwaziri Mkuu na sio Urais, yaani huko ataboronga mbaya!
 
Haya sasa,...with 2015 around the corner, agents at work!
Kwangu mimi hii ni Vita ya panzi.


Mkuu umelongaa.... Kazi ndio imeeanza sasa......twende kazi....kuna nafasi ukiwa unaonekana kama unafaa au unaitamani hivi hasa nafasi ya juu kama presidaa wa country......vita itakuwa ni kali sana na wale ambao nao wanaitamani ni wazi hii ni kambi mojawapo imeshaaanza kazi ya kumchafua mtu ....subiri sasa tutasikia mengi kwa kila anayefikiriwa kuwa ana faa....Je muheshimiwa pombe yeye hajawahi kuiba mke wa Mtu? Hajawahi kubaka? Hana nyumba ndogo au kama zipo zipo ngapi? Sio mdini huyu? ....twende.....kazi :msela:
 
Naona ni mkakati endelevu, wamemaliza kupanga safu zao bungeni sasa waendelea na hatua nyingine. Baada ya Magufuli atafuatia nani mwingine ambaye mnamuona ni tishio? Nikulize kwani ule mkakati wa samaki haukufanya vizuri?
 
Try to think before you make your conclusion.

Wewe ulijua baya gani la JK kabla hajaboronga akiwa raisi?? Si ndio nyie mllikuwa mnamsifia wakati wa kampeni 2005 kuwa eti rais kijana sijui mchapakazi sasa yako wako?? Mh! fatilia aliyoandika Burigi uone kama hayana ukweli. Mtu anatoa kiapo kuwa wana Biharamulo Magh. watakiona kwa sababu walimnyima kula na kweli anatimiza kiapo chake lakini mijitu inaona kwamba that's no concern! Hebu tujenge utamaduni wa kuchulia mambo serious before we conclude on such matters. (kifupi heshima yangu kwako inaanza kushuka)

JK hakujulikana kwa mabaya 2005, lakini pia hakuwa na rekodi ya kujivunia ktk utendaji ktk wizara zote alizofanya kazi, tofauti na Magufuli! Tulimpenda sana kikwete coz ni mpole,mkarimu, full tabasamu, tofauti na ndugu mkapa!
 
Sipingi madai ya Burigi na wala siwezi kuthibitisha Magufuli ni binadamu kama binadamu mwingine na zaidi ni mwanasiasa kama walivyowanasiasa wengine ni waroho wa madaraka na wagumu kukubali kuachia madaraka yao, lakini moja kubwa ambalo nakubaliana na Burigi ni kuwa Magufuli is not a Presidential Figure! licha ya uchapakazi wake, historia inaonesha watendaji wazuri hasa katika eneo dogo ( like wizara) kama magufuli huwa hawahwezi ku deliver Good deeds wanapopewa eneo kubwa zaidi la kiutendaji, mfano mzuri ni Mheshiwa Keenja alifanya vizuri sana alipokuwa Mkurugenzi wa jiji, lakini aliboronga vibaya alipopewa wizara ya Chakula, the same applied to A.L Mrema, so nafikiri The far magufuli can go katika safari yake ya uongozi wa kisiasa ni Uwaziri Mkuu na sio Urais, yaani huko ataboronga mbaya!

Sasa huu ni utabiri, umejuaje Magufuli atashindwa na wengine wataweza?

Vipi mgombea ajaye hatatoka katika mawaziri wa sasa nini???

Ni vyema tukatoa sababu za yeye kutofaa kuliko kusema eti huyu hawezi kumudu uwaziri!

Ni bora tupime uwezo wake na ndiyo maana hii Thread imeanzishwa. Pima uwezo wake kwa matendo mabaya na mazuri si hisia?



 
Try to think before you make your conclusion.

Wewe ulijua baya gani la JK kabla hajaboronga akiwa raisi?? Si ndio nyie mllikuwa mnamsifia wakati wa kampeni 2005 kuwa eti rais kijana sijui mchapakazi sasa yako wako?? Mh! fatilia aliyoandika Burigi uone kama hayana ukweli. Mtu anatoa kiapo kuwa wana Biharamulo Magh. watakiona kwa sababu walimnyima kula na kweli anatimiza kiapo chake lakini mijitu inaona kwamba that's no concern! Hebu tujenge utamaduni wa kuchulia mambo serious before we conclude on such matters. (kifupi heshima yangu kwako inaanza kushuka)

Xuma

Kikwete anajulikana na wengi sarakasi zake tangia akiwa Tanga School, Kibaha Secondary, Chuo Kikuu ulizia aliyokuwa akifanya Hostel 3. Alipokuwa anagawa kadi za TANU mikoa ya kusini, Alipoenda Monduli, Mbunge wa Chalinze, Naibu waziri na waziri wa Fedha na hata alipokuwa waziri wa mambo ya nje. Hajawahi kuwa makini hata siku moja, ni mizaha kwenda mbele. Kama ulikuwa mkubwa baba wa taifa alisema huyu hajakuwa aliimanisha hawezi kukua. Nina kuhakikishia Nyerere angekuwa hai Kikwete asingekuwa raisi wa Tanzania. Alitumia propaganda na vyombo vya habari watu mkadanganyika kuwa anafaa kuwa raisi. Sisi wengine tulijua nini kitafuata.

Chunga kauli zako mimi ni miongoni tulikuwa tunampinga Kikwete kwa nguvu zote, kwa faida yako rais wangu mimi alikuwa ni Salim A Salim. Burigi ni mzushi tu ninafahamiana na Magufuli at a personal nitamtetea daima. Hapendi Nonsense huyo tofauti na wana CCM walio wengi kufata mkumbo kama kuna makosa basi angalieni na mazuri yake. Ni mfumo wa KiCCM unafanya hata wale wazuri waonekane ni wabaya ila kwa Pombe wazee haki yake mpeni.

Xuma sihitaji heshima yako wala siitafuti.
 
Xuma

Kikwete anajulikana na wengi sarakasi zake tangia akiwa Tanga School, Kibaha Secondary, Chuo Kikuu ulizia aliyokuwa akifanya Hostel 3. Alipokuwa anagawa kadi za TANU mikoa ya kusini, Alipoenda Monduli, Mbunge wa Chalinze, Naibu waziri na waziri wa Fedha na hata alipokuwa waziri wa mambo ya nje. Hajwahi kuwa makini hata siku moja, ni mizaha kwenda mbele. Kama ulikuwa mkubwa baba wa taifa alisema huyu hajakuwa aliimanisha hawezi kukua. Nina kuhakikishia Nyerere angekuwa hai Kikwete asingekuwa raisi wa Tanzania. Alitumia propaganda na vyombo vya habari watu makadanganyika kuwa anafaa kuwa raisi. Sisi wengine tulijua nini kitafuata. Chunga kauli zako mimi ni miongoni tulikuwa tunampinga Kikwete kwa nguvu zote, kwa faida yako rais wangu mimi alikuwa ni Salim A Salim. Burigi ni mzushi tu ninafahamiana na Magufuli at a personal nitamtetea daima. hapendi Nonsense huyo tofauti na wana CCM walio wengi kama kuna makosa basi angalieni na mazuri yake. Ni mfumo wa KiCCM unafanya hata wale wazuri waonekane ni wabaya ila kwa Pombe wazee haki yake mpeni.

Xuma sihitaji heshima yako wala siitafuti.

Hapo Nyekundu,CRAP!
 
Kwanza nshakupa Thanks kwa kuwakilisha, in short hakuna mtu anayeijua ccm kama ccm wenyewe, sasa Sophia Simba alishasema wote wameoza Magufuli included, lakini Mr Pombe ni angalau kuliko wengine wote, unaona anateuliwa mtu kama pinda unasema huyu atakuwa afadhali kuliko hawa wengine kumbe hana manufaa yeyote ni msanii tuu, tunataka kiongozi anayetenda na ukimuona unajua anamaanisha anachokisema. Wote hawafai ila yeye ana unafuu, hebu angalia inafikia stage watu wanamkumbuka lowassa kwa utendaji kazi wake wanasahau kitu muhimu kwamba yeye ni fisadi wa kutupwa! Bora Magufuli kazi anafanya na inaonekana ingawa my take angefaa zaidi kuwa waziri mkuu kuliko kuwa Rais.

Wabongo bana, ati afadhali huyu kuliko wengine, kapewa ubunge na uwazir tu, kavuruga mahusiano ya jamii mbil zlizokua moja. Akipewa UraHis, au uPM si atatugeuza KOREA kusini na kaskazin?

Kwa wasoma biblia(anayoisoma makufuli), wanasema ukishindwa kuwa mwaminifu kwa kidogo, hata kikubwa hupaswi kupewa... Na anajua imani yake inamtaka ajue hilo.
 
Mi nahisi mwanaJF mwenzangu bado upo usingizin kwa hayo mawazo mgando na fikra za kale ulizonazo.Hatuwezi kuwa na kiongoz wa nchi eti anaongoza wizara kwa style fulani hiv.In addition mh.makufuli aliwahi kupora mke wa fundi TV(jina kapun) mbeya na kumfanya kimada,alipokuwa wa waziri wa ardhi na alimpatia makazi kwenye nyumba zilizoachwa na wagen waliokuja kwa ajili ya mradi wa maji maeneo ya RRM.Je ni rais gan anayeingilia ndoa za watu?angekuwa mkeo ungetulia eti kwasababu ni kiongoz pekee aliyebak ccm?Unaikumbuk familia ya kina papii?Rais ni yule mwenye kujali utu na mzalendo na si tu kwa kuchapa kaz kwenye wizara fulani.Funguken mhubiri na rev.masanilo msiwe mashabik tu.

Hii ni crap ukiona mtu anaanza kuangalia nani kalala na nani ujue huyo kaishiwa. Tukienda hivyo hakuna atakaye simama. Nadhani unanielewa. Binafsi ninaangalia utendaji, hizi porojo za jina kapuni baki nazo. Mkuu unafikiria kweli wewe mbona unaandika makapi hapa? usifate mkumbo kijana.
 
You might be 100% right or 100% wrong but that's not important issue right now. Nadhani ni vizuri kujikita kwenye matatizo ya nchi hii ambayo yameipeleka nchi yetu ICU badala ya kila wakati kuwaza madaraka na uchaguzi tu

Wewe umeongea cha maana si wale jamaa wanadai eti kapora mke wa mtu jina kapuni lol!
 
Nimekuwa ni msomaji zaidi kuliko mchangiaji kwa muda mrefu lakini nimekuwa nikishangaa sana watu wanapokuwa wanaongea vitu wasivyovielewa ama kwa ushabiki au kwa kutokuelewa, mfano watu wameandika sana kuhusu uwezo wa Dr John Pombe magufuri kuwa anafaa kuwa rais wa jamhuri ya muungano watanzania kwa kutumia vigezo dhaifu sana kuwa kila anapopewa wizara hufanya vizuri nafikiri hicho si kigezo tosha kabisa cha mtu kuwa rais

Kwa wasio mjua Mh. magufuri nilitaka leo wamfahamu kwa ufupi tu kidogo ili na wao wapime kama kweli anafaa kuwa kiongozi wa nchi ktk nafasi kubwa km ya urais.

Magufuri ni mtu mwenye visasi sana na yu tayari kuumiza uma wa watu katika kulipa visasi kwa wasio mjua mh. magufuri alipata kugombea ubunge jimbo la biharamulo mara mbili bila kupita mara zote aliangushwa na kina marehemu phares Kabuye kwa kura nyingi sana ,aliweza kupata ubunge pale tu wilaya ya biharamulo ilipogawanywa majibo mawili yaani Biharamulo Magharibi na Biharamulo mashariki Hivyo akafanikiwa kuin gia bungeni kwa rushwa kubwa sana na kuwa mbunge wa Biharamulo mashariki wakati upande wa Biharamulo magharibi akiwa Mh. Choya.

Baada ya kupata ubunge Aliapa kiapo kama atahakikisha Biharamulo mashariki inakufa, kipindi hicho Magufuri alipata unaibu waziri hivyo alitumia nafasi hiyo kuivuruga Halmashauri ya Biharamulo na na kwa influence miradi yote mikubwa ya wilaya ikawa inaenda jimboni kwake moja kwa moja bila hata kupitia Halmashauri watu wote walitishwa makao makuu ya wilaya na hakuna aliyeweza kusema lolote kama manakumbuka vizuri alifikia kugombana na mbunge mwenzake wa mashariki aliyefikia kusema kama magufuri anatumia uwaziri wake kumhujumu jimboni mwake (kitendo kilicahomluudihi sana magufuri na kuhakikisha nakufanikisha Mh.Choya anadondoka ktk ubunge wa Biharamulo Magharibi. Alifikia kuwa analeta wageni wakitaifa direct jimboni kwake hata bila kupitia makao makuu ya wilaya lakini nia ikiwa ni kiapo alichokiweka kuwa lazima ataiua biharamulo Magharibi kwa kumnyima ubunge mara mbili hapa nataka kuwaonyesha kiongozi huyu mcheshi mchapa kazi lakini mwenye visasi vyenye kuleta maafa kwa wazee wanawake na watoto.

Je mtu huyu anaweza kuwa kiongozi wa umma?

Mwaka uliofuatia mheshimwa Magufuli alipita bila kupingwa baada mgombea mwingine aliyekuwa tishio kwake (jina nalihifadhi) kufanyiwa mizengwe wakati wa kurudisha form mpokea form alijificha na alijitokeza wakati mda wa kurudisha form umekwisha akaonekana mrudisha form amerudisha form too late lakini Mh. Magufuli alikuwa ameisha watisha viongozi wa chama na serikali wilayani biharamulo atakaepokea form za Bwana huyo basi yeye ni naibu waziri atahakikisha hana kazi watu wakatii na wakafanya dhuruma ya kumpitisha magufuri bila kupingwa.Je mtu huyu anaweza kuwa kiongozi wa umma?

Mwaka 2005 kijana mdogo anaitwa nahifadhi jina lake kupitia chama cha CUF ambaye alikuwa katibu wa wilaya wa CUF wilayani biharamulo alichukuwa form kugombea jimbo la biharamulo mashariki kwa magufuri huku akiwa na suport kubwa sana ya vijana na alikuwa anaenda kumwamgusha mh. Magufuli katika kinyanganyiro hicho, alichofanya Mh. Magufuli alimteka kijana huyo na kumpakia kwenye gari hadi mwanza kutoka mji mdogo wa Buseresere walimpelekea mke wa huyo bwana pesa wakampatia simu aongee na mme wake wakimshawishi waende hadi Mwanza wampatie pesa aondoe jina kwani pesa kidogo ya matumizi wameishamwachia mke wake yule bwana. Alipofika mwanza akapandishiwa dau hadi milioni 60 akubali kutorudisha form za ubunge ikiwa hapo imebaki siku 4 kabla form kurudishwa kijana akakabidhi form zake kwa Magufuli wakaenda nae hadi bank kijana kabaki kwenye bench mh. waziri akaingia ndani akatoka akamwambia account yake pale haina pesa waongozane hadi Dar es salaam. Wakapanda ndege hadi Dar kijana akafikishiwa kwenye 3 star hotel kwa bili ya mheshimiwa siku tatu bila kuonanana Mh. Magufuli.

Siku ya nne kijana anaona kwenye TV Magufuli amepita bila kupingwa akashtuka kaulizia hadi ofisini kwa waziri kafika akakaribishwa Mh. kama hamjui akamuuliza shida yako nini akasema nipe pesa zangu mh. akamwambia unakuja kuniomba rushwa nikuachie ubunge wewe kijana huna adabu kabisa. Mkifuatilia CUF, hiki kisa wanakijua vizuri kwani walipelekewa taarifa kama kuna mgombea wao ameenda kuuza ubunge kwa Magufuli ikabidi Green GUARD ya CUF iende kum-arrest na kumpeleka Buguruni makao makuu na kurudi Biharamulo kwa aibu kubwa lakini baadae alimtafutia kazi kwenye mgodi huko Tulawaka anafanya kazi kumziba mdomo kwa sababu kijana alikuwa ameapa kumfanyizia.

Huyu ndiye Magufuli, je anaweza kuwa kiongozi wa nchi katika uhuni wa namna hii?

Sinema ya Magufuli haiishi hapo; kile kiapo chake cha kulipa kisasi Biharamulo Magharibi kiliendelea alipolazimisha kupindisha barabara ya lami kuingia Chato toka Mwanza kwenda Bukoba kupitia Biharamulo makao makuu ya wilaya akaipindidhia Chato nyumbani kwake na kuua makao makuu ya wilaya ya Biharamulo. Huyu ndiye kiongozi anayeweza kuongoza watu?

Mh. Magufuli alipigana na kulobby kwa nguvu zote kuhakikisha Chato inakuwa wilaya ili Biharamulo Magharibi wasifaidi mapato ya ziwa ambalo yanapatikana upande wa Chato na Nyamirembe na ndiyo kilichokuwa chanzo kikuu cha mapato cha wilaya ya Biharamulo lengo ikiwa ni katika kuendelea kulipa visasi kwa nini upande wa magharibi walikuwa hawampi kura kwa mihura takribani miwili alifaulu na Chato ikawa wilaya mpya toka Biharamulo.

Alipojikuta amesahau kuwa mgodi wa Tulawaka upo Biharamulo na haupo Chato alianza kuharasi uongozi wa wilaya ya Biharamulo kuwa ule mrahaba wa mwisho wa mwaka unaotolewa na migodi kwenye halmashauri za wilaya migodi ilipo alitaka Biharamulo igawane nusu kwa nusu mrahaba wake na wilaya ya Chato. Huyu ndiye Mh. Magufuli, je rais anaweza kuwa na tabia hizi chafuchafu namna hii?

Iliposhindikana akiwa waziri wa ardhi Mh. magufuri kwa makusudi kabisa alibadilisha mawe ya mpaka kwa amri kama waziri wa ardhi kuiingiza Tulawaka ndani ya wilaya ya chato hivyo siku si nyingi chato itadai Tulawaka ipo kwao na watapola haki ya wana biharamulo swala hili lipo wazi kabisa halmashauri ya wilaya kupitia baraza la madiwani limelalamika sana kuhusu ushenzi huu wa magufuri huyu ndiyo mtu anaweza kuwa raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania?

Mwaka jana katika mpaka mwingine wa biharamulo na chato kijiji cha biharamulo kinachopakana na chato huko kata ya Runazi wanakijiji waligundua kuna dhahabu na kuna wachimbaji wadowadogo Mh. magufuri yupo analazimisha kubadili mipaka ili hiki kijiji kihamie wilayani chato na kumekuwa na mgogoro wa kiutawala unochochewa na yeye Huyu ndiyo Mh. Magufuli anaepigiwa debe humu ndani kama anaweza kuwa rais rais huangaliwa pande zote mafanikio na madhaifu kwangu mimi madhaifu ya magufuri ni mengi kuliko mafanikio mtakumbuka kilio cha nyumba za serikali lakini huyu jamaa mkumbuke ni bingwa wa kusimamia wakandarasi na kutaka viwango kktk ujenzi lakini yote tisa kumi mh. anajenga ghotofa pale kwake anapoishi Osterbay yeye nendeni mkaone maajabu ya mussa wajenzi mafundi mchundo hata ramani hazijapitishwa sababu wachoraji ni watu wa mitaani na mafundi ni ni vibaruwa mchundo huyu ndiyo Mh. Magufuli.

Lakini skendo kubwa ya huyu bwana ambayo waandishi wangefuatilia kumjua vizuri ni jinsi alivyochezea mipaka ya wilaya ya Biharamulo kubadilisha DN za vijiji na kusogezwa mawe yalioizinishwa na serikali bila hata serikali kujua kuzipeleka Chato hii ni hujuma kubwa na anastahili kujiuzulu waandishi nendeni mkawahoji wananchi na viongozi wa wilaya biharamulo mjue huyu mtu kitu alichofanya mtu namna hii hawezi kuwa kiongozi kabisa

Huko jimboni kwake wafanyakzi wa serikali wote walio against naye amewaumiza sana wengine hata kufunga vibiashara vyao vidogovidogo ili tu wakubaliane naye kifupi hajawahi kupita bila kupngwa ila amekuwa akipita kwa hila kubwa.

Naomba kuwakilisha ili tumpime kwa pamoja. Je, tabia hizi zinaweza kumpa urais kweli?

TUMPIME KWA PAMOJA HAYO NI MAONI YANGU TU

Hii imekaa ki-2015 zaidi. Lakini mkuu mbona bado mbali sana, si tutasahau!

Mkuu hapo kweye bold inaoyesha uashaamua kuwa hafai, hayo ni mawazo yako na lazima yaeshimiwe!

Ni vizuri ungeweka na mazuri yake ili wote tumpime.

Kumbuka hili:

Ili ujue kwa usahihi kama Tanzania inamwitaji Magufuli kama rais ni bora kumpima na wagombea wengine atakaokuwa anachuana nao. Mie binafsi siamini kuwa katika watanzania wote kwa sasa Magufuli ndiye bora katika nafasi ya urais. Lakini ukimuweka na wagombea wengine (labda katika chama chake) yawezekana yeye akawa na sifa nyingi!
 
...sishangai conclusion yako, hasa ukizingatia ma-role model wako ni watekaji, wauaji, wanavisasi na wakamia madaraka km Hitler, Bush, Musolin na majenerali punguani! Do many wrongs make one right? Na Lowassa tumkubali basi, km ni uchapa kaz, au?

This is boorish and irrevant! Inahusiana nini na Magufuli hii kitu. Usiwe bendera kufata upepo. Huwezi linganisha uchapa kazi wa Lowassa na Mkwere, sifa mbaya ya Lowassa ni ufisadi. Ila yule anadhubutu. Mengine hayo yako
 
wanaompenda Magufuli wana-refer mazuri aliyowafanyia Watz, yapo na yanonekana ...wanavigezo/data!
Wewe unatoa maneno mengi kuhusu mabaya ya Magufuli ni maneno matupu yasiyo na ushahidi wa wazi, ni mambo unayafahamu wewe tu na ushahidi wake unao wewe mwenyewe basi!!
Nakushauri wakati mwingine, huna hata haja ya kuandika mambo mengi; unaweza kuandika mistali hata miwili lakini ukaeleza ushahidi wa wazi juu ya unalosema na utaeleweka...vinginevyo unabaki kuonekana mtu mwenye roho mbaya, mzushi, wivu, mchawi nk

Thank you broda! Tuko pamoja
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom