M-pesa
JF-Expert Member
- Sep 4, 2011
- 602
- 151
I am impressed! thanks a lot for sharing.
Mkuu salama,
Mbuzi mambo safi sana, namshukuru LAT kwa msaada wa Badizzo. Nina vibeberu kibao vya kisasa. Nishaanza kuuza mbegu. Mbuzi wa maziwa wapo Mbezi Makabe na wanazaa pacha bila taabu, juzi nimenunua wawili, ni 150,000/ kila mmoja. Bado sita kwa yule mzee. Kwa sasa nafanya upanuzi na uboreshaji wa fish ponds,kwa upande wa tilapia walifika market size ndani ya miezi sita,japo niliwaweka ktk mazingira magumu sana.
Uchimbaji unaendelea, na African catfish nitawaweka pond ya peke yao ili na wao nione kama watafikia market size ndani ya muda wa kitalaam.Hivi ninavyo andika niko Iringa mjini, nilifuata vifaa vya shamba, msimu unapiga honi, ninataka kuhakikisha tunapiga bao. Nikirudi dar nitakujulisha, ila ni kipindi cha november ndio tutafanya safari hiyo.