kwa wanandoa wanawake-kwa nini ujichoshe na mume?

Hivi smile, hivi vituko huwa unavipata wapi? maana dah..... nikifungua nyuzi zako lazima kwanza nicheke, sometimes hadi boss anajua kumbe sifanyi kazi bali nabrauzi internet. Ila safi sana maana napata nafasi ya kufungua mdomo .....
 
Ndoa inapitia vipindi tofauti, labda kwa faida ya wasomaji nijaribu kuelezea in a nutshell;

Siku ya harusi mpaka miaka mitatu baadae, hapo kuna mtoto kama mmebahatika ila hata kama hakuna mtoto hapo bado wanandoa hampati stress mkiamini mtapata tu. Ndoa kipindi hiki huwa tamu, mke na mume hupitiana kazini, kama wana magari mawili wao hutumia gari moja, wanatoka out for dinner, hakuna anaemhisi mwenzie anacheat, mapenzi motomoto na home shopping za pamoja, kila uendako wamjulisha mwenzio nk nk nk!

Mwaka wa tatu mpaka wa saba; mshaelezana misimamo ya ndoa yenu, kila mmja sasa keshafahamu true colors za mwenzake! Mke kajua mumewe huwa hafui c.h.pi, mume kajua mkewe haogi jioni etc etc etc, ndugu wameanza kuja, ndugu wa mkeo wanakuja zaidi, ndugu wa mume wakija wanaingia kama kwao hawaogopi, mke kaanza kupunguza outing, mke kaanza kuchukia marafiki baadhi wa mumewe, mke kaanza kuficha kipato chake kwa kisingizio mwanamke lazima awe na akiba. Mume anagundua mke hapendi kwenda ukweni kwani hapatani na baadhi ya mawifi zake. Ugomvi wa mara kwa mara kwani mshazoeana mnaishi kama haitatokea mmoja kumtaliki mwenzake pamoja na maudhi yote. Mke ndo anakuwa msemaji, mume hukaa kimya kwani yeye keshaboreka so anasubiri jioni ifike aende kuangalia futbol kwenye pub pamoja kwake ana DSTV ila haipandi, na wakati huo kanyumba ndogo hakakosekani ka kuchangamsha damu maana mke hujisahau au hukosa hamu kwa kisingizio cha ugomvi au uchovu, etc etc etc.

Miaka tisa kuendelea; mshazoeana, mshasameheana sana, mke keshafuma msg za mapenzi kibao, mume keshafuma nae, either mmebahatika kudumu na kupita, mnajikuta mnaanza kukua kiakili, mnajali watoto, mnajali maendeleo hapo hata mke akijua kuna katoto cha nje, hukasirika ila huwa mpole na anaweza kukuambia umlete nyumbani amfahamu etc etc etc! Hapo kama hamkutalikiana, mapenzi hurudi kwa kasi na mnapofikisha miaka 15 mnatamani mfikishe JUBILEE!

Wandugu NDOA SI LELEMAMA ESPECIALLY NYIE WADADA.
Mkuu unatisha sana
 
Back
Top Bottom