Kwa Wanandoa: Bila tendo la ndoa hakuna ndoa(?)

amakyasya

JF-Expert Member
Jun 26, 2013
3,480
907
Jamani hakuna ubishi kuwa tendo la ndoa ndilo linaloshikilia ndoa bila hivyo hakuna maana ya ndoa.

Hata kama kuna mataizo mwanandoa hastahili kumnyima unyumba mwenzie, cha kufanya ni kutafuta suluhu ya tatizo huku huduma ya msingi ya ndoa ikiendelea kama kawaida.

Kilichotokea kwa mumewe Flora Mbasha mpaka kabaka shemejiye ni matokeo ya kunyimwa unyumba kwa muda mrefu na aibu hii ni kwa wote wawili. Katika hili sio kwamba nampongeza huyu jamaa kubaka ila najaribu kusisitiza wajibu wa mwanamke au mwanandoa kwa mwenzie.

Tafakari, chukua hatua.

==========
Maoni:

Mwanamke, unapombania tendo la ndoa mmeo, fahamu hilo Ndio ndoa yenyewe

Habarini,

Tujikumbushe wanawake, maana ubize wa kazi nao unatufanya tuwanyime wwanaume mchezo uleee...

Naona hili suala bado wanawake halijawakaa sawa, Kumekua na malalamiko huku ndani mengi kuhusiana na wanawake kuwanyima tendo la ndoa waume zao au kuwapa kwa kubeep.

Sikia wewe mwanamke ulieolewa, Ndoa haiwezi kukamilika bila huo mchezo, na wanaume wanatoka nje za ndoa zao kwakua wanawake wao wanawapangia siku za kufanya mapenzi.

Mwanamke hakikisha unampa mumeo mchezo wakati wowote akitaka na pia usisubiri akuombe muandalie mazingira ya kucheza kamchezo hako, mpe mama ale ili asitoroke.

Mwanamke unajifunika muda wote mkiwa ndani acha mwili wako kimtego zaidi. Hatakama umechoka tafuta njia ya kumfanya mumeo aridhike kwa kachezo hako.

Najua makungwi wapo huku, Karibuni tujikumbushe atoto evelyne salt miss chagga

Maoni 2:

Ndoa ni zaidi ya Tendo la ndoa!

Leo naomba tuwekane wazi juu ya hili maanake naona vijana wengi siku hizi wana maoni tofauti juu ya ndoa na maana yake na namna ya kuidumusha

Wengi wana illusions za maisha ya ndoa walio wengi wanaamini tendo la ndoa linachukua asilimia kubwa zaidi na mengine ni kidogo sana.

Ukweli ni kwamba ndoa ni zaidi ya kugegedana, japo tendo la ndoa ni kiungo kikubwa katika ndoa, lakini hilo sio kila kitu, ndoa ina mengi na ndo maana tukiwa alter tunaapa katika shida na raha.

Ukiingia kwenye ndoa kwanza kumbuka umejitoa kwa ajili ya yule mwenzi wako ambaye mnatoka katika malezi tofauti tofauti na pia mmeunganisha koo mbili ambazo zote macho yao bado yapo juu yenu, kwani ninyi kufunga ndoa haimaanishi kwamba mtakuwa na ulimwengu wenu wenyewe.

Kwa sababu hizo basi katika ndoa haya yanaweza kutokea:

- Kutoelewana kati yenu.

- Kutoelewana kati ya mmoja wenu na ndugu.

- Ugonjwa wa kufisha kati ya mmoja wa ndoa.

- Malezi ya watoto.

Na mengine mengi ambayo ukiyaangalia yakijitokeza hata huwezi kufikiria tendo la ndoa.

Hivyo basi, this is my take:
Kwa vijana tuache kuliweka tendo la ndoa kama kipaumbele ambacho tungependa wenzi wetu wa ndoa wawe nacho sijui awe mjuzi kiasi kuonja kabla ya ndo ndio imekuwa habari ya mjini, hilo ni la ziada tu mengi yanahusika.

Nawasilisha karibuni wote kwa pamoja tulijadili hili na wenye uzoefu watupe uzoefu wao ili sote tujifunze na tunufaike.

Recommended for reading:

1) Kwa Wanandoa: Conjugal Right/Haki ya tendo la ndoa

2) Tendo la Ndoa: Faida/umuhimu wa kushiriki tendo hili

3) Zifahamu nyakati kuu 3 muhimu za kufanya tendo la ndoa

4) Sababu 10 kwa nini mnatakiwa kufanya tendo la ndoa asubuhi mara kwa mara kwa wanandoa
 
Unajua sababu ya kumnyima?ushamfumania mara kadhaa,kwa nini nsikunyime labda mi sikutoshi ndo maana. flora si chizi amnyime maradhi mengi jamani,tutauana.Kingine mwanaume hana akili milupo wote hawa ndo umfate shemeji???genye hizo genye gani hasa mpya chini ya jua!
 
Unajua sababu ya kumnyima?ushamfumania mara kadhaa,kwa nini nsikunyime labda mi sikutoshi ndo maana. flora si chizi amnyime maradhi mengi jamani,tutauana.Kingine mwanaume hana akili milupo wote hawa ndo umfate shemeji???genye hizo genye gani hasa mpya chini ya jua!
Alitakiwa ajichunguze na kujitathmini kwa nini mumewe anachepuka ili aweze kumuweka kwenye himaya yake vizuri. Inawezekana Flora mwenyewe alianza uvivu na kusahau wajibu wake kwa mumewe.
 
Sometimes ukiwa mlokole kupitiliza ndo matokeo yake hayo.
Ila mdau kwanini abake wakati hawa viumbe wamejaa kibaoo.
 
Alitakiwa ajichunguze na kujitathmini kwa nini mumewe anachepuka ili aweze kumuweka kwenye himaya yake vizuri. Inawezekana Flora mwenyewe alianza uvivu na kusahau wajibu wake kwa mumewe.


Mbona wewe km vile umeshathibitisha kwamba Florah ndo alikua na matatizo?? hata kama Florah ndo alikua na matatizo kwa kumnyima mumewe but does that makes it okey kwenda kubaka?? siangetafuta jinsi nyingine ya kujiridhisha. Mbona kuna watu wananunua wanawake wa kufanya nw tendo la ndoa na wengine wanatafuta watu ambao wako tayari.

Hivi km ni kweli huyo mume alikua anacheat we ulitaka Florah ndo aendelee kumvuta tuu, mbona tunasahau kuwa hata Florah ni binadamu na anahisia pia? Mbona kuna wanaume wanapatiwa kila kitu and still wanacheat??? Hata wanawake pia wapo wanaopata kila kitu and they still cheat.

So kwangu mie kila mtu awe responsible kwa makosa yake na sio kutaka kumsingizia mwingine ndo amesababisha. Kila mmoja wao ana mchango wa kuifikisha ndoa yao hapo ilipo no matter who started.
 
^^
Wawe watumishi wa Mungu, wawe watu maarufu wa fani zote, Wawe wachangiaji bora wa miaka yote JF au popote pale...
Ukweli utasimama, hawaishi maisha ya mapenzi yaliyotofauti na dunia hii. Si ajabu kwao kwani yakifunguliwa yaliyofichwa katika nyumba zetu, kuna siri zinazonuka
^^
 
hawa kumbe walimpokea bwana sio....?sasa nini wanadhalilishana....!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom