Kwa walioko kwenye ndoa, mawazo yenu please

Jamani mimi ni kijana wa kiume nimeoa miezi mitatu iliyopita, naomben wadau mnisaidie kina jambo linanitatiza. Mimi kwetu ni Dar es Salaam na wazazi wangu wanakaa Dar es Salaam. Lakini mke wangu yeye kwao ni mkoani na wazazi wake wanaishi huko mkoani. Swali langu ni hili, hivi naweza kwenda nyumbani kuwasalimia wazazi wangu bila kuwa na mke wangu mfano nimetoka kazini halafu nikapitia nyumbani then nikamwambia mke wangu kuwa nimepitia kwetu, hiyo itakua mbaya au inatakiwa kila nikienda nyumbani niwe na mke wangu au nimfahamishe mapema kabla ya safari? Naombeni ushauri wenu na namna ya kuhandle hili suala maana mimi bado mchanga kwenye ndoa.

ongea na mkeo uone yeye analichukuliaje hilo, vunja ukimya zungumza na mwenzio
 
Ameshasema kwa waliooa tu; halafu mtu anaingia anasema "ingawa mimi sijaoa ........". Huku ni kutomtendea haki mwenye maada. Yeye anataka waliooa tu waseme! Wale ambao hamjaoa, kaeni kimya, msikilize waliooa wanasema nini; nafasi yenu ipo!

Ukishaoa au kuolewa, surprises huwa si kitu kizuri. Kifupi ni kuwa ukienda sehemu ambayo mwenzio hajui kuwa umekwenda huko ni vizuri umtaarifu, jamani technolojia inaruhusu. Zamani enzi za barua na simu za waya tu ilikuwa vigumu, ila sasa ni rahisi, kwa nini usimtip mwenzio kuwa unapitia kwa dingi wako?

Kupita pita huko mara kwa mara peke yako kuna mpa wasi wasi mwenzio kuwa pengine una mambo unajadili na wazazi wako ambayo hutaki yeye ajue. Hizi perceptions kwenye ndoa ni kitu kibaya sana na kinaleta wasi wasi usio na msingi. Mwambie mwenzio nitapitia kwa wazee.

Kupita pita huko vile vile peke yako kunamfanya mwenzio aonekane yeye hawajali wazee wako. Mbona wewe wapita yeye haji? Wale wazazi wako wanaweza kufikiri kuwa unaenda peke yako sababu hutaki kufuatana na mkeo.

Kifupi ni mengi sana ya hisia tu, ila yana matokeo mabaya. Mwambie kuwa utapita huko, kama ana nafasi naye aungane nawe!
 
Mimi nadhani unamtafutia balaa mke wako. Majukumu ya familia yako yakiaanza kubana ukisha pata mtoto automatically hizo safari kwa wazazi zitapungua kwa asilimia kubwa sana. Then results zake zinaweza kuwa mbaya itasemekana kwamba mke wako ameanza kuzuia then kitakacho fuata mke wako hatokuwa in good terms na wakwe zake. Pangilia safari zako you have to get used to it ndio maana ukawaacha wazi wako ukambatana na mkeo. Also kumbuka wazi wako pia waliwaacha wazazi wao.
 
wazazi wako.wanajua kuwa unakwako hivyo ni vyema.safari za nyumbani kwenu zipungue. Mkeo ni mtu muhimu sana na karibu kuliko yoyote mpe nafasi aone umuhimu wake kwako, pangani pamoja kutembelea wazazi wa pande zote, tangu ulipooa mkeo ndiyo mtu wa kwanza kwako, ni vizuri mnapotembelea wazazi muwe pamoja tena muwe na kiasi isiwe mara kwa mara.
 
Guys I am really overwhelmed for your comments and contributions, kweli Jamii Forums ni kila kitu ,ntazingatia michango yote na naamini hakuna kitakachoharibika, asanteni sana na Mungu awabarikini kwa michango yenu mizuri

 
habari kaka. Mimi ushauri wangu katika suala hili ni kuwa, hata kama huendi na mke wako kwa wazazi wako, ni muhimu KUMPA TAARIFA yaani awe anajua kuwa umepitia kwa wazazi wako. Unajua kaka, katika hiyo hiyo ndoa, kila mmoja wenu anatakiwa awe anafanya kitu kwa mwenzake ambacho hata yeye anapenda, yaani hapa namaanisha hata ingekuwa ni yeye wazazi wake wanaishio hapa dar, WEWE USINGEPENDA akapitia kwao huko BILA kukupa wewe taarifa... kwa sisi waislam, hata ukienda msikitini unatakiwa umpe taarifa mwenzako awe na taarifa zako. Sasa kama unaenda bila kumjulisha halafu unapata matatizo njiani kwa namna yeyote ile, ndio utaanza kumtafuta au?hatuombei hayo ila tunatakiwa kufikiria kwa upande wa pili pia. UWE UNAMUAGA/KUMPA TAARIFA na ARIDHIE, ndio uendelee na safari zako. Ni hayo tu.
Jamani mimi ni kijana wa kiume nimeoa miezi mitatu iliyopita, naomben wadau mnisaidie kina jambo linanitatiza. Mimi kwetu ni Dar es Salaam na wazazi wangu wanakaa Dar es Salaam. Lakini mke wangu yeye kwao ni mkoani na wazazi wake wanaishi huko mkoani. Swali langu ni hili, hivi naweza kwenda nyumbani kuwasalimia wazazi wangu bila kuwa na mke wangu mfano nimetoka kazini halafu nikapitia nyumbani then nikamwambia mke wangu kuwa nimepitia kwetu, hiyo itakua mbaya au inatakiwa kila nikienda nyumbani niwe na mke wangu au nimfahamishe mapema kabla ya safari? Naombeni ushauri wenu na namna ya kuhandle hili suala maana mimi bado mchanga kwenye ndoa.
 
mie nahisi umeoa ukiwa mdogo sana,maswala mepesi kama hayo yanakushinda kufanya maamuzi,je yakija mazito si utakufa kwa pressure?

Mi nadhani kila jambo kama kuna uwezekano wa kuomba ushauri ni bora uombe alf mwisho wa siku unaatoa maamuzi kuzingatia ushauri uliopewa hata kwa masuala mazito.
 
hilo swali hukustahili kulilta humu kwani linahitaji akili kidogo sana. wewe umeoa, that means wewe na mke ni kitu kimoja. but suala la kwenda nymbani kwenu lisiwe kisingizio cha kila siku ukitoka kazini.

kama kuna ulazima wa kupita nyumbani then unaweza kwenda bila wasiwasi ila ni vyema ukamjulisha mkeo kua ukitoka kazini utapita kwenu as kuna ishu inayokupeleka huko.

Mara nyingine funga safari wewe na mkeo muende wote kwa wazazi wako na pia hata wazazi wake. ila mjenge mazoea pia ya kwenda kuwasilimia wazazi wako mara kwa mara kwani nae ni mmoja wa familia yenu kwa sasa.
 
kusalimia mara moja moja sio mbaya but usifanye tabia..maana baada ya mda mke ataanza kumaindi...
 
Usiende mwenyewe Hebu jaribu kwenda na mkeo kwa wazazi japo weekend mojamoja kuepusha lawama na manung'uniko yasiyo na lazima. Umeoa maana yake ni umekua mambo ya kufatanafatana na wazazi kila dakika si mazuri.
 
Mimi nijuavyo akishakua na familia yako wewe mtoto wa kiume yabidi uwe ni mtu wa msimamo. Na kitu kimoja kinachoangaliwa ni uwezo wa kujitegemea - kiuamuzi.

Kwenda kusalimia wazazi sio mbaya, ila ni mara ngapi unaenda kusalimia? yaan unaenda kwa mdingi wako afu mwapiga stori mwishowe wawaambia nilipita tu kimtindo kuwacheki? itakushushia hadhi yako wewe kijana. either wanaweza kufikiri una tatizo kwe familia yako ila kusema unashindwa au you are not grown up.

na usipomwambia mkeo kuwa umepita kwenu, baadae mkweo akampigia simu kumwambia kuwa ulikuwepo kule, jua hapo unatengeneza ugomvi mwingi ne kwa mama watoto-kuwa kule kwa wazazi ulifuata nini bila kumshirikisha?

na isitoshe sio kila mara lazima ukutane na wazazi wako wote. waweza kumita m-sure sehemu mkapiga stori, then kila mtu akachukua hamsini zake. na hii itakua na maana sana kuliko kuwa hukauki nyumbani kwao.

KIufupi, Ndoa huwa inathibitisha maturity yako. sasa jiulize a matured person anatakiwa a-behave vp?
 
ukipita kila siku/mara kwa wazazi wako unaweza mpa hisia mwenzi wako kwamba maamuzi yako mengi
yanatoka kwa wazazi wako, hivyo mkitofautiana kidogo tu na mkeo lawama zinaweza angukia kwa wazazi
wako. hivyo epukana na trip za mara kwa mara kwa wazazi wako.

jee wazazi wa mkeo wangekuwa na wao wapo hapo mlipo utafurahia mkeo akiwa kila siku anashinda kwa
wazazi wake?
 
asubui unapotoka home mwambie,honey leo ntapitia home kuwapa hi.aki obligate then pospone mpange siku muende wote.au kama vp mjulishe kwa njia ya simu kwamba unapitia home kuwapa hi.
 
punguza safari za nyumbani za mara kwa mara, na kuna siku unaweza pita pia ukampa taarif, ni namna tu ya nyie mlivyozoea, sie tuna mfanyakazi mwenzetu mwanaume, hata tukisema tukapate lunch mje ya ofisi anainu simu utasikia naenda kula nje ya ofisi niko na blackberry,nokia, kimchina nk, nashangaa kweli, mi hapo wala sisemi wakati mie mwanamke,mahusiano ni nyie wenyewe mlivyojipangia
 
ni vizuri ukimtaarifu mkeo ili kuepuka maswali yasiyokuwa na majibu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom