Kwa wale wanaojiunga 1st year wazingatie haya

zema21

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
619
251
Vijana wengi wanapopata nafasi za kujiunga na vyuo huwa wanafurahi saana na kuona kuwa wamepiga hatua kubwa saana na pia huwa hawashauriki wakiamini wameshafika mahali ambapo wanaweza kujiamulia mambo na kufanya lolote wanalolitaka.....
Ukienda kutembelea vyuo mbalimbali utasikitika kuwaona baadhi ya mabinti wadogo wakitembea na nguo zinazoacha sehemu kubwa ya miili yao nje(nusu uchi). Pia wavulana/wanaume baadhi huishia kuingia kwenye ulevi na uvutaji wa bangi na mambo mengine machafu..
Pia utashuhudia wengi wao wanawekana kinyumba...

Ushauri wangu kwenu ni kwamba kabla hujafanya maamuzi jitafakari kwanza... fikiri kwa makini, wafikirie ndugu zako, wazazi, walezi, wadogo zako na wengineo.....kisha ndo ufanye maamuzi ya kujiingiza kwenye haya magenge kwani wengi wamejikuta wakiwa wanajutaa mno lakini inakuwa haina maana kwao kwani huwa inakuwa too late kwao.....kwa wale waliokuwepo UDOM 2011 college of education walishuhudia jamaa mmoja akijaribu kujiua kwa hali na mali katika jaribio la kujirusha ghorofani baada ya kujigundua kuwa ameambukizwa HIV na kwa makusudi na binti aliyekuwa mpenzi wake.. Pia yupo jamaa alimwagiwa maji moto usoni na msichana aliyekuwa mpenzi wake lakini kisa cha kumwagiwa maji msichana alikuwa hana mapenzi ya ukweli kwa kijana yule....Tafakari kila njia za mienendo yako ukiwa chuoni..uhakikishe kila unalolitenda halitakuwa na majuto yoyote kwako na jamii yako...kuwa mfano wa kuigwa na jamii badala ya kuwa reference ya maovu....
Kama unataka kuingia katika relation iwe ni mara yako ya kwanza au la kuwa makini saana mchunguze mno unayetaka kuingia naye katika mahusiano...Kumbuka kwenda kupima ukiwa na mwenzi wako......pia kumbua saana kuwa maisha hayajabadilika wala level yako ya undergraduate si ya kukufanya ujisahau ujione kama ndo umesha-win .....
Mtangulize MUNGU katika kila Jambo hudhuria msikitini, kama ni mkristo Fellowship/kanisani usikose....tenga muda wako kufanya mambo ya kijamii pia MWENYE MASIKIO NA ASIKIE
Naomba kuwasilisha
 
Eh Mwenyezi Mungu nakukabidhi maisha yangu haya yenye vishawishi vingi.
Ubarikiwe sana ndugu kwa huu ushauri
 
Nashukuru mkuu,ujumbe umepokelewa. I wish someone called 'bitbull' kama sijakosea jina lake apate ujumbe huu pia. Inaonyesha jamaa kaenda kuanza na wenge.
 
Nashukuru mkuu,ujumbe umepokelewa. I wish someone called 'bitbull' kama sijakosea jina lake apate ujumbe huu pia. Inaonyesha jamaa kaenda kuanza na wenge.
 
Back
Top Bottom