Kwa wale mlio na uhitaji wa kusoma/kujifunza lugha ya Kichina UDSM

emmarki

JF-Expert Member
Nov 22, 2012
682
918
Mimi nikiwa mmojawapo niliyekuwa na shauku ya kutaka kujifunza hii lugha ya kichina. Niliwandikia UDSM mail, nashukuru wamenijibu mapema jana. Soma zaidi kwa ufafanuzi.

Pamoja na Salamu kutoka CI

Hii ni kuhusiana na Darasa la Lugha ya Kichina kama habari iliyopo inavyotaka
1. Kuna masomo ya jioni ambayo hutolewa mara nne kwa wiki (Jumatatu, Jumanne; na Alhamis na Ijumaa).
Kwa kila siku hizo, wanafunzi hukutana na walimu kuanzia saa 10:30 jioni hadi saa 12:30 jioni.
2. Madarasa haya yanawaandaa wanafunzi kujifunza lugha ya Kichina kwa ngazi mbalimbali. (Ngazi hizo zinajulikana kama HSK. Hivyo kuna ngazi sita, yaani HSK I, II, III, IV, V na VI). Ikiwa mwanafunzi atapitia ngazi hizi zote na KUFAULU , anahakikishiwa kuwa atakuwa na uwezo wa kuongea lugha ya Kichina kwa kiwango cha juu (Advanced level )
Mafunzo kwa kila ngazi huchukua miezi miwili.
3. Ada kwa kila ngazi ni Tsh. 300,000/= kwa kila mwanafunzi.

Muda wa kujiandikisha.
Mafunzo katika ngazi ya awali yaani HSK 1, yataanza Januari 16, 2023.
Mwanafunzi anayetarajiwa kujiunga anaweza kutuma maombi kwa
ci@udsm.ac.tz

Nitakuwa tayari kujibu swali au kutoa maelezo ya taarifa yoyote ambayo si wazi

Karibu

Aldin
 
Inachukua muda gani kusoma ngazi hizo zote sita ,
 
Back
Top Bottom