Mimi naamini elimu ni kitu cha msingi kwa mwanamke ili aweze kusimamia maisha yake mwenyewe, familia yake hata kukwepa manyanyaso yanayosababishwa na baadhi ya wanaume ndani ya jamii. Hata ndani ya ndoa mwanamke aliye elimika ni rahisi sana kukabilia na changamoto za mazingira yanayo mzunguka. Hebu angalia wanaojiunga kidato cha tano hapa chini
"Wanafunzi 36,366 ambao ni asilimia 98.31 ya waliokuwa na sifa stahili wamepangwa kidato cha tano na vyuo vya ufundi, kati yao wasichana ni 11,210 sawa na asilimia 100 ya wenye sifa na wavulana ni 25,156 ambao ni asilimia 97.58 ya wanafunzi wenye sifa," .
Wanafunzi wa kike waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano pamoja na vyuo vya ufundi ni asilimia 30.83 ya wanafunzi wote 36,366 waliopangwa.
Kutokana na uwiono 30:70 wa wanafunzi walijiunga kidato cha tano ni dhahiri kwamba kumpata mke mwenye elimu kuanzia kidato cha tano ni changamoto kubwa. Kumbuka hii dunia ya utandawazi elimu ni silaha kubwa ya kupambana nayo.