Kwa ufupi: Bilal alikuwa aondoke CCM...

Kubalini tu kwamba JK kama mchezaji wa Uruguay kacheza mpira unaoingia kimiani..CCM wamejipanga vizuri bara na visiwani na sioni mahala Upinzani wanaweza kumpa shida unless...... mnajua nataka kusema nini?
Ni wakati wa penalt kick - Upinzani chagueni wapigaji tuone!

Ninavyomfahamu Jakaya kwakawaida ni jeuri, lakini kwa kumteua Bilal kuwa running mate wake ameonesha ukomavu na busara ya kisiasa kuwa anaweza kusikiliza ushauri!! I could be wrong lakini nadhani yeye mwenyewe hakuwa na wazo la kumteua Bilal bali wazee wenye busara walishaona ugumu wa ccm kushinda visiwani pale wanaccm kutoka visiwani walipoondoka Dodoma na kurudi visiwani kabla ya Congress!! Bila kumteua Bilali kazi ingewawia ngumu sana safari hii; na ndio maana kuja kwa Salmin Dododma kwenye vikao vya uteuzi kulikuwa na maana yake muhimu!! Tushukuru sanity prevailled!
 
Bilal angetoka aende wapi Jamani?..hizi discussion zetu sometimes hazina tofauti na zile za vijiwe vya kahawa. Huwa tunawadharau wa vijiwe vya kahawa, na kumbe sote ni walewale..tumetofautiana tu majamvi ya mijadala.
 
MM, mimi nadhani hawa jamaa wa CCM walitaka kucheza karata za kisiasa, karata za kutuliza mambo visiwani. Kwa jinsi ilivyo walitaka kutuliza kiu ya wapemba ambao wamekuwa wakilalamika kuwa hawapati nafasi za uongozi a.k.a urais. Tatizo ni kuwa CCM hawapo tayari kumpa mgombea wa CUF nafasi kama hiyo, kwahiyo Shein akatumwa kwa vile anaonekana kuwa na sifa hata kama si lazima ziwe za kweli. Kwa bahati mbaya Seif anatoka pemba kwa hiyo njia nyepesi ya kupunguza au kugawa kura za pemba ni kupitia Shein. Hapa ndipo karata mbovu ilipochezwa kwasababu unguja kwa mazoea wanadhani ndio wazanzibar na rais lazima atoke hapo. Kitakachofuata ni CCM kupoteza majimbo ya unguja kwa kura za hasira.
Kama upinzani ungekuwa unajua kusoma alama za nyakati hili la dodoma ni ''gross mistake'' na wange tumia fursa hii kuingia ikulu kiulaini. Bahati mbaya hakuna mkakati wa hilo. Nasema hakuna mkakati kwasababu hata huku bara upinzani umedoorora. Kama ingelikuwa nchi za wenzetu wanaojua kucheza na politics JK asingerudi magogoni. JK amezungukwa na ushahidi wa kutosha kabisa kuwashawishi wananchi kuwa ameshindwa kazi lakini wapinzani wamelala hadi october 22 ndipo waanze kampeni.
Mfano mzuri kama JK antumia data za kupika kuwa uchumi umekuwa kwa asilimia 6.4 kwanini wapinzani wasiwaambie wananchi kuhusu inflation toka 7 hadi 11.
Kwanini wapinzani wasitumie data kuonyesha mamilioni yanavyotafunwa!
Kwanini wapinzani wasieleze uzembe wa serikali kama kupoteza bilioni 200 kwa fuel adulteration
Kwanini wapinzani wasieleze wananchi kuwa fenicha :sick: za ofisi moja zinajenga zahanati.
Kwani wapinzani wasieleze wananchi kuwa hela za vitafunio vya chai ni kubwa kuliko thamani ya vijiji vyao.
etc etc etc....

Wapinzani kama mtaenda na sera za kinadharia asilimia 70 wanafuata mkumbo na hawatawaelewa, waambieni wananchi uhalisia wa maisha yao na umasikini wao na si wa taifa. Nina uhakika ukimweleza mwananchi kuwa thamani ya VX moja ni sawa kujenga madarasa 50 au zahanati 10 watawaelewa. Lakini si Singara wala zinduka hatuzisikii tena.
This year was an opportunity to reclaim our country from fisadi but it seems as if we have long way to go.
Nguruvi3,
Wapinzani wakianza kufanya kama unavyoshauri utasikia CCM wakilalamika kuwa wameanza kampeni kabla ya wakati wake. Wapinzani lazima wawe waangalifu, to play by the game, ili wasitumbukie katika mtego wa CCM. Wakati wa kujadili uongo na statistics za kupikwa za CCM utawadia tu katika uchaguzi wa mwaka huu, lakini tuseme mfano, CHADEMA, ambacho ni chama pekee makini kwa hivi sasa, wakianza kupiga kelele utasikia malalamiko kuwa wameanza kampeni kabla ya wakati wake. Tuvute subira na kama kweli tunataka mabadiliko, tuwaunge mkono CHADEMA kwa hali na mali.
 
Jamani haya maswala tumeyaona toka wakati wa Nyerere...Hii kitu ilishapangwa mapema semeni sote tulikuwa kizani kama hao kina Bilal na wengine. Kila mmoja wao aliahidiwa nafasi yake ktk mkeka wa KULA pilau la Maulidi!..Meza gani amekaa haiwezi kumfanya asusie chama kubwa kwani angepoteza hata Utajiri wake, CCM wangemmaliza kisiasa na kiuchumi..

Mkandara mkuu, safari hii wazenj walikuja tofauti na walikwisha amua kurudi kwao mara tu baada ya Bilal "kushindwa" kwa kutumia wingi wa wajumbe wa kutoka bara!! Kuja kwa komandoo kuhudhulia vikao hivi vya chama baada ya muda mrefu ilikuwa message tosha kwa Jakaya na wenzie kuwa walikuwa na lao jambo. Tushukuru wahenga wameweza kutegua kitendawili hiki!!
 
.

Na hivi ndivyo mnavyovyakiwa kufanya na CCJ yenu, ama join them ama tuunganishe nguvu against common enemy, other wise, we are doomed and will remain doomed!.

PASCO, you have nailed it!!!! HIli ni somo zuri sana na natumaini kwamba Mwanakijiji amekusoma vilivyo.... The biggest problem ya upinzani ni kukosa mwelekeo especially when it comes to common enemy!!!
 
By the way Shein, kutoka makamu wa rais wa Jamhuri na kuwa rais wa Zanzibar ni kushuka mamlaka au ndio yameongezeka?

Shein ilikuwa ni lazima aachie ngazi, maana yeye kama makamu ile ni taasisi ya urais ambayo hutakiwa baada ya miaka kumi uchomoke.

Kuwa Rais/Mtu wa mwisho kwa serikali ni kupanda cheo. regardless ya udogo wa nchi husika. Rais wa Rwanda ni sawa na Rais wa Nigeria. Kuwa makumu wa Rais wewe ni mshauri tu.

Aidha in terms ya ukubwa wa sehemu ya kutawala yap ameshuka madaraka... lakini madaraka aliyokuwa nayo si yalikuwa ya kushauri tu?
 
chrtsrv.dll

Thanks for reminding us kwamba shilingi yetu itaendelea kuporomoka hadi tutakapoacha kuchagua mabazazi wa kisiasa... in fact inasikitisha jinsi tunawapa akina bilal, KJ na ccm yao promo hapa jamvini wakati our bigger problem is politicization of everything hadi uchumi
 
Nguruvi3,
Wapinzani wakianza kufanya kama unavyoshauri utasikia CCM wakilalamika kuwa wameanza kampeni kabla ya wakati wake. Wapinzani lazima wawe waangalifu, to play by the game, ili wasitumbukie katika mtego wa CCM. Wakati wa kujadili uongo na statistics za kupikwa za CCM utawadia tu katika uchaguzi wa mwaka huu, lakini tuseme mfano, CHADEMA, ambacho ni chama pekee makini kwa hivi sasa, wakianza kupiga kelele utasikia malalamiko kuwa wameanza kampeni kabla ya wakati wake. Tuvute subira na kama kweli tunataka mabadiliko, tuwaunge mkono CHADEMA kwa hali na mali.

Jasusi kaka yangu, hii ni rai nzuri sana, lakini je hao CHADEMA wako tayari kuungwa mkono na wapinzani wote?? wewe huoni kwamba tayari wao vichwa vyao vimekua vikubwa kuliko uwezo wa shingo zao wakati bado ni neonates kwenye siasa hizi za majitaka??

Je huoni kwamba hii rai ni vizuri ingetoka kwa CHADEMA wenyewe , washuke chini, wawe humble na wa-extend their hands to reach out to other opposition parties??

si hawa CHADEMA baada ya mawe ya muda mfupi tu hapa jamvini wali-succumb na kuliacha jahazi hili lenyewe??

I PRAY FOR CHADEMA TO COME BACK AND EXTEND THIER INVITATIONAL TO ALL OPPOSITION PARTIES ili common enemy awe addressed, IMO, i wish for opposition kusimamisha mgombea mmoja tu kila jimbo ili apambane na wa CCM and that means kura za maoni kwa kila jimbo kwa wapinzani zipigwe pamoja na nomination moja
 
yeah JK amefanya vizuri kwa kuwa wakati wa Mkapa ilikuwa 1000 Tsh kwa dola moja na kwa JK ni 1500. 1000 seems to be lower than 1500, isn't it?

Ukiangalia takwimu zote za uchumi utaona kuwa Mkapa was far better by any measure kuliko JK. Naona kazi zinazohusu uchumi JK ameziacha kuwa ni kiporo cha serikali inayokuja, yaani baada ya yeye kumaliza muda wake.
Enh hii ndiyo interpretation. Yaani unaangalia value at the end baada ya kuanzia kwenye initial value. Huku si kulianganisha na ndiyo maana tunaendelea kulaumu bila ya kuwa na back up.
 
Wana JF Mi kila nikisign in humu ndani huwa najifunz mambo mengi ambayo yanajenga fikra za mtu.

Nipo ugaibuni lakini kupitia mzee michuzi nilitazama tukio zima.

Kilichonikera cha kwanza ni hotuba ya mkuchika aliposema kuwa walioda hotel na kuna baadhi ya watu wameingia bila ridhaa yao na hawakuwa wajumbe wa kamati ya CCM.swali nilililo jiuliza-Je ukiwa mjumbe wa CCM Una haki gani ya kumwamisha au kumuonea mtanzania yoyote yule? Jambo hli liliniuma saana maana watu waliokuwa hotelini ni binadamu na naamini walikuwa na cfa zote za kuishi kwenye zile hoteli. Na kama huu unyama wa kufukuza watu walioufanya kwa kusaidiwa na polisi wasiojua wajibu wao kikamilifu umebarikiwa kutoka juu-hakika hawana budi kuwaomba radhi wale wote waliowafukuza kutoka kwenye hotel zao.

La pili ni ufujaji wa pesa zetu sisi-maana na mimi nalipa kodi. Ukienda shuleni jamani watoto wanakaa kwenye vumbi na mwalimu amecmama . Wamebanana hawana hata sehemu ya kuweka mifuko yao achilia mbali sehemu yenyewe ina vumbi. Watu wanalia sukari imepanda bei hadi 2500 wakati tuna viwanda maana yake ni nini? Wafanyakazi hatupewi mshahara wakati kumbe hela zimehifadhiwa kwa ajili ya mkutano wa CCM Dodoma. Basi mmetunyima sisi hizo hela wafanyakazi-basi waokoeni akina mama wajawazito na wazee wetu wasitaafu,na hapo tukiachilia mbali wale ambao wanakunywa maji ya barabarani toka uhuru kwani hawana vicma mpaka leo na wala hamna mpango wa kuwekwa kwa vicma hivyo.

La Tatu ni waimbaji ambao hata wa nyimbo za injili wote jana walicfia uovu na kubariki machafu yote yanayofanyika kwa kutoa cfa hata amabzo ahazipo. Sasa hawa ndo wasanii wa kutuletea maendeleo? Je watawezaje kufichua uovu unaoendelea kwenye jamii? Nilickitika saana na kupata hacra baada ya kuona watu wazima wanacheza mduara-maana ya hii ni nini? Na hii inaleta picha gani kwa mabalozi wetu wanaotupigania kupata misaada kutoka kwenye nchi zao? Da cna la ziada maana na machozi yananilenga wana JF nilivyoona jinsi gani maskini wa tanzania atakavyoendelea kuwa maskini cku zote bila kunyanyuliwa kutoka pale alipo.

Baada ya kuyasema haya machahe niaongelee uteuzi. Cku zote mwenye hela huwa ana nguvu zaidi na ndiyo maana kwa uwezo wa mwenyezi mungu tu-Mheshimiwa Lowassa alijiuzuru, Ila naamini wote tunajua makosa yake wana JF na hilo ni moja tu-Na je yale ambayo hatuyafahamu ni mangapi? Pamoja na hayo yote bado anaungwa mkono na wana CCM Na kuna watu bado wanaamini kuwa alionewa. Mzee Bilali mimi nina uhakika ya kuwa atafanya kazi yeye kama yeye hataburuzwa na mtu na hii italeta changamoto ktk utendaji wa kazi za Kiongozi wetu mkuu maana yeye c anasafiri? Basi nchi atakuwa anaiongoza bilalil-Yatakayotokea tuombe uzima tuone wenyewe.

Kuhusu Dr Shein-yule mzee kaonewa saana c Wakati wa Mkapa na wala c Wakati wa Mzee Jk , as if he was not there at all-Lakini ukimya wake ulikuwa wa maana saana . Na yeye alitaka apate fursa ya kufika mahali kuwa ndo msemaji mkuu bila ya kushauri. Maana ukishauri c lazima ulichoshauri kikubaliwe na kukataliwa ni mojawapo ya matokeo. Kwa kuwania kiti hiki cha uraisi nampongeza saana-Tuseme ukweli ana utu na uzalendo kwa watanzania. Na naamini atatenda kazi zake ipasavyo.

Kwa kumalizia tu naomba walau mwaka 2015 tupate kiongozi bora , maana wanaotajwa tajwa naona bado jamani-Naamini tanzania ina watu wengi wenye busara,wapenda maendeleo na wanaochukia na kuumia wakiona mtanzania anateseka na hao watu ndo tunataka mungu awainue kwa ajili ya kuiongoza Tanzania. Mimi huwa naamini kuwa tukipta mawazir kama watano wenye kusimamia yale wanayoyasema kama magufuli ,tutapiga hatua-hatutakuwa hapa tulipo tena. Mimi naamini hivyo.

Nawakilisha
 
MM, mimi nadhani hawa jamaa wa CCM walitaka kucheza karata za kisiasa, karata za kutuliza mambo visiwani. Kwa jinsi ilivyo walitaka kutuliza kiu ya wapemba ambao wamekuwa wakilalamika kuwa hawapati nafasi za uongozi a.k.a urais. Tatizo ni kuwa CCM hawapo tayari kumpa mgombea wa CUF nafasi kama hiyo, kwahiyo Shein akatumwa kwa vile anaonekana kuwa na sifa hata kama si lazima ziwe za kweli. Kwa bahati mbaya Seif anatoka pemba kwa hiyo njia nyepesi ya kupunguza au kugawa kura za pemba ni kupitia Shein. Hapa ndipo karata mbovu ilipochezwa kwasababu unguja kwa mazoea wanadhani ndio wazanzibar na rais lazima atoke hapo. Kitakachofuata ni CCM kupoteza majimbo ya unguja kwa kura za hasira.
Kama upinzani ungekuwa unajua kusoma alama za nyakati hili la dodoma ni ''gross mistake'' na wange tumia fursa hii kuingia ikulu kiulaini. Bahati mbaya hakuna mkakati wa hilo. Nasema hakuna mkakati kwasababu hata huku bara upinzani umedoorora. Kama ingelikuwa nchi za wenzetu wanaojua kucheza na politics JK asingerudi magogoni. JK amezungukwa na ushahidi wa kutosha kabisa kuwashawishi wananchi kuwa ameshindwa kazi lakini wapinzani wamelala hadi october 22 ndipo waanze kampeni.
Mfano mzuri kama JK antumia data za kupika kuwa uchumi umekuwa kwa asilimia 6.4 kwanini wapinzani wasiwaambie wananchi kuhusu inflation toka 7 hadi 11.
Kwanini wapinzani wasitumie data kuonyesha mamilioni yanavyotafunwa!
Kwanini wapinzani wasieleze uzembe wa serikali kama kupoteza bilioni 200 kwa fuel adulteration
Kwanini wapinzani wasieleze wananchi kuwa fenicha :sick: za ofisi moja zinajenga zahanati.
Kwani wapinzani wasieleze wananchi kuwa hela za vitafunio vya chai ni kubwa kuliko thamani ya vijiji vyao.
etc etc etc....

Wapinzani kama mtaenda na sera za kinadharia asilimia 70 wanafuata mkumbo na hawatawaelewa, waambieni wananchi uhalisia wa maisha yao na umasikini wao na si wa taifa. Nina uhakika ukimweleza mwananchi kuwa thamani ya VX moja ni sawa kujenga madarasa 50 au zahanati 10 watawaelewa. Lakini si Singara wala zinduka hatuzisikii tena.
This year was an opportunity to reclaim our country from fisadi but it seems as if we have long way to go.

Haya ni maoni yasiyokuwa na ukweli wowote, kwani Tz sio Europe au America ambako watu ni waelewa na ukiwaeleza ukweli unapata ushindi. Huu udhaifu wa CCM unaosema wapinzani wanatakiwa kuwaeleza wananchi ni vitu ambavyo viko obvious (kwa wananchi wa nchi zenye mwamko) hata havina haja ya kuambiwa na mtu! By the way upinzani ni nini kama sio sisi wananchi tunaoathirika na huu utawala mbovu wa CCM? Tatizo la Tz ni kuwa watu (haswa wewe) tunataka mabadiliko yaletwe na wachache (viongozi wa upinzani of course) huku wenyewe tumekaa pembeni na kuangalia kama sinema.....
 
PASCO, you have nailed it!!!! HIli ni somo zuri sana na natumaini kwamba Mwanakijiji amekusoma vilivyo.... The biggest problem ya upinzani ni kukosa mwelekeo especially when it comes to common enemy!!!

De Novo hivi kweli wewe unaona unaweza kuungana na akina mrema na kundi lake waliokuwa wakitukanwa pale Dodoma huku wakiwashangilia mabwana zao? Siamini kwamba Chadema hawataki kuungana na opposition parties zingine lakini jambo hili linatakiwa kufanywa kwa uangalifu la sivyo mchezo wote waweza kuonekana wa sanaa kabisa. Nadhani unaelewa nini nasema.
 
Haya ni maoni yasiyokuwa na ukweli wowote, kwani Tz sio Europe au America ambako watu ni waelewa na ukiwaeleza ukweli unapata ushindi. Huu udhaifu wa CCM unaosema wapinzani wanatakiwa kuwaeleza wananchi ni vitu ambavyo viko obvious (kwa wananchi wa nchi zenye mwamko) hata havina haja ya kuambiwa na mtu! By the way upinzani ni nini kama sio sisi wananchi tunaoathirika na huu utawala mbovu wa CCM? Tatizo la Tz ni kuwa watu (haswa wewe) tunataka mabadiliko yaletwe na wachache (viongozi wa upinzani of course) huku wenyewe tumekaa pembeni na kuangalia kama sinema.....
Kinacho takiwa mkuu ni uhamasishaji kutoka kwa waelewa ambao kwa bahati ghafi ni wanasiasa ambao hawatambui wajibu wao mbele ya jamii ya Kitanzania ambao wengi wao wanaishi vijijini ambako vyombo vya habari havifiki kwa asilimia zote....! Bado lawama zitawaendea wao mpaka watakapo badilisha mwelekeo wao wa kudeka deka.
 
Jasusi kaka yangu, hii ni rai nzuri sana, lakini je hao CHADEMA wako tayari kuungwa mkono na wapinzani wote?? wewe huoni kwamba tayari wao vichwa vyao vimekua vikubwa kuliko uwezo wa shingo zao wakati bado ni neonates kwenye siasa hizi za majitaka??

Je huoni kwamba hii rai ni vizuri ingetoka kwa CHADEMA wenyewe , washuke chini, wawe humble na wa-extend their hands to reach out to other opposition parties??

si hawa CHADEMA baada ya mawe ya muda mfupi tu hapa jamvini wali-succumb na kuliacha jahazi hili lenyewe??

I PRAY FOR CHADEMA TO COME BACK AND EXTEND THIER INVITATIONAL TO ALL OPPOSITION PARTIES ili common enemy awe addressed, IMO, i wish for opposition kusimamisha mgombea mmoja tu kila jimbo ili apambane na wa CCM and that means kura za maoni kwa kila jimbo kwa wapinzani zipigwe pamoja na nomination moja
De Novo,
CHADEMA may be not perfect. But it is the only serious opposition party we have here so far. Wapo hapa akina Mnyika, Mchukia Fisadi, Mzee Slaa mwenyewe, ujumbe umewafikia. Sidhani kwamba kama NCCR au CUF wangekuja na pendekezo lisilohusisha personalities, kuhusu mstakabala wa nchi yetu na jinsi ya kuiondoa nchi kwenye makucha ya CCM kwamba CHADEMA watasita kuwasikiliza. Lakini sijaona. CUF wanaonekana kuwa more comfortable with the CCM status quo, labda kwa sababu ya muafaka wa Zanzibar. What about the mainland?
 
De Novo hivi kweli wewe unaona unaweza kuungana na akina mrema na kundi lake waliokuwa wakitukanwa pale Dodoma huku wakiwashangilia mabwana zao? Siamini kwamba Chadema hawataki kuungana na opposition parties zingine lakini jambo hili linatakiwa kufanywa kwa uangalifu la sivyo mchezo wote waweza kuonekana wa sanaa kabisa. Nadhani unaelewa nini nasema.

Nakuelewa sana mkuu.... lakini wanasema mchawi mpe mwana akulelee, na ndivyo kikwete alivyofanya kwa bilal [just my assumption though]... PAmoja na tamaa ya mrema kuwa maarufu, au tapeli chenge nk. simply kwa kuwa wao ni wapinzani, then wako kwenye fungu moja na ninyi, wote mnaitwa vyama vya upinzani na generic name yenu ndiyo hiyo!!

Dawa ni kuendelea kuwaalika, kutangaza umoja na kuwapa nafasi, taratibu utaona changes... kuwaacha peke yao si suluhisho kwani ndio wanaonyesha jinsi wapinzani wasivyo na umoja

ukiwa na ndugu kichaa utamkana???
 
Bulesi,
Mkuu hii habari ya mkutano wa NEC na kusema Bilal hivi ama vile ni utata tunavyoona sisi lakini sii kwa CCM..Picha nzima ilisha chorwa ubaoni kilichotokea ni kuwakilisha tu..

Hawa kina Salmin lazima waje kwenye CCM convention kama miaka yote iliyopita wala sii jambo geni. Bilal alikataliwa wakati wa Mkapa na Karume akachukua Urais wa Zanzibar hivyo hakuna Uadui baina ya Bilal na Kikwete wote hawa walitoswa pamoja na kuwa walikuwa chaguo la wananchi, tena naweza kusema Kikwete ndiye kamwezesha Bilal kuwa hapo alipo leo laa sivyo yangekuwa ya Salmin mwenyewe.

Ujue Siasa ni mchezo mchafu kama Chess vile.. kete zilishapangwa mapema haya ni matokeo ambayo tayari wazee wa CCM waliisha yapanga kwa sababu utawala wa nchi zetu ndio kazi kubwa na ngumu kwao (wanasiasa) kuliko kutekeleza sera. Na swala la Shein kugombea limeepusha mengi sana ikiwa ni pamoja na wapinzani wengi wazee wa visiwani toka kina Nassor Moyo hadi Salmin wote wamekuja afiki baada ya kupewa picha nzima.

Why JK amepata asilimia 98 pasipo mshindani unafikiri hakuna watu wanaompinga?..Na zaidi ya hapo itazame picha nzima utajua wenzetu wamejipanga toka kina Nahodha, Khatib na wengine woote hawa wana nafasi zao pamoja na kwamba wangependa sana kuchukua madaraka. leo hii JK ana nguvu ya kusema Nahodha hujakomaa kama alivyosema mwalimu kwa JK..

Kasheshe,
Mkuu naelewa rais ni rais lakini tunavyoambiwa na siasa za nyumbani Zanzibar sio nchi wala Taifa, hivyo madaraka yake sii sawa na Senate au Premier ni kama tenga la kuvunia. Ndio sababu ya kuuliza kama kiutawala ameshuka au...Ilikuwa nyongeza tu ya kuxchemsha baraza!

Kusema kweli binafsi siafiki kabisa mpango huu wa meza kubwa ambapo Rais wa Jamhuri ananakuwa na mwenza (makamu wa rais) toka visiwani kisha visiwani nao kuwa na rais wao ambaye pia anakuwa na waziri kiongozi.. Yaani uongozi wa nchi hii umepangwa kwa tabaka za Uraia hivyo ni vigumu sana kufanya itikadi kuwa msingi wa kuunda upinzani isipokuwa Uuwiano kuwa msingi wa utawala wetu. No wonder wanawake wanataka nao wachukue Bunge kwa asilimia 50 na Wenye Udini wanataka kuona mabadilishano ya kiti cha Ikulu kutokana na imani ya dini.
 
HTML:
Kinacho takiwa mkuu ni uhamasishaji kutoka kwa waelewa ambao kwa bahati ghafi ni wanasiasa ambao hawatambui wajibu wao mbele ya jamii ya Kitanzania ambao wengi wao wanaishi vijijini ambako vyombo vya habari havifiki kwa asilimia zote....! Bado lawama zitawaendea wao mpaka watakapo badilisha mwelekeo wao wa kudeka deka.

Sijui ni hapa kwetu tu au na kwingineko Duniani, najiuliza kwa nini Siasa siku zote imeangukia kwenye mikono michafu, angalia Kina Bilal (Mla rushwa wa scolarship wakati ule leo anakuwa VP) kina Chenge, Lowasa, RA na wengine wengi kurasa elfu moja na zaidi. Hata waliokuwa wasafi sasa wamekuwa wamoja wao, maana ni wachache na wengine wameamua kuchafuka, kina BWM, kina Kingunge, Kina...
Hivi kweli Nchi yetu ni ya kupewa Bilal as VP? just kwa sababu ya maslahi ya kundi dogo la CCM?
 
Mkuu ndio maana wanasema Miafrika Ndivyo Tulivyo.. wee nenda kwenye madance huko utasikia wakisifiwa wezi na majambazi wakitangazwa wakati ngoma inachemka kweli kweli...Hatuna role model isipokuwa wale wenye kutunyanyasa na fedha zao...
Kisha tomeisha zoea Umaskini hatuna depression wala mjomba wake tunapeta tu, sawa na watu wanaokoga kisima cha maji machafu..Ni kazi kubwa kuwaambia usafi wa maji ya ziwa au Bomba.
 
Back
Top Bottom