Kwa ufupi: Bilal alikuwa aondoke CCM...

Bilal ni moja kati ya nguzo za mshikamano wa CCM Bara na Visiwani hasa pale inapofikia juu ya uteuzi wa mgombea wa nafasi ya Raisi wa Zenj, kumbwaga ingewezekana kama ilivyofanyika mwaka wa 2005, ila kule kwetu hakuaminiki na lolote lingeweza kutokea au litatokea juu ya uamuzi huu waliouchukua CCM bara nasema hivyo kwa sababu ya uwezo wa kumpitisha mgombea yeyote hata kama Zenj hawamtaki kama ilivyofanyika mwaka wa 2000 ambapo kura zilishapigwa na matokeo yalibatilishwa DOM, Mzee Mwan.... Bilal ni mvumilivu angelibaki tu, vilivile alilenga mwezi ndo maana aliangukia kwenye nyota alipoukosa.
 
Amekuwa ni chaguo lisilo chaguo; chaguo lililojichagua na kuchaguliwa. Ilikuwa ni "Urais au nothing". Bilali hakuwa na uamuzi wa kurudi bila ya kitu kinachokaribiana na urais. Uamuzi wa Shein kugombea Zanzibar umekuja baadaye sana baada ya kuona kuwa mtu pekee mwenye nguvu Zanzibar kuweza kumrithi Karume ni Bilal hao kina Nahodha na wenzake walikuwa ni wasindikizaji tu.

Hata hivyo Bilal kwa sababu wanazozijua wao alikuwa tayari anaigawa Zanzibar na kugombea kwake Zanzibar kungempa ushindi mwepesi tu Seif. Lakini hakuwa tayari kujitoa safari hii na alijua kabisa nguvu pekee anayoshindana nayo ni ya Rais wa Jamhuri ya Muungano.

Lakini alikuwa anajua vile vile kuwa JK ni dhaifu kwenye masuala magumu. Alijua JK hawezi kufanya kazi kukiwepo na dissent ya kweli ndani ya CCM, dissent ambayo kwa mara ya kwanza ingewapa ushindi rahisi zaidi Zanzibar. Lakini kilichoharibu ni wajumbe wa kutoka Zanzibar walioamua kuondoka juzi kwa hasira kurudi Zanzibar wakiwa na dhamira moja tu nayo ni kuhakikisha Shein hashindi visiwani.

Lakini JK ni mwanasiasa ambaye anatumia nafasi zinazojileta kuzuia migogoro, yuko tayari kumuachilia mtu wake wa karibu aanguke (kama linamletea yeye sifa) na kama kumleta karibu mtu ambaye ni tatizo kwake.

Sasa, Bilal ni chaguo lililojichagua; hawakumpa nafasi JK kumchagua mtu mwingine, asingeweza kumchagua mtu mwingine; hakukuwa na uwezekano wa kumchagua mtu mwingine.

Ni jinsi gani hawa wawili watafanya kazi? Ni jinsi gani wataweza kupatana?

Well.... Wamarekani wanasema... "Politics make strange bedfellows"..

Historia itaamua.

MM
.
Mzee Mwanakijiji, in politics, hakuna permanent friends au permanent enemies, only convenience. Bilal was an enemy, ili kushinda vita, keep close your friends, and enemies even closer, so they can't trike you.

Shein alitumwa ili kuunusuru muafaka baada ya Bilal kupiga kampeni ya wazi wazi, atapiga no kwenye referendum. Baada ya Shein kupita, wakapima upepo, na kujaribu kupima vumbi atakalorudi nalo Zanzibar, ndipo wakaamua bora wampooze, vinginevyo hakuliki wala hakulaliki.

Mambo mawili yatafuata.

La kwanza, kama Bilal alikuwa anautaka urais wa Zanzibar kwa nia ya dhati, then hata huu umakamo kwake ni boya tuu, hivyo he will still hit'em hard! na wafuasi wake hata back down kwa kilemba cha ukoka cha U VC, hivyo mushindi ni kwa Seif.

La pili, kuna uwezekano mkubwa Bilal kaahidiwa 2015 anarudi Zanzibar, Shein anakuja Bara, Membe ndio VC, hivyo atavumilia, kwa kujifariji na ving'ora na mafao kwa miaka 5 tuu, hivyo atawapooza wafuasi wake ili kuipa CCM ushindi.

Kwenye vita, ni do or die, Bilal aliamua to do mpaka afe, ila pia unapofika mahali ukagundua adui yako ana nguvu kuliko wewe, na ukiendelea kupigana ni hakika utashindwa na utaishia kujifia kibudu, the better join them au ili tuu uendelee kuishi na manung'uniko moyoni, ama ili kujitenga upya, ukishajihakikishia una nguvu za kutosha, ndipo uta strike again.

Bilal baada ya kushindwa, kakubali yaishe, ame wa join them now against one common enemy CUF.

Na hivi ndivyo mnavyovyakiwa kufanya na CCJ yenu, ama join them ama tuunganishe nguvu against common enemy, other wise, we are doomed and will remain doomed!.
 
Yaani watu wanachezea hii nchi na watu wake....mambo ya cheap politics na kutafuta majibu mepesi kwa maswali mazito.....Lets wait n see!!
 
Du!!! Ina maana mzee mzima katishiwa nyau akatishika??? Hii ni hatari kwa kiongozi mkuu wa nchi. Kwa hiyo ina maana kuna maamuzi mengi tu huwa hayafanyi kwa maslahi ya nchi bali kwa kutishiwa nyau. Haaaaaaa!!!! Hu si uanaume bwana??? Tanzania ilipofikia sasa inahitaji kiongozi jeuri asiyesikia vitisho vya wazee wala watoto bali anayeweka mbele maslahi ya nchi. Bahati mbaya tangu Nyerere aondoke hatujampata kiongozi kama huyo. Lakini siku chache zijazo KITAELEWEKA tu.

Sasa kama rais na makamu wake wako kama paka na panya nchi itaendeshwaje kama si usanii mtupu!!!
 
Your are oppressed when u grant ur consent...bilal alidhamiriaa kukomaa nao mpaka kielewekee..nampongeza kwa hilo.

JK kwa mara nyingine na ya mwisho ameshindwa kusimamia chaguo lake la VP anayemtaka! 2005 kwa shein alitishia nyau anataka mtu wake, wazee wa chama wakamwambia mwache shein akamilishe na aunganishe awamu ya tatu na ya nne!!!

Leo kaambiwaa Bila Bilal Zenj hakitaelewekaa, kabwaga manyanga!!!
 
UKIWEZA JINYONGE, UKICHUKIA CHUKIA , UKILIA LIA. LKN HAMNA AWEZAE KUYAPANGUA YA MUUMBA WETU
"JK TU 2010"


Hii signature ya Malaria Sugu inaonyesha kuwa huyu muungwana ni kada mkubwa wa kijani na njano
 
Hii itakuwa ni mara ya pili kwa JK.
Kuna fununu zinasema hata 2005 hakuwa anataka asimame na Dr.Shein ila 'wadau' wakamwambia hamna jinsi ni lazma asimame nae,na akasimama nae kwa shingo upande.
 
UKIWEZA JINYONGE, UKICHUKIA CHUKIA , UKILIA LIA. LKN HAMNA AWEZAE KUYAPANGUA YA MUUMBA WETU
"JK TU 2010"


Hii signature ya Malaria Sugu inaonyesha kuwa huyu muungwana ni kada mkubwa wa kijani na njano

Ni kweli kabisa. Kama wewe ni mfuatilia mzuri sana wa JF Jukwaa la siasa. Hakuna siku yaweza pita bila huyu bwana kutaja jina la JK. Yaani ni sawa na mimi siku ipite bila Kumsifu mume wangu.

The problem with this guy. he Doesnt have scientific reaosning why he loves Jk or CCM!!
 
hata kuwekwa kwa Shein pale hawezi kupata kura za watu wa Pemba. Wapemba watamchagua Seif tu(CUF)........na Watu wa Unguja walio CCM watashindwa na wa kumchagua since wasingependa kuchagua mtu kutoka Pemba.

Badala ya kuwa kumetafutwa suluhu inaweza ikawa ndio imeharibu kabisa................hapa ni kusubiri na kuona, lakini once uchaguzi umefanyika na Shein akashindwa (kama wanavyoshindwa ccm kila mwaka znz), itakuwaje?

CCM wa zanzibar wanaomuona Shein kuwa si ccm kamili watamhukumu vipi na watachukua hatua gani?

huu ndio kwanza mwanzo.............
 
niliwahi kuwaambia hapa kuwa unafiki ni mbaya sana. jana jk alikuwa hana pa kutokea isipokuwa kutaja jina la Bilal

ila kuna watu wameniudh sana hapa jf, huwa wanapinga sana sera za ccm na jk wake hapa janvini lakini juzi na jana walikuwa dom na tena wanariport hapa janvini yanayojiri. Wanafiki wakubwa

heri malaria sugu aliyejiweka wazi
 
Wakuu,

Nina uhakika Bilali will feel gud kwa uraisi wa Zanzibar.
Kuna kitu alitaka kufanya waondokane na ukoloni (Bara)

Surely he is not dump, he know amepewa ili wam-contain, he will strike them hard!!
 
ila kuna watu wameniudh sana hapa jf, huwa wanapinga sana sera za ccm na jk wake hapa janvini lakini juzi na jana walikuwa dom na tena wanariport hapa janvini yanayojiri. Wanafiki wakubwa

heri malaria sugu aliyejiweka wazi
Mkuu Edson, Natanguliza heshima:

Fafanua. Utawezaje kupinga sera ukiwa gizani? Lazima uwepo kama mshiriki 'hasi' hili uweze kusikia yanayojiri toka kwenye kinywa cha 'farasi'!
 
Asnte mkuu Nyunyu. Ki-ukweli Kikwete si mtu mwenye msimamo wenye nguvu ya hoja. Hao wanaoitwa 'wazee' wa chama wanafahamu udhaifu huo. Ndio maana kila JK anachofanya wanaweza kumsambaratisha kirahisi na kuhakikisha chama kinaendelea kushika hatamu sic! Tabia sugu ya JK ni kukurupuka na kutoshaurika hivyo kwa hili la Bilal wasilaumiwe washauri, ilaumiwe tabia ya JK ya kuwa kiongozi asiyeweza kuona mbele na kuongoza. Bilal bado anaonekana kuwa kiongozi thabiti na wakifanya chezea...watakipata mbele ya safari
 
niliwahi kuwaambia hapa kuwa unafiki ni mbaya sana. jana jk alikuwa hana pa kutokea isipokuwa kutaja jina la Bilal

ila kuna watu wameniudh sana hapa jf, huwa wanapinga sana sera za ccm na jk wake hapa janvini lakini juzi na jana walikuwa dom na tena wanariport hapa janvini yanayojiri. Wanafiki wakubwa

heri malaria sugu aliyejiweka wazi

Mkuu,

Information is power, how do you fight bila kufanya wrecking!!!
Lazima tujua adui yetu anafanyaje mambo yake, kuweza kuweka strategy vizuri.

Hii siyo shida bana!
 
niliwahi kuwaambia hapa kuwa unafiki ni mbaya sana. jana jk alikuwa hana pa kutokea isipokuwa kutaja jina la Bilal

ila kuna watu wameniudh sana hapa jf, huwa wanapinga sana sera za ccm na jk wake hapa janvini lakini juzi na jana walikuwa dom na tena wanariport hapa janvini yanayojiri. Wanafiki wakubwa

heri malaria sugu aliyejiweka wazi
Edson, sio lazima wawe ni wanafiki, wanaweza kuwa ni maripota tuu, kazi yao kuripoti kinachojiri, hivyo hata kama hukubaliani na JK na CCM yake, when it comes to facts, JK ndie rais wako, wangu, wa Lipumba, Seif, Chadema etc na CCM ndicho chama tawala, tukipende tusikipende, tukikubali, tusikikubali, ila facts ndizo hizo.

Kwa mfano mimi binafsi, CCM inanitia kichefu chefu, lakini bado ningekuwepo Kizota jana, ningeripoti kinachojiri, na labda hata ku appreciate jinsi JK alivyokuwa anayarudi kwa pride jana baada ya kumaliza mkutano wao, na bado nikirudi forum kwenye opinioni, napinga nyundo za kufa mtu.

Au japo sio mwana CCM na sio mwana Chadema, au sina chama chochote ninachoshabikia, siipendi CCM kutokana na marorosa yake, bado hiyo Octoba 31, naweza kujikta nalazimika kuichagua CCM hiyi hiyo mbaya na uoza wake, simply because sijaona chama kingine chochote cha kuchagua, kwa mtindo wa heri zimwi likujualo, ndio maana nimekuwa nikisisitiza sana, Watanzania wengi, wemeichokav sana CCM, ila kwa vile wapinzani hawajajiaminisha, CCM, itaendelea kuchaguliwa.
 
Historia imejirudia kwa mara nyingine JK analazimika kutekeleza chaguo la CCm na sio Chagua lake, mwaka ule alilazimishwa kumteuwa Shein kama running mate wake na mwaka huu kalazimishwa amteuwe Bilal!
 
niliwahi kuwaambia hapa kuwa unafiki ni mbaya sana. jana jk alikuwa hana pa kutokea isipokuwa kutaja jina la Bilal

ila kuna watu wameniudh sana hapa jf, huwa wanapinga sana sera za ccm na jk wake hapa janvini lakini juzi na jana walikuwa dom na tena wanariport hapa janvini yanayojiri. Wanafiki wakubwa

heri malaria sugu aliyejiweka wazi



:wink1: hakuna rafiki au adui wa kutumu kwenye siasa! huo ndio ubaya wa siasa. usipokuwa mnafiki utaambulia public defeat.
 
du!!! Ina maana mzee mzima katishiwa nyau akatishika??? Hii ni hatari kwa kiongozi mkuu wa nchi. Kwa hiyo ina maana kuna maamuzi mengi tu huwa hayafanyi kwa maslahi ya nchi bali kwa kutishiwa nyau. Haaaaaaa!!!! Hu si uanaume bwana??? Tanzania ilipofikia sasa inahitaji kiongozi jeuri asiyesikia vitisho vya wazee wala watoto bali anayeweka mbele maslahi ya nchi. Bahati mbaya tangu nyerere aondoke hatujampata kiongozi kama huyo. Lakini siku chache zijazo kitaeleweka tu.

Sasa kama rais na makamu wake wako kama paka na panya nchi itaendeshwaje kama si usanii mtupu!!!
siasa ni mchezo mchafu
 
Back
Top Bottom