Kwa polisi hawa je, tutafika?

May 21, 2011
33
11
Kama mfanyabiashara nimekuwa nikisafiri mara kwa mara na kushuhudia magari yakikamatwa na trafiki polisi ambao mimi ninawaita polisi rushwa kwa tuhuma mbalimbali kama vile speeding, gari kuwa chafu, bima kuisha, madereva kutokuwa na leseni, breki zenye matatizo, nk. Hata hivyo sijawahi kushuhudia hatua zozote za kisheria zikichukuliwa dhidi ya wahusika. Polisi rushwa hawa huwa wana vidaftari ambavyo baada ya gari kusimamishwa huchorachora ndani yake wakijidai kwamba wanaorodhesha makosa ya gari husika. Hata hivyo baadaye kidogo utashuhudia gari linaondoka baada ya makondakta kwenda pembeni na polisi rushwa ambapo rushwa hutolewa. Kwa nn polisi rushwa wanatamba mchana kweupe kwa kula rushwa waziwazi? Matokeo ya rushwa hizo ni kuwa polisi hawa ni wanene zaidi ya wenzao, wanameremeta zaidi ya polisi wenzao, wanasomesha watoto wao kwenye rushwa ambazo pia kuna watoto wa mawaziri kama SAVANNA PLAINS INTERNATIONAL SCHOOL (SHINYANGA) kwa karo tshs 7 milioni kwa mwaka, wana mali na magari mengi kuliko hata IGP MWEMA... yaani wamekubuhu kwa rushwa na ni matajiri wa kutupwa. Matokeo mengine ya rushwa hii ni vifo na uharibifu mkubwa wa mali za wananchi kupitia ajali zinazozuilika kabisaaaaaaaaaa: hakuna haja ya kufanya utafiti kubaini kuwa karibia 90 asilimia ya magari Tanzania hayapaswi kuwa barabarani (not road worthy) kwani ni mabovu, machafu nk. Lakini kwa sababu ya rushwa magari haya yako bara2ni na matokeo yake ni hizi ajali ambazo kwa sasa zinaongoza nchini kwa kusababisha vifo: vifo vya ajali vinazidi vifo vinavyosababishwa na malaria au UKIMWI nk. Kinachosikitisha ni kuwa polisi rushwa wamehalalishwa kula rushwa: hawashughulikiwi kabisaaaaaaaaaaaa, si na TAKUKURU wala na polisi wakubwa.

Polisi rushwa hawa ni janga kwa taifa changa la Tanzania na ni lazima washughulikiwe kisayansi ama sivyo, tutakwisha. Mbinu za kushughulikia rushwa hii ni pamoja na (1) TAKUKURU iamke na kutumia sheria yake PCCA namba 11 ya 2007 vifungu 26 na 27 vya limbikizo la mali kwani mali za polisi rushwa ni za kifisadi na hazielezeki; (2) IGP MWEMA atumie PGO kuwashughulikia baada ya kutuma taarifa za kiintelijensia kukusanya taarifa za mienendo na mali zao; na (3) kuunda kitengo cha ukaguzi wa magari nje ya polisi (Directorate of Vehicular Inspection au Transportation Safety Board) ambacho kitakuwa na wataalamu waliobobea wa mambo ya MAGARI na kitakagua magari kwa mujibu wa ratiba na kujaza fomu maalumu ya ukaguzi (ambayo dereva atamuonyesha polisi rushwa pale atakaposimamishwa na kuruhusiwa kuendelea na safari) siyo kila siku kama ambavyo polisi wanafanya kwa sasa ambapo ukitoka Mwanza kwenda Dar gari linaweza kusimamishwa na kukaguliwa mara 20 wakati wa safari hiyo... huu ni mwanya mkubwa sana wa rushwa na kikwazo kwa maendeleo ya nchi yetu. Hili la (3) ni muhimu sana kwani (a) polisi hawana wataalamu wa ukaguzi wa magari na ndiyo maana ukaguzi wao siku zote ni wa mambo madogo2 kama gari kuwa chafu na gari kuchubuka rangi. Polisi std vii au kidato iv hawana utaalamu wa ku-overhaul engine na kuona matatizo yake kwa mfano na ndiyo maana kwa wao kinachosababisha ajali siku zote ni mwendokasi (tazama kipindi seconds from disaster kwenye national geographical channel ili ushuhudie ajali zinavyochunguzwa, na siyo mwendokasi pekee ndicho chanzo cha ajali ); na (b) utaratibu huu utaziba mianya ya rushwa ktk utaratibu wa polisi kukagua magari kila siku gari linapokuwa bara2ni badala yake, kama mataifa mengine yanavyofanya, polisi watasimamia ratiba za ukaguzi wa magari kwa mujibu wa ratiba na wala sio wao wenyewe kufanya ukaguzi huo.
 
Back
Top Bottom