Kwa nini watumishi wa serikali hawaendi kugombea ubunge kupitia upinzani?

Ngalikivembu

JF-Expert Member
Oct 6, 2010
1,959
872
Nimekuwa nikijiuliza kwa nini watumishi wengi wanapoamua kugombea ubunge wanakimbilia ccm tu na si upinzani kama cdm hivi?wanaogopa?kwani sheria inawakataza kugombea upinzani?au kuna tatizo?na je akishindwa kupata ubunge huo hatarudishwa kazini?maana katika wale ninao wafahamu walowahi kufanya hivo ni dr mvungi aliye gombea urais 2005.kuna siri gani zaid hapa wanajf?
 
kwasababu wengi hawana shida na sera za CCM, CCM ki chama inashida na baadhi ya viongozi wake waliooza kupindukia..., CDM wanahitaji kuimarisha network na kujaribu kuunganisha vyama vingine labda watapata wengi zaidi
 
Wanapenda vya urahisi -- kwa mawazo yao wanadhani wakigombea wakiwa CCM serikali ya chama hicho kitaiba kura ili washinde -- kitu ambacho siku hizi kinaanza kuwa kigumu.
 
Zimebaki siku chache tu kabla hawaqjaanza kufanya hivyo... uwoga unaanza kuondoka sasa
 
so far navyoelewa ni kwamba ukigombea kupitia ccm unakopeshwa muda na sio kuacha kazi kama ukigombea kupitia upinzani.then ukimaliza muda wa kula nchi wanarudi kazini kama kawa ila upinzani haurudishwi kazini.ccm ni mafisadi waizi n[ wadhulumati:msela:
 
Mkuu kabla hujarukia watumishi wa serikali umewahi kujiuliza pia ni kwanini wananchi wengineo nao wanakimbilia ccm? kuku dhihirishia hilo ndio maana majimbo na kata zote ccm imesimamisha wagombea wakati upinzani kuna majimbo na kata kibao hawakusimamisha wagombea sababu hawakujitokeza kugombea.
Hapa sidhani issue kama ni watumishi bali ni jamii nzima kwa ujumla wanahofu kugombea upinzani bila kujali mtumishi au mwingine.
Na kwa mtazamo unaouchukulia wewe naona wafanyabiashara wakubwa ndio waoga zaidi kugombea upinzani.
 
wanaogopa kuonekana wasaliti pia wanalinda ajira zao maana wakishindwa wengi hurudishwa kwenye ajira zao
 
Hii mada naomba nichangie. Mi naona ni kuwa wengi wao wanasiasa wa TZ hawana wanachoamini (conviction) wala hawana falsafa. Wanagombea kwa maslahi binafsi tu, hawana cha kutimiza zaidi kuangalia vp watapata chakula chao. Wanalipa fadhila kwa kuonekana kwenye misiba, kutoa rambirambi hela nyingi, kuchekacheka na wananchi wao ili wawaone wema, na pengine kuwalipia ada watoto wa wapiga kura wao wanapokwama ada (toka mifukoni mwao). hawana miradi ya maana kuondoa umasikini uliokithiri wa wananchi wao ili wananchi wajitegemee wenyewe. Wale wanaotokea serikalini kama watumishi wanaogopa wakikosa ubunge watakuwa hawana pa kukimbilia, kwa vile serikali ni ya CCM kwa kiasi kikubwa hadi sasa. Pia utawala wa sheria hauko imara kulinda maslahi yao kama wataonewa wakirudi ofisini baada ya ubunge au wakikosa kupitia upinzani. Ktk hali hii tutajaza wanasiasa opportunists tu.
 
CCM wanapenda sana kubaka demokrasia! Ukigombea upinzani hawakupi ile likizo isiyokuwa na malipo lakini ukiwa upande wao unapewa likizo ukishindwa unarudi kazini sasa hiyo inakuwa ngumu kwa watumishi kuamua hilo. Kuna jamaa yangu aliwahi kugombea upinzania jimbo moja hivi akapata kiti hicho kwa vipindi viwili mfululizo lakini alipoanguka uchaguzi wa 2010 hakurudishwa kazini maana jamaa walikuwa wameshamfukuza kazi tayari.
 
Back
Top Bottom