Kwa nini wasanii wengi wa Tz wanapenda kuimba nyimbo za kulalamika?

tindikalikali

JF-Expert Member
Jan 14, 2011
4,855
1,117
Kwa nini wasanii wengi wa Tz wanapenda kuimba nyimbo za kulalamika?

Malalamiko mengi ni kuachwa au kukataliwa kisa pesa...kilio kimekuwa ni pesa pesa..umasikini......ebu tujikumbushe hawa wachache....

1. Barua ya Daz nundaz.....jamaa alitoswa kisa pesa.....katika ile barua inasomeka " kumbuka ufukara umasikini kututenga vimechangia hilo usipinge bwana, sasa nani alaumiwe unadhani..hivi punde mi nataraji kufunga pingu maishani ili niishi maisha yaliyo ya juu tena kama almasi katika barua hii nimeambatanisha na kadi hii ya mwaliko ni yako''.........hitimisho ni hili..."aliyemjalia yeye ndiye aliyenipa mimi ufukara".........

2. Umsikini wangu wa Q-chief.....japo aliboronga katika uhandishi bado alieleweka kilio chake...."alidai umasikini wake ndiyo uliomponza na kumfanya akose mke"

3. ukisikiliza Wasi wasi ya Banana bado ishu ni umasikini...watoto wamependana lakini kikwazo kipo kwa wazazi....."naamini kama wanipenda lakini moyoni ninawasiwasi bado kutokana na tofauti baina yangu mimi na wewe"

4. Pia Momba katika kabwela bado kilio ni hicho hicho........

5. Stamina naye na Rich Mavoco bado wanalia na ukabwela...

6. Top C naye analamikia Ulofa wake anaona ndo sababu ya kukataliwa...

7. hata ukisikiliza Vumilia ya University Corner(UVC)...bado kilio ni kile kile

8. Kuna huyu mwingine sijui anitwa nani...aliyetuimbia "Anarudi kijijini".. kumbuka .wakati anakuja mjini hakusema....naye kilio chake ni hicho hicho.

Haina ya nyimbo za namna hii ndizo zimekuwa zikivuma sana mtaani..na unaweza ukaongeza unazozifahamu

NIONAVYO.........

1. HALI YA MAISHA YA MTANZANIA NI NGUMU NA INAONEKANA WANAUME WENGI WAMEKATA TAMAA YA MAISHA, WANAAMINI MAPENZI NI PESA NA INAWEZEKANA HAWATAKI AU WAMESHINDWA KUZITAFUTA

2. AKINA DADA WAMEKUWA KIMASLAHI ZAIDI...WAMEACHA UTU NA KUJALI PESA ZAIDI...HAPA UKICHUNGUZA HATA WALE WANAODAI KWAMBA WANAPENDWA SANA..UNAKUTWA KINACHOPENDWA NI PESA NA SI WAO.

3. WENGI WANASHINDWA KUTAFUTA WATU WA AINA YAO..KWA MAANA WANAOFANANA NA HALI ZAO

SULUHISHO

KUENDELEA KULALAMIKA TU HAITOSHI(KUMBUKA HAWA WASANII NI MIONGONI MWETU NA WANAWASILISHA MAWAZO YETU NA MAISHA YETU YA KILA SIKU).

KAMA PESA NDIZO ZINAZOPENDWA, NAWE UNAHITAJI KUPENDWA BASI UNATAKIWA KUTAFUTA PESA ILI KUEPUKA KULAUMU WENGINE KWA JAMBO LINALOJULIKANA

ITAENDELEA.....
 
Sidhani ni kwa kila dada anayekuwa hivo....yani money over everything sikatai kwamba wapo....but sidhani kwa mtu mwenye akili yake anaweza akasema leo nikatafute fukara atanipenda zaidi ya yule mwenye hela..itakula kwako...afterall LOVE WONT PAY THOSE BILLS. ni mtazamo wangu and zaidi ni kitu nilichojifunza.....tena wasumbufu kuliko wote ni hao wasio na hela.
 
Ulizoandika hazifiki hata 10% ya bongo fleva

mkuu ulitaka niorodheshe zote? Nina uhakika ni zaidi ya 80% za mapenzi ni za kulalamika kuhusu pesa sikiliza

Mbona-PNC

Uje kidogo-Pasha

Mazoea-Pete

Rudi-PNC

hayakuwa mapenzi-sugu
mtu na pesa-afande sele
si ulinikataa-solo thang
usiniache-chelea man
thamani ya penzi-pasha
vumilia-smasho
tamika -dully sykes
mpenzi kwaheri-jmoe
asha-TID
mbagala-diamond
nalia na mengi-diamond
unikimbie-amini
sifai-Q-jay
kizunguzungu-abdu kiba
 
kwani ni sehem gani mtanzania halalamiki.!maisha ya mtanzania lawama tu.
 
Raisi analalamika, waziri mkuu analalamika mpaka kulia, mawaziri wanalalamika( mkumbuke nundu,wasira, kombani, mkulo, ngeleja nk) mabalozi wanalalamika, makatibu wanalalamika, walimu, macashiers, wahasibu, madokta, makayumba!
Damn! Nchi nzima wanalalamika
 
Back
Top Bottom